Nimepick hiki kutoka kwenye hotuba ya Raisi

BLUE BALAA

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
1,222
764
Kwa wale wajasiria mali nime pick hii toka speech ya Mh Raisi

Kwa ajili ya kuziba pengo la miezi ya Mei na Juni kibali kimetolewa cha kuagiza tani 50,000 za sukari kutoka nje ya nchi. Tunatarajia kupata tani 12,500 kutoka nchi za Afrika Mashariki na tani 37,500 zitatoka nje ya Afrika ya Mashariki. Bahati mbaya sana kuna upungufu mkubwa sana wa sukari duniani, hivyo bei imepanda kuliko wakati wowote katika miaka ya hivi karibuni. Tani moja ya sukari inauzwa kwa dola za Marekani 900 ikilinganshwa na dola za Marekani 500 mwaka 2009. Hivyo, sukari itakayoingizwa wakati huo itakuwa na bei kubwa. Kwa nia ya kuzifanya bei ziwe chini na kuwapa watumiaji nafuu, sukari hiyo haitatozwa ushuru wa forodha. Tutafanya hivyo pia kwa vyakula vyote muhimu tutakavyolazimika kuagiza kutoka nje kwa sababu ya uhaba wa mvua uliokumba maeneo mengi hapa nchini.
 
huyu mkwere kaishiwa sera yani eti watu walificha sukari ili kulangua bei na umegundua na ukufanya lolote kuwawajibisha
 
Wale wale walioficha SUKARI, kwa mujibu wa RAISI, ndiyo wale wale watakaogiza SUKARI na kuiuza kwa bei kubwa!

Kila kitu hapa Bongo ni DEAL! I was told hata Mabomu ya Gongo La Mboto ni DEAL kwa wauza vyuma chakavu!
 
Back
Top Bottom