Nimependwa na jimama nifanyeje?na kuna tetesi kuwa mme wake alikufa kwa ugonjwa wa ukimwi

Unaonekana na wewe pia unamtaka huyo jimama! :eyebrows::eyebrows::eyebrows:
Natumaini una akili timamu za kufanya maamuzi sahihi juu ya hili.
Usisahau kutupa feedback ya maamuzi yako.
 
Ushauri wangu kimbia tena usiangalie nyuma.ila na we kweli wa ajabu jitu linaskendo mbaya alafu unaomba ushauri..ENDEKEZA NJAA TUKUZIKE.ila kama unalipenda kalipimishe.
 
Unaonekana hujawahi kufa wewe, halafu sijui masabuli babaako! hata adabu huna wewe, hilo limama likufunulie mautupu yake utavumilia weye? Kubali ufe labda baada ya hapo ndo utajua uzuri au ubaya wa jambo hilo.

Hajui ladhii ya haya majimama huyu?
 
Msomi wa chuo kikuu mlimani mwaka wa pili unalia lia hapa......
1. Eti umeambiwa unapendwa......(kama mtoto wake, kwa kuwa unafaulu sana au just platonic love? Y umefikiria love ya chupi tu?? )
2. Limekuuliza una mchumba.....(ukakataa eti unamuogopa...... kwa mamako mzazi utamtambulishaje huyo mchumba kama mtu baki tu unamuogopa ????
3. Umesikia mume wake kafa kwa ukimwi......So what nawe huna uhusiano naye wa kimapenzi??? Stigmatization tuuuu!!!!!!
4. Jimama linakupigia simu kukuambia usiku mwema na kukutumia buku mbili.....huwa unajibu nini? hizo vocha huwa unatumia au unarudisha??

Anzia hapo as elimu yako inatosha kuelewa katikati ya mistari hiyo.
Mchango wa mawazo utapata hapa Jf kama hivi .
Zipu yako kufunguka au kubaki imefungwa inategemea na vichwa vyako vinafikiria nini na vinafikiriaje wakati huo brooo
 
miaka 3 mumewe kafariki unadhani we wa kwanza kutongozwa au we ni mzuri zaidi ya wengine ? Fanya uchunguzi wako anao wangapi hadi sasa mbali na wanafunzi
 
Hujui cha kufanya hapo kweeli ? Usomi wako unakusaidia nini sasa.inawezekana hata m*vi yakikubana unauliza watu ufanye nini. Kimbia fasta kabla hujaanza kujilaumu.
 
Unajua najiuliza wasomi wetu wa siku hizi wana akili gani. Radio, TV, na magazeti yamejaa matangazo ya UKIMWI na FATAKI! This is the same person, who is a University student, whom we expect to lead the nation! ndio mtu huyo huyo anauliza maswali ya ajabu namna hii.

This is JF, a home of great thinkers!
 
Kwa swali hilo inaonyesha ni jinsi gani 'umeelimika'. Kama umeshindwa kusema no ni bora ungebaki chekechea kujifunza neno hili 'NO'. Inawezekana unaliona ona lakini hujui ling nguvu kias gan
 
Ni kwamba umeshindwa kufanya uamuzi ama?Kama una gelofrend jiandae kupigwa chini.
Haya sasa Uchaguzi ni wako
Chagua Uzima au Kifo
Kuchagua Uzima maana yake kumpiga kibuti huyo jimama
Kuchagua Kifo maana yake ni kusema ndiyo kwa jimama.
NB:Nauza Majeneza yaliyotumika.
 
Kaka, nahisi wewe ulianza kumpenda au inaoekana unahitaji msaada toka kwake. mimi sioni ubaya kwako wewe kumwambia kua una mpenzi unaona aibu ya nini? mbona yeye hajaona aibu ya kukutongoza? halafu wewe unajifanya unamheshimu, Im sure km ungekua unamheshimu ungemwambia kuwa una mpenzi wako. achana na huyo mama na usidhani kuwa huyo ni kama hivi videmu vidoo vya mtaani huyo akikupata atafanya kila awezalo usitoke kwenye himaya yake. namalizia kwa kusema
KAZI NI KWAKO
 
Wewe kijana..zingatia kitabu, kama alikuambia anakupenda ndio kwamba alikuambia anataka mahusiano na wewe? alichokuambia umjibu sawa hata wewe unampenda sana na mpotezee elekeza nguvu na juhudi kwenye masomo.
 
Msomi wa chuo kikuu mlimani mwaka wa pili unalia lia hapa......

Anzia hapo as elimu yako inatosha kuelewa katikati ya mistari hiyo.
Mchango wa mawazo utapata hapa Jf kama hivi .
Zipu yako kufunguka au kubaki imefungwa inategemea na vichwa vyako vinafikiria nini na vinafikiriaje wakati huo brooo

1. Kichwa kimoja najua kiko busy na masomo na asikihusishe na mambo haya maana atafeli.
2. Wasi wasi wangu ni hicho kichwa cha pili, kwa kawaida hakina akili lakini kina ushawishi ambao mara nyingi ni potofu.

Nimejaribu kusoma comments zake huyu jamaa, naona kama yote aliyoelezwa humu hayajamuelea.
Wewe Mwendapole1 nachelea kuwa ushagonga hilo jimama likusaidie kupona supp na kupata hivyo vibuku mbilli mbili, subiri kuona "value for money" ya huo ujinga wako.

Unajifanya huelewi kumbe unatafuta watu wa ku-support upuuzi wako eeeh! Ushauri si lazima ukidhi matarajio yako. Take care!
 
Ni kwamba umeshindwa kufanya uamuzi ama?Kama una gelofrend jiandae kupigwa chini.
Haya sasa Uchaguzi ni wako
Chagua Uzima au Kifo
Kuchagua Uzima maana yake kumpiga kibuti huyo jimama
Kuchagua Kifo maana yake ni kusema ndiyo kwa jimama.
NB:Nauza Majeneza yaliyotumika.

Ungesema na bei kabisa pamoja na material yake maana huyu nadhani hatahitaji yale ya wanene.
 
Back
Top Bottom