Nimesikitishwa na Watanzania!

Kila kitu kimesimama! Barabarani hakupitiki, watu hawafanyi kazi kisa kifo cha Steve Kanumba. Ninaangalia TV watu wengi wapo leaders kumzika SK! Hilo taifa ni la wajinga Kama viongozi wake! Watu wote Hawa walio leaders hawazalishi kitu! Taifa maskini na wananchi wake maskini vichwani. Lowassa nadhani hakuhangaika na Huu msiba wa kisanii

RIP Kanumba

Rt Rev Masa

...ama kweli duniani kuna watu na viatu.....
 
...ama kweli duniani kuna watu na viatu.....
Una maana gani? ni uzembe uliopitiliza watu kujazana Leaders badala ya kujikita kwenye uzalishajimali, si wote ambao wako pale kwamba ni kweli wanaomboleza. siamini hilo na hata siku moja siwezi kufuata Mkumbo wa kwenda kwenye msiba wa mtu ambaye sikuwahi kufahamiana naye na wala siyo Kiongozi wa Kitaifa.
 
mvua za masika hazinyeshi .... watanzania tunafanya juhudi gani kukabiliana na hii changamoto ya kuendelea kusubiri mvua kwenye kilimo kwa kudra za mwenyezi mungu
 
hawa viongozi wetu wa serikal,
kwenye msiba wa dr remmy ongala mbona hawakujitoa sana kama huu?
 
Utakuwa umelogwa wewe AMA unapepo! I'm talking from economic point of view! Ujinga Huu watz hao walio leaders hajafanya kazi yeyote ya kuzalisha

Kweli kabisa leo nakuunga mkono Masanilo, wabongo wavivu wa kufikiri! Yani mijitu imeacha uzalishaji kabisaa! Nachoka.
 
hawa viongozi wetu wa serikal,
kwenye msiba wa dr remmy ongala mbona hawakujitoa sana kama huu?

kila jambo na wakati wake mkuu, yawezekana leo akafa msanii mwingine watu wakaw mara 100 zaidi ya hawa waliohudhuria msiba wa Kanumba, hata wakati wa msiba wa Dr Remmy tulisema watu walikuwa wamefurika..

all in all watanzania ni wavivu sana badala ya kuzalisha wameenda misibani, na kuna washikaji wamesafiri kutoka Iringa mpaka Dar kuja kuhudhuria mazishi yaani wameacha vipindi chuoni kisa msiba
 
Khaa jamani mbona kufuru namna hiyo kwahiyo ulitaka watu wasiende kuzika?wangekosekana napo mngesema sasa sijui mnataka iweje?yamepotea mabiloni mangapi hata leo mlalamikie umati ulioenda kumzika kanumba yaani binadamu wana hila kama kkikwapa kunuka bila kidonda acheni hizo.
 
Kuhangaika na misiba ni jadi yetu Waafrika na Kanumba (RIP) bila shaka alikuwa na umaarufu mkubwa kwa Watanzania wenzetu wengi. Lakini ukweli mwingine uliopo hapa ni wa wajanja wengi kupata fursa "adhimu" ya kujipa ujiko katika msiba huu. Hawawezi kuiacha ipite hivihivi. Na kama kawaida yao kila mkulu lazima akauze sura na kujinasibu hapo (penye umaarufu) kama vile itafidia utendaji duni kwenye majukumu yake ya msingi; kama vile alikuwa na mchango wowote wa maana katika umaarufu aliofikia bwana mdogo huyo. Sie wengine tungefurahi kuona hamasa ya aina hiyohiyo katika masuala yote muhimu ya kitaifa - hata katika kuikuza sanaa nchini.

au kupiga kura...
 
As a matter of facts nimeguswa na msiba wa SK na pia hatma ya Lulu kama binadamu ambaye bado yupo hai,na pia kila nafsi ingependa kuzikwa vema.
ila naona kama watz tumezidisha,nakumbuka msiba wa Michael Jackson ulikuwa na Motorcade ya magari matatu tu..wengi walishuhudia kwa Television na other media coverages
How comes mtu yupo pale leaders saa kumi na moja na nusu alfajiri? Nimeamin kweli watz wengi ni maJobLess na walio na kazi zao pia hawazipendi
Ina maana Everybody anataka kuonekana maana sio kushiriki...tunasubiri taarifa za kuzimia na kudondoka mitini maana hilo eneo halitoshi waombolezaji wengi sembuse makaburi yenyewe tunazikiwa juu ya wafu wenzetu waliozikwa kitambo na kusahaulika
Nchi imekuwa ya kisanii na hadi sasa inaongozwa na wasanii kimaigizoigizo
RIP SK..poleni wafiwa na mimi mwenyewe!
 
