Nimesikitishwa sana na kauli hii ya mkoa wa dsm

Mulangila Mukuru

JF-Expert Member
Feb 24, 2010
1,945
724
Akiongea ITV leo jioni Mkuu wa mkoa wa DSM amedai kuwa serikali itaongea na kampuni ya AZAM MARINE ili watanzania bara waliopoteza ndugu zao kwenye ajali ya meli Zanzibar ili kesho au keshokutwa waweze kwenda Zanzibar kwa gharama zao waone kama watawatambua ndugu zao. Jambo hili ni aibu kwa serikali inayojiita makini kushindwa kutoa hata msaada wa usafiri kwa wafiwa ili wakajaribu kwenda kuona kama wanaweza kupata miili ya ndugu zao
 
hiki kilio kwa serikali yetu kitajibiwa na mwenyezi Mungu...!
Nimesikitika sana baada ya kupata taarifa kuwa meli ilikuwa chakavu na ilinunuliwa marekani baada ya kushindwa kutoa huduma za usafiri huko Marekani...dah
 
Serikali ambayo haijifunzi kukokana na majanga yanayotokea.
Ilikuwa mabomu ya Mbagala, baada ya mwaka mmoja tu yakaipuka mabomu kama yale Gongo la mboto.
ajali kama hiyo ilitokea hata mwaka haujapita, leo inatokea tena ajali kama ile ile.
 
ongeza na mgomo wa madaktari uliotokea mara tatu bila ufumbuzi.
Nionavyo tatizo ni wananchi wanaoshindwa kuiwajibisha serikali.
 
ongeza na mgomo wa madaktari uliotokea mara tatu bila ufumbuzi.
Nionavyo tatizo ni wananchi wanaoshindwa kuiwajibisha serikali.
mkuu nadhani wakati umefika sasa wa mimi na wewe kuchukua hatua zinazostahili. Tuanzie wapi?
 
mkuu nadhani wakati umefika sasa wa mimi na wewe kuchukua hatua zinazostahili. Tuanzie wapi?

njia ambayo mimi huwa naitumia kila ninapofika kwenye mkusanyiko basi huwa najitahidi kuanzisha mada juu ya maisha magumu halafu na hakikisha nawaelimisha walioko hapo uozo wote wa ccm naamini 2015 hawang'oki..
 
Moja ya Kero za muungano,

Hizi ajali za baharini mara zote zinasababishwa na meli zilizosajiliwa huko Tanzania visiwani (Zanzibar). Linapokuja suala la kusajili meli za kubeba mafuta za Iran wanasema si suala la muungano linapokuja suala la uwajibikaji baada ya ajali watasingizia Muungano...

Enough is enough, Ile mamlaka inayosajili vyombo vya baharini huko TZ visiwani ivunjwe mara moja, ikishindikana basi meli zote zinazosajiliwa huko TZ visiwani lazima zisajiliwe tena tz bara kabla ya kutoa huduma yeyote...:hat:
 
Back
Top Bottom