Nimepoteza hamu kwa mke wangu,nifanyaje?

mkuu Attache nakupongeza sana kwa kuwa mkweli sana na kutuonyesha uhalisia ambao watu wengi huukataa ama huona kama dhambi kuukiri kwamba wanapita katika hali hiyo.

kwanza nakutia moyo si jambo la ajabu kwa mtu na mkewe kupotezeana hamu. hali hii hutokana na sababu nyingi sana na nitajaribu kusema chache nyingine wadau wataongezea.

1) kukinai- kama ambavyo mtu akila menu moja mara nyingi hukinai kadhalika na wapenzi hukinaiana hali hii usipokuwa makini nayo unaweza kujikuta unakwenda kutafuta ladha tofauti nje na ya hapo kwako. ni vyema ukajua hili kisha ukatafuta namna ya kunogesha penzi lako humo ndani.

2) kuchokana kutokana na kuzoeana kuliko pitiliza- ni wazi kwamba kwenye mapenzi mazoea hayatakiwa hata kidogo. kila siku inabidi wenzi wajitahd kuimprovise mambo mapya ili kutokuzoeana hili litapunguza ile hali ya kuona ni kawaida tu awepo asiwepo.

3) mapenzi kwa watoto- hali ya kuzaliwa mtoto katika familia huleta furaha kwani ni baraka ya ajabu kati yenu. lakini sasa mapenzi haya yakielekezwa kwa watoto tu yakasahahulika kwa upande wa nyie mnaowaunganisha hao watoto mambo huenda kombo.

4) matamanio ya life style za wengine- hii ni kutokana na exposure ambayo mmoja wa wapenzi anaipata so kama mmtu ana marafiki ambao life style yao ni aya aina fulan na ukiangalia ya kwako ni tofauti basi automatically utaishia kutokuyapenda maisha yako simply kwasababu unaona hayafanani na yale ambayo unatamani mkeo awe anayafanya yanayosadifu uliyoayaona.

5) overexpectation especially before joining together. kuna watu wengi ambao enzi za uchumba watakuwa wana over expectation nyingi juu ya wenzi wao sasa wanapokuja kuish maisha halisi hali huwa tete manake anakuta alotarajia sio hivyo hukosa hamu nae kabisa.

6) pretendence hili husababishwa na maigizo mengi yasiyokuwa ya kweli wakati wa uchumba sasa unapokuja ndania kila mtu anaonekana jinsi alivyo ndipo kuchokana kunapokuja.

7) kulea- wengi wa akina mama hubadilika maumbo na harufu za mwili wanapokuwa wanalea watoto wadogo sasa kama mkeo amebadilika labda kawa mnene zaid ama ana harufu fulan ama nywele zake ndefu zimekatika katika ama ngozi imekuwa sio nyororo tena ama kifua kimetanuka sana nk

namna ya kufanya ili kuepukana na hali hii.

chunguza kwa makini sababua ya wewe kumchoka je ni kwasababu analea, ama upendo kahamishia kwa mtoto nk? ukishajua fanya haya yafuatayo.

1) yale ambayo ni yake binafsi like usafi, uvaaji nk yarekebisha kwa kumwelekeza kwa upendo. mgharamie nywele ziwe utakavyo na hata ngozi iwe upendavyo.

2) yale ambayo yanatokana na tabia labda aliigiza sasa badili mid set yako kwamba she is real now and anza kuishughulikia tabia moja baada ya nyingine hadi ziwe kama upendavyo.

3) kama sababu ni kukinai ama mazoea ama yakufanana na hayo, just try to improvise sio kila siku mlale kitandani siku nyingne tupa godoro chini mlale chini ili tu kuwepo na kaupya fulan humo ndani, pia mshirikishe mubuni njia tofauti ya kupeana mapenzi na mshirikishe kweny kuimprovise.

ikishindikana kabisa take a vacation mwambie labda aende kijijini kusalimia ama wewe chukua likizo safiri just fofr a weak ili umiss naamin akirudi mambo yatakuwa safi. kamwe usitoke nje ya ndoa yako.

nakuitia pia snowhoite aje aendelee hapa nilipoishia. ila usiogope tafuta suluhu ya tatizo lako kwa makini. kumbuka kusali daima.

