Nimetangaza nia ya kugombea Udiwani!

Kila la heri mpiganaji wetu, vijana ndio nguzo kwenye harakati ya kulikomboa taifa letu mikononi mwa wakoloni weusi/mafisadi, tuko pamoja ila jitahidi kuwashawishi watu wa huko kwa hoja nzito zenye kujenga. Mtaji wa kijana kwenye siasa ni uwezo wake wa kujenga hoja za maana na kuzisimamia. Kila la kheri.

Nakupongeza sana kwa kuzichukua harakati za ukombozi wa mtanzania kwa vitendo kwa kusimama ktk uchaguzi ili kukabiliana na wana maghamba tunataka watu kama nyie ili nchi hii ikombolewe kwani it is time to get off the side line and get involved to liberate our country piece by piece.

Big up and god protect you.

Nenda mkuu,ukifanikiwa jitahidi kuifanya halmashauri kuwa ni chombo cha utumishi wa umma huku ukiimarisha D by D kwa maendeleo yenu. Nenda kiongozi, yes we can.

Ndugu, jamaa na marafiki wa JF habarini za saa hizi? Mimi sijambo!

Mimi, Ndege Edward S. Jacaduogo nimeamua kwa dhati kabisa bila kushinikizwa na mtu yeyote kugombea udiwani kata ya Nyahongo liliko jimbo la Rorya mkoani Mara kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)!

Hii ni kutokana na kujiuzulu kwa madiwani watatu wa kata tatu tofauti jimboni Rorya kuanzia December 2010 kutokana na maslahi ya kisiasa ndani ya CCM katika harakati za kuwania uenyekiti wa halmashauri ya Rorya. Kama nilivyowahi kueleza hapa JF kuwa madiwani watatu hao waliojiuzulu walikuwa kama wafuatao:

1. Ndugu Ambogo wa kata ya Nyahongo (CCM)

2. Ongujo Wakibara wa kata ya Mkoma (CCM)

3. Okeya Ogigo wa kata ya Nyamtinga (CCM).

Kampeni zinaanza tar 07/09/2011 na kura ni tar 02/10/2011 lakini mpaka sasa watu bado wanaendelea kuchukua fomu na wa CHADEMA tayari wamechukua fomu wanne na mwisho wa kuchukua fomu CHADEMA ni tar 24/08/2011. CCM wamechukua watano na mwisho ni leo jumapili 14/08/2011.

Mimi ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) 2011 katika mchepuo wa usimamizi wa biasha (BBA). Nilikuwa mwanaharakati na mwanachama mzuri wa CHADEMA na nilikuwa muwakilishi (CR) wa BBA kwa muda wa miaka mitatu.

Kwa heshima na taadhima na kwa dhati kabisa naombeni ushirikiano wenu na michango yenu ya kimawazo!

Tuko pamoja.

Kwa pamoja tutashinda kwani tunaamini katika Nguvu ya Umma.

Kwa pamoja tushikiane kutokomeza ufisadi na manyanyaso na udhalishaji wa kila namna!

Naomba kuwasilisha....

kaka kwanza nakupa pongezi kwa hatua uliyofiki.pili ukipata udiwani usiende tu kwasababu siasa inalipa bali nenda kasimamie halmashauri ili miradi iliyopangwa iweze tekelezwa.mwisho nilikuwa naomba utuweke majina ya wanachadema wanaoenda kugombe katika izo kata kwa hata st agustine kulikuwa na wanaharakati wengi wanaolitaka jimbo la rorya.

sasa ulikuwa unataka nini?Mchango? Nenda kawajulishe watakao kupigia kura sio sisi. Mijitu mingine bana
Naona umetoka chooni bila kuchamba kwa kusikia harufu ya ubwabwa!!
rudi kachambe kwanza.

hapo nakupa tano, mwanangu. naona kama umeshashinda maana hao wakurya lazima wakigeuke hicho chama cha magamba. kaa nao hao magamba walojiudhuru hakikisha wanakuwa upande wako na watakuletea wapigakura waliowachagua wao. ukichanganya na wapiga kura wa cdm, hapo magamba itakuwa imekula kwao.

Nenda kaka nenda. Tuko nyuma yako kwa sala na maombi. Mungu akujalie shauku ya moyo wako kama uko tayari kweli kusaidia wana Rorya. usiwe kama wale madiwani wa Arusha waliofukuzwa kwa kutokuwa na nidhamu. Nenda kwa nia ya kutumikia wananchi.

Welldone dude !hakikisha unayajua matatizo ya Rorya vizuri kwani ni mtaji wako kisiasa!

Wananchi wako ndiyo wanaokufahamu kama unaingia kimaslahi binafsi au kwa maslahi ya umma

Nakutakia kila la heri kwenye safari uliyoanza. Kumbuka kuwa cheo ni dhamana, na uitumikie nchi kwa faida ya wote!

Naomba utuambie ndani ya chama unagombea wewe na akina nani kwenye hiyo kata ili waliopo huko watoe michango yao hapa kwa ulinganifu. Au umepita bila kupingwa?

Hongera sana mkuu,nikutie Moyo tu endelea na harakati hizo na utashindwa ila lolote litakalokutatiza lilete hapa Jf upate ushauri mahususi wala wasikukatishe hawa vibaraka wa Magamba ambao wapo humu ndani wewe pokea michango inayokufaa wala usibishane nao

Ndugu, jamaa na marafiki wa JF habarini za saa hizi? Mimi sijambo!
Mimi, Ndege Edward S. Jacaduogo nimeamua kwa dhati kabisa bila kushinikizwa na mtu yeyote kugombea udiwani kata ya Nyahongo liliko jimbo la Rorya mkoani Mara kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)!

Hii ni kutokana na kujiuzulu kwa madiwani watatu wa kata tatu tofauti jimboni Rorya kuanzia December 2010 kutokana na maslahi ya kisiasa ndani ya CCM katika harakati za kuwania uenyekiti wa halmashauri ya Rorya. Kama nilivyowahi kueleza hapa JF kuwa madiwani watatu hao waliojiuzulu walikuwa kama wafuatao:

1. Ndugu Ambogo wa kata ya Nyahongo (CCM)

2. Ongujo Wakibara wa kata ya Mkoma (CCM)

3. Okeya Ogigo wa kata ya Nyamtinga (CCM).

Kampeni zinaanza tar 07/09/2011 na kura ni tar 02/10/2011 lakini mpaka sasa watu bado wanaendelea kuchukua fomu na wa CHADEMA tayari wamechukua fomu wanne na mwisho wa kuchukua fomu CHADEMA ni tar 24/08/2011. CCM wamechukua watano na mwisho ni leo jumapili 14/08/2011.

Mimi ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) 2011 katika mchepuo wa usimamizi wa biasha (BBA). Nilikuwa mwanaharakati na mwanachama mzuri wa CHADEMA na nilikuwa muwakilishi (CR) wa BBA kwa muda wa miaka mitatu.

Kwa heshima na taadhima na kwa dhati kabisa naombeni ushirikiano wenu na michango yenu ya kimawazo!
Tuko pamoja.

Kwa pamoja tutashinda kwani tunaamini katika Nguvu ya Umma.

Kwa pamoja tushikiane kutokomeza ufisadi na manyanyaso na udhalishaji wa kila namna!

Naomba kuwasilisha....
kawaambie wakurya wenzako huko sisi siowapiga kura wako. kama wapo basi utakuwa wewe na wengine wawili tu. sioni tija ya uzi wako hapa. au ndo madhara ya kusoma chuo cha kata?

Back
Top Bottom