Nimetangaza nia ya kugombea Udiwani!

Naweza kuja kukusaidia kufanya kampeni niko tayari kutoka hapa dar nije kwa sababu lameck na ochere awana uwezo wa kuiongoza rorya nakuleta maendeleo hilo linajulikana kabisa cha msingiiiiii kama unanitaka nitakuja na team yangu nzima mpaka hapo tufanye mambo tutakupa spport kubwa sana kwa sababu hata mimi nimenunua tender hapo ili niwe na service computer za halmashauri najua kwa ubinfsi wa ochere na lameck kwa nafasi zao inawea kuwa kikwazo kikubwa sana kwa sababu wana watu wao ambao watawaleta, wasiliana na mimi kwa pressdown@hotmail.com

Pamoja sana mkuu

Rai yangu kwako ni kwamba usifanye siasa kama njia ya kutokea,inahitaji moyo mkuu wa upiganaji hasa katika CHADEMA

Usijefanya makosa yoyote kama walivyofanya jamaa zetu 5 wa AR

Hongera sana Mkuu.If you need my support dont hesitate to communicate ila ni baada ya kura za maoni.Nakutakia ushindi mwema...

cdm imeleta mwamko mkubwa kwa vijana na faida tunaiona bungeni wazee majasho na majotroo kibao,nenda kijana tuwachape bungeni hadi mtaani!

wazee kule wanalalamika eti hawapewi shikamoo na akina wenje,Lema! Naomba upate nafasi ili wajue kimenuka rasmi,si bungeni si kitaa! Wajistaafishe!

we ni taila coz m2 anaomba mchango co majunguo huna mchango kaa kimya upo!lione na nahic we fisadi
Diwan mtarajiwa kaza but hz kele2 za chura

wazee kule wanalalamika eti hawapewi shikamoo na akina wenje,Lema! Naomba upate nafasi ili wajue kimenuka rasmi,si bungeni si kitaa! Wajistaafishe!

wanawasingizia tena wenje mbunge wangu nyamagana mwz anaheshima bwana bac 2hao wazee wanajistukia na ufisadi wao
nawapa hekoo!Lema,Wenje,n.k au we unawaonaje vjana
wam

Nawashukuru sana kwa jinsi mnavyozidi kunipa moyo. Naamini kuwa maombi yenu yatanifanikishia ushindi!
Tuzidi kuombeana na kutakiana kila la heri. Tuko pamoja!

Ndugu, jamaa na marafiki wa JF habarini za saa hizi? Mimi sijambo!
Mimi, Ndege Edward S. Jacaduogo nimeamua kwa dhati kabisa bila kushinikizwa na mtu yeyote kugombea udiwani kata ya Nyahongo liliko jimbo la Rorya mkoani Mara kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)!

Hii ni kutokana na kujiuzulu kwa madiwani watatu wa kata tatu tofauti jimboni Rorya kuanzia December 2010 kutokana na maslahi ya kisiasa ndani ya CCM katika harakati za kuwania uenyekiti wa halmashauri ya Rorya. Kama nilivyowahi kueleza hapa JF kuwa madiwani watatu hao waliojiuzulu walikuwa kama wafuatao:

1. Ndugu Ambogo wa kata ya Nyahongo (CCM)

2. Ongujo Wakibara wa kata ya Mkoma (CCM)

3. Okeya Ogigo wa kata ya Nyamtinga (CCM).

Kampeni zinaanza tar 07/09/2011 na kura ni tar 02/10/2011 lakini mpaka sasa watu bado wanaendelea kuchukua fomu na wa CHADEMA tayari wamechukua fomu wanne na mwisho wa kuchukua fomu CHADEMA ni tar 24/08/2011. CCM wamechukua watano na mwisho ni leo jumapili 14/08/2011.

Mimi ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) 2011 katika mchepuo wa usimamizi wa biasha (BBA). Nilikuwa mwanaharakati na mwanachama mzuri wa CHADEMA na nilikuwa muwakilishi (CR) wa BBA kwa muda wa miaka mitatu.