Kila kitu kimesimama! Barabarani hakupitiki, watu hawafanyi kazi kisa kifo cha Steve Kanumba. Ninaangalia TV watu wengi wapo leaders kumzika SK! Hilo taifa ni la wajinga Kama viongozi wake! Watu wote Hawa walio leaders hawazalishi kitu! Taifa maskini na wananchi wake maskini vichwani. Lowassa nadhani hakuhangaika na Huu msiba wa kisanii

RIP Kanumba

Rt Rev Masa

Rev. Wenzio wanashindana nani kalala kwenye msiba wa kanumba tangu utokeee
Ni kweli inauma ila tuliobaki bado tunatakiwa kufanya kazi tuishi!
RIP Kanumba
 
kila jambo na wakati wake mkuu, yawezekana leo akafa msanii mwingine watu wakaw mara 100 zaidi ya hawa waliohudhuria msiba wa Kanumba, hata wakati wa msiba wa Dr Remmy tulisema watu walikuwa wamefurika..

all in all watanzania ni wavivu sana badala ya kuzalisha wameenda misibani, na kuna washikaji wamesafiri kutoka Iringa mpaka Dar kuja kuhudhuria mazishi yaani wameacha vipindi chuoni kisa msiba

Hapa unanikumbusha jana wakati naangalia ITV news saa 2 usiku eti kuna mashabiki wametoka Zanzibar kuja tu kuipokea Simba ambayo ilifungwa 3-1 kule Algeria lakini ikapata tiketi ya kuingia raundi ya pili kwa favour ya Aggregate results!!
Hii nchi imejaa uzembe imefika wakati sasa namuunga mkono yule DC aliyeamuwa kuwachapa bakora walimu wa ile shule kule Bukoba, bila viongozi wa aina ile hii nchi haitokwenda popote.
 
Nilipoona JK ameenda sinza kuhani msiba wa huyu muhuni Kanumba nilishangaa sana lakini sikusikitika kwani hulka na tabia ya huyu mkw.er.e inaelewa.
Lkn hili swala la kumzika huyu muhuni, ambaye ameauwa na kicheche Lulu, kufanywa msiba wa kitaifa, limenikera na kuniudhi sana.
Nchi hii imejaa mambumbumbu sana, umaskini tuliona nao tunastaili kabisa.
Watu wanaacha shughuli zao, barabara zinafungwa, kisa mzinzi amefariki, shame on us watz..
 
Binadamu wengi akili haziko sawa nadhani sio Watanzania tu kuna watu walienda kujazana kwenye mazishi ya Whitney Houston pamoja na kwamba waliishia kwenye police line yaani walikuja na viti kabisa wakawa wamechill.
 
Inabidi uelewe kwamba kwa wasanii wa television na sinema, kuwaangalia kila siku unajenga uhusiano nao japo hawakufahamu, na uhusiano huu unakuwa mkubwa sana kama vile ni rafiki zako wa karibu. Ndio kinachowapa hawa wasanii "celebrity status". Hivyo wanapokufa watu wengi huhisi kupoteza mtu wa karibu sana. Mifano halisi ni watu walivyohisi juu ya kifo cha Michael Jackson, Bob Marley, Whitney Huston, Bruce Lee nk. Hivyo usishangae kuona shughuli zimesimama kwa ajili ya mazishi ya Kunumba.

Tanzania inavyo pigika kiumaskini jibu lake limejibika leo. Taifa letu lina wajinga wengi, wasio na kazi za maana lina viongozi wengi wanaitwa wa kitaifa wasio na maana na wanajishughulisha na vitu vya ovyo, eg Rais kwa huo msiba, badala ya kua dress kwanini mafuta ya petrol yamepanda kutoka sh1,940 kwa lt kuwa 2,331 kwa litre. Ama kwanini umeme unakatika bila wateja kutaarifiwa. Mi najikana kuwa mtanzania kwa huu ujinga ninaouona.
 
Kila kitu kimesimama! Barabarani hakupitiki, watu hawafanyi kazi kisa kifo cha Steve Kanumba. Ninaangalia TV watu wengi wapo leaders kumzika SK! Hilo taifa ni la wajinga Kama viongozi wake! Watu wote Hawa walio leaders hawazalishi kitu! Taifa maskini na wananchi wake maskini vichwani. Lowassa nadhani hakuhangaika na Huu msiba wa kisanii

RIP Kanumba

Rt Rev Masa

Kwa kweli inasikitisha, Watanzania tunatakiwa tutafakari, ndo kusema watu hawana kazi za kufanya. Tujifunze kutoka kwa mataifa yalioendelea. Jesus aliwahi kusema ''Waache wafu wakawazike wafu wenzao''
 
Sidhani kjipangia hutofautiani na mnyama, na kama uliweka thread hii ili ujue tutachangia nini
 
Kwa kweli inasikitisha, Watanzania tunatakiwa tutafakari, ndo kusema watu hawana kazi za kufanya. Tujifunze kutoka kwa mataifa yalioendelea. Jesus aliwahi kusema ''Waache wafu wakawazike wafu wenzao''
Ripoti kutoka makaburi ya Kinondoni mazishi yameshakamilika muda huu ila watu hawataki kuondoka!!......wengine wanahojiwa na mwandishi wanasema eti ilibidi mwili wa Kanumba ukae siku 3 pale Leaders ili waage vizuri, namuhurumia sana mtu anayetamani kuwa Rais wa Nchi kama hii, sidhani kama wana takwimu sahihi ya nchi yao ilivyojaa mambumbumbu na wasiojuwa hata kwa nini wapo Duniani.
 
Back
Top Bottom