Nimesikitishwa sana na kibonde na clouds fm kuhusu mbunge nasari

ivi hawa jamaa wa clouds mi nlisha wapotezea kitambom sana, ni magamba
 
Wanajf,
nimesikiliza kipindi cha jahazi cha clouds fm ambapo leo topic ilikuwa inahusu hotuba ya mbunge joshua nasari. Kilichonisikitisha sana ni kauli ya kibonde kuhusu nasari. Kibonde ameonekana kama kesha muhukumu nasari na anachoamini kwake ni kwamba nasari haweyi kupewa nafasi yoyote ya kusikiliywa kwasababu ya kauli yake. Kibonde anasema na kusisitiza kwamba anayepaswa kupewa nafasi ya kuelezea jambo hili ni mwanasheria tu na nasari hana haja ya kupewa nafasi japo watangazaji wenzake wamejaribu kumsisitiza kwamba kuna haja ya kumsikiliza nasari naye lkn kibonde anaonekana tayari ana majibu ya kitu gani kifanyike kuhusu nasari. Na hapo ndipo ninapokosa logic ya kwanini wanamwita mwanasheria redioni wkt kibonde tayari ana majibu.

Je ni ufafanuzi upi zaidi anaohitaji kutoka kwa mwanasheria?

Je ni mara ngapi tumewahi kusikia kauli kama hizi ktk tanzania? Je kuna haja ya kutoa hukumu kabla ya muda?

Nawasilisha.
Telo.
Mkuu pole sana!....acha nikuambie kitu cha ukweli kabisa bila kumung'unya maneno.
Cloudz media wamechagua upande mbaya sana wa historia na future ya media yao.
Ukiwasikiliza baadhi ya watangazaji wao(mfano ni huyu Kibonde) na baadhi ya vipindi
vyao vya kila siku utagundua hii Radio na Tv yao vipo kwa hajili ya CCM. Wenyewe
wanasema eti hii radio ni ya vijana...lakini ukiwafatilia between the line utagundua hii
media siyo ya vijana wala nini,bali ni radio ya wapenda sifa na ushabiki kwa CCM tena
waziwazi. Binafsi nawapenda sana Cloudz ila nawaonea huruma kwa kushindwa kusoma
alama za nyakati...kwani iwe isiwe jahazi la CCM linazama kweupeeee! Time will tell.
BACK TO THE TOPIC....Ni kweli Nassari alikosea,lakini mwenyekiti wa chama alishalitolea
ufafanuzi ila baadhi ya watangazaji wa Cloudz wanatumiwa na CCM!...yetu macho,time
will tell
 
Naminimemskia naomba kufahanu katika kampeni za Arumeru kina hata suku moja walimlusha kama mgombea? Na kauli za lusinde walisga hata play katika kipindi chake cha jahazi?

Kuhusu kauli za Lusinde kipindi cha Jahazi Kibonde aligoma kuiplay ile script kwa mantiki kwamba ilikua na kauli chafu zisizofaa kuekwa na kusikilizwa na Umma; lakini kwenye Power Breakfast iliekwa wazi. Kimsingi kauli zote za wabunge hawa Lusinde na Nasari si nzuri kwa lengo la kuijenga Nchi.
 
Mimi hao Clouds nimeacha kusikiliza mara ya mwisho nimesikiliza 2006 hadi leo ctaki kuisikiliza radio ya magamba hiyo ndo maana hata Masoud Kipanya aliwakimbia ili awe free.
 
Mimi naona wale wadudu wake wameshaanza kupanda kichwani... Mtu makini hawezi kuropoka kama mtoto anayejifunza kuzumgumza!!! KAMA NIPIGE TAFU ZAKE ZIMEMUISHIA MWAMBIE aende TUMAINI AU St. BENARD WANAGAWA BURE!
 