Kwa heshima na taadhima na kwa dhati kabisa naombeni ushirikiano wenu na michango yenu ya kimawazo!
Tuko pamoja.

Kwa pamoja tutashinda kwani tunaamini katika Nguvu ya Umma.

Kwa pamoja tushikiane kutokomeza ufisadi na manyanyaso na udhalishaji wa kila namna!

Naomba kuwasilisha....
What?... yaani watu wamejiuzulu Udiwani kwa sababu ya maslahi ya kisiasa ndani ya CCM ktk Uchaguzi wa MEYA?.Duh! kumbe ya Arusha cha mtoto na naanza kuipata picha ya kiburi cha madiwani!

Haya mkuu wangu JACADUOGO2 maadam umeshachukua form jitahidi ktk ushawishi na muhimu zaidi UMAARUFU wako hapo Nyahongo.. wapambe wako lazima waifanye kazi ya ziada kwa sababu kata hiyo ilikuwa ya CCM, hivyo sii swala la kuokota kata iloachwa ila kunahitajika nguvu ya ziada kuwashinda CCM..

Ndugu hongera sana kwa uamuzi sahihi uliouchua, Sasa tunataka wahitimu wa vyuo tujikite kwenye udiwani zaidi na si ubunge peke yake ili tuweze kuharakisha upatikanaji wa maendeleo, Usisikilize magamba wa humu wanasemaje, Hongera hongera sana, Hata mm nimemaliza chuo mwaka huu degree ya uhasibu na 2015 nami nagombea udiwani Kata ya kasulu mjini kupitia CHADEMA.

Big up

Hongera sana,kwa kuchukua UAMUZI MGUMU SANA. katika ngazi ya udiwani wengi huwa siyo Graduates wa Chuo kikuu,huo ni uamuzi mgumu tayari,kwan utakutana na Mwenyekiti wa Halmashauri mwenye elimu chini yako,na bila shaka madiwani vivyo hivyo,kwa elimu yako tu ,watajenga chuki.

Ngazi ya Diwani ni ngazi muhimu sana kuliko Ubunge kwa Jamii,kwani wewe utakuwa unasimamia utekelezaji wa maamuzi ya Bunge na matumizi ya serikali.kimsingi Tunahitaji Madiwani Wasomi kuliko Wabunge wasomi.cha kushangaza Madiwani wetu wengi siyo wasomi,hivyo basi kila siku wanakuwa na mikwaruzo na Wataalam wa Halmashauri+ mkurugenzi.ila Tukiwa na Wataalam Wasomi,Madiwani Wasomi,hata maamuzi ya Halmashauri yatakuwa makini Zaidi.

Nakuunga mkono,na nitakupa Mchango wangu wa mawazo ktk Kampeni Zako.Kwa kuanzia piga kampeni kisasa zaidi,angalia jinsi gani unaweza kutumia Simu ya mkononi kama Campaign Tool .
1-Andaa mfumo wa kukusanya Namba za simu.
2-Kukusanya Maoni kwa mtandao wa simu
3-kupata michango kwa mtandao wa simu.

Kila la Kheri

Stay away from gutter politics and ad hominem arguments. Be servant not master... People's problem is your capital.

All the best if you can follow this principle!

2gether m2 wangu u make the right choice at the right time don't loose hope u'll win

kawaambie wakurya wenzako huko sisi siowapiga kura wako. kama wapo basi utakuwa wewe na wengine wawili tu. sioni tija ya uzi wako hapa. au ndo madhara ya kusoma chuo cha kata?

Haters kama ninyi unakuta ni wana CCM, uwezo wa kufikiri ni duni!

kawaambie wakurya wenzako huko sisi siowapiga kura wako. kama wapo basi utakuwa wewe na wengine wawili tu. sioni tija ya uzi wako hapa. au ndo madhara ya kusoma chuo cha kata?

Tatizo lako umeanza kutumia mitandao hii juzi.

Back
Top Bottom