Asante sana sana. I believe wengi sana watafind post yako very helpful I being the first one.Nimefall kwenye categories kama mbili au tatu ya ulizozitaja. Nita act promptly kabla haijafika pabaya.
Na hapo kwenye kusali pia,huwa ninasali but nasahau kuombea hili,hivyo umenifungua sana.
Be blessed.
 
pole,

hauna stress?

Badilisheni mazingira, tafuteni waga mpya, na usali kuombea ndoa yako

Stress pia inaweza ikawa sababu? Lately nimekua na mambo mengi sana,kazini mambo ni mengi na nimeanzisha biashara flani ambayo bado ni changa hivyo inahitaji close supervision, if so inaweza ikawa inachangia sana. lakini pia tatizo ni nikimuangalia simuoni kama nilivyokua namuona mwanzoni,nashindwa hata kuelezea. Asante sana kwa ushauri wako, nitajitahidi kupunguza mawazo kwa kubadili mazingira pia kusali zaidi, kama ulivyoshauri, kuondoa hali hii.
 
Asante sana sana. I believe wengi sana watafind post yako very helpful I being the first one.Nimefall kwenye categories kama mbili au tatu ya ulizozitaja. Nita act promptly kabla haijafika pabaya.
Na hapo kwenye kusali pia,huwa ninasali but nasahau kuombea hili,hivyo umenifungua sana.
Be blessed.

amen fanyia kazi ushauri pasi kukata tamaa. nimefurah kama nimeyagusa maisha mayo to such extent.
 
omba Mungu huyo mwanamke asijue ..akijua tu imekula kwako, lazima atakitembeza nje
 
Mimi ushauri wangu SIO ENDELEVU ila una ukweli ndani yake. Itakuwa mkeoa KABONGEKA sana baada ya kuzaa, kajiachia na misupusupu ile, na stress za mtoto. Nido limelala basi ukimuona KUSHNEY MARIDHAWA!!! Hii inatokea sana wadada wa kawaida. Mi ushauri wangu she should HIT THE GIM, DIET sana na umfanyie SHOPPING babu kubwa ya NGUO NA MIWIGI, VIATU, MIPOCHI. Hii itamrudishia the SEXY LOOK uliyoizoea. Na kama haendi kazini, mtafutie biashara ili AOGE ASUBUHI na kutoka, maji ya asubuhi mazuri kuongeza mvuto. Trust me ukifanya hivo mwenyewe utamsahau!!!!!
 
vipi kuhusu matarajio yako ya kimaisha?
unardihika ulipo kazini?
mkeo unahisi amebadilika umbile alilokuwa nalo mwanzo?
unahisi mkeo ana attention sana na mtoto kuliko wewe?
kifedha je unamudu kuprovide kwa familia yako?
unajiamini uwezo wako wa kijinsia uko poa?
kuna kitu negative umesikia kuhusu mkeo?
unahisi mkeo amekudominate kiuchumi,kielimu,kimawasiliano,?
hebu funguka zaidi kwa mwongozo huo hapo juu!

Kazini mambo yanabana sana and matarajio ya maisha kuna vitu vingi bado sijavifikia,umbo kabadilika though ni kidogo but mostly in a positive way,alikua mwembamba now kanawiri,attention ya mke wangu ipo sawa tena ninamuona kama anapenda sana kuwa karibu yangu,kifedha ninaimudu I am certain,kijinsia I absolutely have no doubt,sijasikia chochote -ve kuhusu yeye. Kiuchumi hajanizidi wala kielimu but sijaelewa "kimawasiliano" ina maanisha nini snowhite.
 
Mimi ushauri wangu SIO ENDELEVU ila una ukweli ndani yake. Itakuwa mkeoa KABONGEKA sana baada ya kuzaa, kajiachia na misupusupu ile, na stress za mtoto. Nido limelala basi ukimuona KUSHNEY MARIDHAWA!!! Hii inatokea sana wadada wa kawaida. Mi ushauri wangu she should HIT THE GIM, DIET sana na umfanyie SHOPPING babu kubwa ya NGUO NA MIWIGI, VIATU, MIPOCHI. Hii itamrudishia the SEXY LOOK uliyoizoea. Na kama haendi kazini, mtafutie biashara ili AOGE ASUBUHI na kutoka, maji ya asubuhi mazuri kuongeza mvuto. Trust me ukifanya hivo mwenyewe utamsahau!!!!!

