Nimepata sababu ya kumshistaki Mwema na Kikwete

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,903
1,053
Wakuu nilipokuwa nikisoma katiba nimeshangaa kwamba ninayo ruhusa ya kumshitaki Mwema mahakamani kwa kuvunja katiba makusudi, kwa kuzuia maandamano na kuwapiga wananchi.
kifungu (1) na cha (2) cha ibara ya 26 ya katiba ya mwaka 1977 kinaniruhusu.

"26.-(1) Every person has the duty to observe and to abide by this
Constitution and the laws of the United Republic.
Act No.15
of 1984
Art.6
(2) Every person has the right, in accordance with the procedure
provided by law, to take legal action to ensure the protection of this Constitution
and the laws of the land.
"
Mwema anajua wazi kwamba kifungu cha katiba wanayoapa kuilinda kinasema kwenye katika ibara ya 20 hivi:
"20.-(1) Every person has a freedom, to freely and peaceably assemble,
associate and cooperate with other persons, and for that purpose, express views
publicly and to form and join with associations or organizations formed for
purposes of preserving or furthering his beliefs or interests or any other interests.
"

Kisha kutokana na ibara ya 26 kifungu cha 1 na 2 nataka kumshitaki Kikwete, Pinda na CCM kwa kutaka kuingiza suala la Mahakama ya Kadhi katika serikali kinyume na katiba inavyotaka. Nimeona jinsi katiba ilivyokuwa wazi katika hili. Nategemea kutumia vifungu hivi vya katiba hii hii kuwashitaki kwa Ibara ya 20:

"(2) Notwithstanding the provisions of subarticles (1) and (4), it shall not
be lawful for any political party to be registered which according to its
constitution or policy -
(a) aims at promoting or furthering the interests of any faith or religious group;


Sasa basi kwa makusudi kabisa wote ninao kusudia kuwashitaki wanaivunja katiba hiyo waliyoapa kuitunza na kuifuata.
Naomba mwanasheria aliyetayari kunisaidia ani PM
.
 
Tafuta sahihi za watanzania wanaotaka kuungana na wewe katika kesi hiyo na mimi nitakupa saini yangu kwa haraka sana. Nenda kwenye press conference kisha eleza nia yako na contact zako kisha nitakupa signature yangu kuwa nitachangia kesi hiyo na nitakuwa upande wa walalamikaji.
 
NaOMBA NIWAPE KWA KISWAZI SABABU ZA KUWASHTAKI MWEMA ,JK,MAKAMBA NA RPC WA ARUSHA
KUTOKA IBARA YA 20 NA 26 YA KATIBA YETU MBOVU YA KIKWETE NA MAFISADI WAKE
Uhuru wa mtu
kushirikiana na
wengine Sheria
ya 1984 Na.14
ib.6
20.-(1) Kila mtu anastahili kuwa huru, bila ya kuathiri sheria
za nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani,
kuchanganyika na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo
hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au
mashirika yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au
kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.
(2) Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya (1) haitakuwa
halali kwa chombo chochote cha siasa kuandikishwa ambacho
kutokana na Katiba au sera yake-
(a) kinakusudia kukuza au kupigania maslahi ya-
(i) imani au kundi lolote la dini;


(ii) kundi lolote la kikabila pahala watu
watokeapo, rangi au jinsia;
(iii) eneo fulani tu katika sehemu yoyote ya
Jamhuri ya Muungano;
(b) kinapigania kuvunjwa kwa Jamhuri ya Muungano:
(c) kinakubali au kupigania matumizi ya nguvu au
mapambano kama njia za kufikia malengo yake ya
kisiasa;
(d) kinapigania au kinakusudia kuendesha shughuli zake
za kisiasa katika sehemu moja tu ya Jamhuri ya
Muungano;
(e) hakiruhusu uongozi wake kuchaguliwa kwa vipindi na
kwa njia za kidemokrasia.
(3) Bunge laweza kutunga sheria inayoweka masharti
yatakayohakikisha kuwa vyama vya siasa vinazingatia mipaka na
vigezo vilivyowekwa na masharti ya ibara ndogo ya (2) kuhusu
uhuru na haki ya watu kushirikiana na kujumuika.
(4) Bila ya kuathiri sheria za nchi zinazohusika ni marufuku
kwa mtu yeyote kulazimishwa kujiunga na chama chochote au
shirika lolote, au kwa chama chochote au cha siasa kukataliwa
kusajiliwa kwa sababu tu ya itikadi au falsafa



Wajibu wa kutii
sheria za nchi
Sheria ya 1984
Na.15 ib.6
26.-(1) Kila mtu ana wajibu wa kufuata na kutii Katiba hii na
sheria za Jamhuri ya Muungano.
(2) Kila mtu ana haki, kwa kufuata utaratibu uliowekwa na
sheria, kuchukua hatua za kisheria kuhakikisha hifadhi ya Katiba
na sheria za nchi.
 
Back
Top Bottom