Nimependa picha hii je wewe?

mpayukaji

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
940
349
NYJC501-1010_2010_122102_high.jpg
Picha inayoonyesha madikteta wanne waliodondoka mmoja baada ya mwingine huku mmoja akiuawa. Kweli dunia inakimbia.
 
Shida ni tafsiri ya dikteta!
Hivi,George Bush wa marekani na Gaddafi wana tofauti zipi?
Infact bush anamzid udikteta,lakin ni magaid wasio na zana na uwezo wa kifedha ndio wanao andamwa wakati magaidi matajiri au wale vibaraka wa magaid matajiri wanatamba na kusifiwa na vyombo vya habari vya magaid matajiri!
 
nimedharau sana uelewa wako juu ya hao uliowaita madikteta. Ni bora nchi iongozwe kidikteta na mambo yaende kuliko nchi iongozwe kudemokrasia na mambo yake yawe kama bongo. Leo hii ealibya wanajutia maamuzi yao. Hawatopata tena fursa ile waliyoipata kwa gadafi.
 
Mak uko sawa,hakuna umasikini mbaya kama wa mawazo! hasa mazuri!
 
Unahitaji ukombozi wa fikra uweze kuelewa udikteta aliyofanya gaddafi na huu unaofanywa na mataifa ya magharibi,pole sana
 
Kama Gadafi ni dikteta Je Kikwete na serikali yake utamwitaje? Ya nchi yenu mnayashindwa kazi kuleta unoko
 
Well spoken the great thinker!
nimedharau sana uelewa wako juu ya hao uliowaita madikteta. Ni bora nchi iongozwe kidikteta na mambo yaende kuliko nchi iongozwe kudemokrasia na mambo yake yawe kama bongo. Leo hii ealibya wanajutia maamuzi yao. Hawatopata tena fursa ile waliyoipata kwa gadafi.
 
Shida ni tafsiri ya dikteta!
Hivi,George Bush wa marekani na Gaddafi wana tofauti zipi?
Infact bush anamzid udikteta,lakin ni magaid wasio na zana na uwezo wa kifedha ndio wanao andamwa wakati magaidi matajiri au wale vibaraka wa magaid matajiri wanatamba na kusifiwa na vyombo vya habari vya magaid matajiri!
Mkuu Tofauti kubwa ni kwamba udikteta wa Bush ulikuwa ni wa muda wenye kikomo . Hakuwa na ruhusa ya kuendesha udikteta wake maisha yake yote na pia kumrithisha mwanaye.
 
nimedharau sana uelewa wako juu ya hao uliowaita madikteta. Ni bora nchi iongozwe kidikteta na mambo yaende kuliko nchi iongozwe kudemokrasia na mambo yake yawe kama bongo. Leo hii ealibya wanajutia maamuzi yao. Hawatopata tena fursa ile waliyoipata kwa gadafi.

gadafi alikua na nafasi ya kuwaachia na walibya wenzake kuongoza nchi yao, failier to do that ameifelisha nchi yake na watu wake pia. Kiongozi mwenye mafanikio huanza na kumaliza vema utawala wake. Gadafi is a failier ruller.
 
Hatutaki marais wapya kiloa asubuhi tunataka maisha waliyokuwa wakiishi watu wa libya kipindi cha utawala wa ghadaf,
 
Bora kutawaliwa milele na mtu kama Gadaf kuliko utawala wa miaka kumi ya mtu kilaza kama JK. Yetu yanatushinda kazi kushupalia ya wenzetu, unayaona maisha ya walibya leo? Heri dogo janja kuliko KUBWA JINGA.
 
Mkuu,kumbuka shetan ni shetan tu,awe mwarabu au mzngu.
Well,bush aliua maelfu yake na kupumzika.OBAMA anafanya nini sasa?Kwan ugaid wa kumrithsha mtoto na wa kumrthsha asiye mtoto kuna tofaut ip ya kimantiki?
Mkuu Tofauti kubwa ni kwamba udikteta wa Bush ulikuwa ni wa muda wenye kikomo . Hakuwa na ruhusa ya kuendesha udikteta wake maisha yake yote na pia kumrithisha mwanaye.
 
Mkuu Tofauti kubwa ni kwamba udikteta wa Bush ulikuwa ni wa muda wenye kikomo . Hakuwa na ruhusa ya kuendesha udikteta wake maisha yake yote na pia kumrithisha mwanaye.
mkuu unamanisha bush mkubwa au mdogo?mkubwa alimrithisha bush mdogo,yani mwanae
 
Back
Top Bottom