Asante sana,but hajabongeka,amekua na mwili mzuri instead na bahati nzuri ana kazi pia.
 
hizi ndoa jamani..............................kaniki kukuuu manake kila ukishona hapa inafumukia hapa.
 
ila nakumbia siku ukimegewa basi ile hamu yako kwake itarudi. believe me kuna wanaume huwa wanajidai ooh! mie mwanamke hanisumbui wala hanikondesh na kama atatoka atoke tu, sasa siku wake wakipata japo kafununuu tu kwamba mkeo anatoka na fulani lol! utashangaa na ukweli hali hii huongeza mapenzi mara milion kuliko kujinyenyekesha kwa mwanaume.

natamani ajue kwamba huna hamu nae ili atafute liwazo mitaa ya kati halafu wewe ndo utakapo rudisha hamu mara million.
 
Ni muda mfupi tangu nimuoe mke wangu na tumebahatika kupata mtoto wa kiume mwaka jana. Tatizo ni kuwa,muda huu mke wangu kaongeza mapenzi kwangu ila mimi simpendi tena kama ilivyokua zamani na hata hamu naye imepungua. Sina nyumba ndogo na sijawahi kutoka nje ya ndoa hata mara moja wala sina mwanamke nje anayenichanganya. Hali hii imetokea ghafla na ninadhani bado hajatambua lakini ninawasiwasi atatambua punde kwa sababu hata kumuambia nakupenda imekua vigumu sana nowadays. Je hii ni kawaida katika ndoa na ni kipindi cha mpito? nifanyaje niweze kuondoa hali hii?
Ninaomba msaada wana jf.

Vipi uliingia labour kushuhudia mkeo akijifungua?kama ndio tafuta ushauri.maana wengine hua inawaadhiri kisaikologia.Pole,Mungu akusaidie hiyo hali ikutoke.
 
kama mfuko unaruhusu, badilisha mazingira kwa muda tu. safiri nae out of your normal 'boring' place. tumezoea kukaa sana eneo moja (home) kwa muda mrefu.

change sex positions everytime you f...ck her. Inaelekea wewe mazee ni wa missionary style tu. lazima uchoke. mkeo ndo mwanamke pekee wa kumwonyesha kalufundi ulichonacho. na yeye utashangaa atakavyo respond vizuri na kumuona mpya everyday.
usisubiri Vicheche wa mtaani wa exploit hiyo opportunity. na kama kweli hujaruka fence yako hadi leo, basi usijaribu, manake wewe unaonekana bado bikra kwa vicheche nje ya gate.
ukiishi na mkeo kama baba na mama, lazima ukinai mapema. Ishi nae kama mshikaji wako tu wa kitaa. utani mwingiii, X unapiga jikoni, sebuleni, bafuni, garden, darini etc.
usipofanya hivi, utashangaa kuna njemba inajitokeza na kufanya yale ambayo wewe ulikuwa unaona kama si heshima mbele yake. LOVE is all about FUN. make full use of it.
chezea missionary style wewe! UTAKUTA MWANA SI WAKO.
chimba dhahabu hadi uipate mwenyewe. usisubiri wana apolo wakusaidie.
 
Kazini kuko sawa?
Familia yako haisumbui?

Kama hayo yote yako sawa, katambike kidogo.

Kongosho!!!!! unainacha hoi sana majibu yako... ila kweli kama kazini na familia haina tatizo , kwanini asiende kwenye maombi kama kawaida yetu? Akatambike?
 
You jf buddies sometimes you are da great thinker mmemshaurui vizuri sana mda mungu awabariki jamani.kila nililokuwa nawaza nakuta mdau kalisema so blesssd.mtoa mada zingatia hayo .ogopa kumsaliti mtu asiyekusaliti hii dhambi haisameheki.au k sio mnato tena?
 
Aisee. Sali sana, na umuambie aongeze kipimo cha limbwata kidogo.
Pambana nayo hiyo hali kwa kuwa rafiki yake. Walau fanyeni utani ama muende gym kama sio kutembea pamoja jioni. Hakikisha mnapata muda wa kuwa peke yenu bila mtoto.
 