Kibonde ni gamba la kichovu na ndiyo linajipenyeza kwenye issue ya Mh:saaaaana. Akiibuka kitaa 0718yake inapigwa mgawo.
Muipige mgao hamjitaki??? Msimsikie tu kwenye hilo likipindi huyo kwisha kazi.........!
 
Kibonde daima hana akili, kuna haja ya kumjadili?
Kuna mwandishi gazeti la Ijumaa kamchambua vema sana kwenye matoleo ma3 mfululizo.
 
uharibifu umeshatokea...cdm inatakiwa iichukulie hii kitu positively kwa kuwasimamia vizuri vijana wao wanaopata uongozi wa kisiasa...!
 
Jamani si mwingine ni zaidi ya Ephuraim Kibonde.

Mi sijampenda kbs kutokana na maongezi yake ya kila mara ktk kipindi cha jahazi kinachorushwa na Clouds Radio kila siku na mara zote akiwepo hakika anazoza mbovu sana hasa kutetea mafisadi na kuwapinga wasema haki.

Mi amenijengea nimchukie mbaya mbovu!

Simpendi kbs! Acha niweke wazi ya kwamba namchukia kuanzia sasa!

Shwain sana!!
 
Uwongo ukizungumzwa sana huonekana ni ukweli.
Tusilalamike bila suluhsho, tumtafutie majawabu ili kukomesha tabia yake.
 
U must be crazy!! hii ni live from nafsini mwangu!

umewahi kumsikia mara ngapi?? na siku nyingine ambayo ndio uliyojua jina lake mbona haukulalamika??

Hivi mtu akiwaza tofauti na wewe au au akiwa na mtazamo mwingine ndiyo unamchukia?? hauoni unajidhalilisha mkuu!!

nyie ndiyo mnakuwa wanoko kwa familia zenu, mnawalazimisha watoto wenu washabikie timu zenu na wake zenu kufuata kila mnachosema, hizi ni character za kidikteta na ubinafsi uliokubuhu ambao unausema bila aibu...simply kwa sababu kuna watu wenye akili kama wewe watakupa support..u know that


sasa ni hivi, nitakuuliza maswali mawili matatu ya kiume na uyajibu

ni lazima usikilize hiyo radio??

je unajua jahazi, kibonde ni mmoja wao unapomsikiliza unategemea nini? na kama unataka aseme uwazavyo wewe kwa nini usimwajiri??

hivi unapoandika humu unataka iweje?? Kibonde atakusikiliza??

unajua chuki huondoa busara na emotion uleta aibu!!

Leave Kibonde alone...amezaliwa na kuumbwa na Mungu kama wewe

Kibonde yuko so genuine kwa anachokisema, mara nyingi amelaumu sana serikali na utendaji wake wa kazi, tena huwa anawatukana wakati mwingine. akitetea mafisadi ni yeye pia! mpotezee sio kuleta ujinga wako humu ukidhani kila mmoja anawaza kama wewe!

si bora anayewasupport kwa uwazi kuliko wengi wenu mko kimya kimya na mara ....hamad! mnakuwa wakuu wa wilaya!! wako sabini wapya hakuna unayemsema humu...ila umemsikia kibonde!!!Think
 
Jamani si mwingine ni zaidi ya Ephuraim Kibonde.

Mi sijampenda kbs kutokana na maongezi yake ya kila mara ktk kipindi cha jahazi kinachorushwa na Clouds Radio kila siku na mara zote akiwepo hakika anazoza mbovu sana hasa kutetea mafisadi na kuwapinga wasema haki.

Mi amenijengea nimchukie mbaya mbovu!

Simpendi kbs! Acha niweke wazi ya kwamba namchukia kuanzia sasa!

Shwain sana!!

Labda alikuwa anatafuta u DC sasa hivi atajirekebisha.
 
Acha kusikiliza hicho kipindi ama redio station yenyewe,au kama vipi fuata stail ya Iringa ili nafsi isiumie zaidi!
 
Back
Top Bottom