Kazini mambo yanabana sana and matarajio ya maisha kuna vitu vingi bado sijavifikia,umbo kabadilika though ni kidogo but mostly in a positive way,alikua mwembamba now kanawiri,attention ya mke wangu ipo sawa tena ninamuona kama anapenda sana kuwa karibu yangu,kifedha ninaimudu I am certain,kijinsia I absolutely have no doubt,sijasikia chochote -ve kuhusu yeye. Kiuchumi hajanizidi wala kielimu but sijaelewa "kimawasiliano" ina maanisha nini snowhite.
hapo kwenye bold inaweza kuwa ni taizo kama linakula sana kiakili.kuhusu kudominate kimawasiliano ni pale mke anapokuwa ana sauti sana kwnye maamuzi yenu mara nyingi hii huwa inabelittle wanaume kihisia,kama hali iko hivo kikweli huna shida sana since kwa kusema hapa tu tayari umeanza step ya kwanza kulimaliza hilo tatizo kakaangu!tuje kwenye mambo ya rum,vipi kuhusu mazingira,vipi kuhusu style mnazotumia,vi[i kuhusu mapishi ya mkeo,vp kuhusu unalitazama vipi lile tendo kwa ujuml?vipi kuhu wewe mwenyewe lifestyle yako,unafanya mazoezi?unakula mlo wa aina gani?vitu gani unapenda mkeo avifanye kwako huvipati na unahisi huwezi kumwambia?ila kubwa kabisa hapa mnasali na mkeo pamoja kama mke na mume?mnaombea ndoa yenu?
my take!
furaha na amani yetu kimaisha haipo kwenye token la msingi ni kutafuta amani ya ndani kabisa kwenye mioyo yetu na mengine huwa yanateremeka tu kama uko poa upstairs!lwork on it mtazamame mkeo ni mwanamake wa aina gani talk with her!ANGALIZO!utafute namna nzuri ya kuzungumza nae hili sio in a way ajisikie vibaya since umekiri mwenyewe yeye si tatizo!muonyeshe ulivyo tayari kusaidiwa muokoe ndoa yenu!kila na kheri na Mungu awabariki sana!
 
kama mfuko unaruhusu, badilisha mazingira kwa muda tu. safiri nae out of your normal 'boring' place. tumezoea kukaa sana eneo moja (home) kwa muda mrefu.

change sex positions everytime you f...ck her. Inaelekea wewe mazee ni wa missionary style tu. lazima uchoke. mkeo ndo mwanamke pekee wa kumwonyesha kalufundi ulichonacho. na yeye utashangaa atakavyo respond vizuri na kumuona mpya everyday.
usisubiri Vicheche wa mtaani wa exploit hiyo opportunity. na kama kweli hujaruka fence yako hadi leo, basi usijaribu, manake wewe unaonekana bado bikra kwa vicheche nje ya gate.
ukiishi na mkeo kama baba na mama, lazima ukinai mapema. Ishi nae kama mshikaji wako tu wa kitaa. utani mwingiii, X unapiga jikoni, sebuleni, bafuni, garden, darini etc.
usipofanya hivi, utashangaa kuna njemba inajitokeza na kufanya yale ambayo wewe ulikuwa unaona kama si heshima mbele yake. LOVE is all about FUN. make full use of it.
chezea missionary style wewe! UTAKUTA MWANA SI WAKO.
chimba dhahabu hadi uipate mwenyewe. usisubiri wana apolo wakusaidie.

umeona enh love is all about fun and having it!nimependa ulichoandika!
 
hilo ni tatizo lakuanza kufanya mapenzi kabla ya kuingia kwenye ndoa, unajikuta kama unao mke wako maana mnakuta ndani ya ndo hakuna jipya...
 
huwezi kumuoa mke wako, kilichomkuta ni kwasababu hakuna jipya ndani ya ndoa yao, kila kitu walifanyaga huko maguesgt house na ma hotelini unadhani hapo hautomchoka? Yeye mwenyewe anakuzuga ila kaona huna jipya maana kila kitu mlisha fanyaga kabla ya ndoa
kazini kuko sawa?
Familia yako haisumbui?

Kama hayo yote yako sawa, katambike kidogo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom