Nimepata chuo na mkopo lakini nimenyimwa ruhusa kazini nifanyaje ?

Sep 22, 2014
58
3
Hivi mtumishi anaponyimwa ruhusa na mwajiri wake kuwa asiruhusiwe kwenda kusoma eti hajakizi vigezo hasa kuwa kazini miaka miwili na huku chuo kapata na loan tena asilimia 90 ni halali ?

Na pia mtumishi huyo hahitaji kugharamiwa chochote na mwajiri wake lakini bado ananyimwa ruhusa.

Je afanyeje ili aruhusiwe kwani anataka kusoma.

Ushauri wenu jamani ni mhimu sana
 
Mfumo mzima wa uongozi wa mwajiri wake, ni tofauti kabisa na matakwa ya mfanya kazi kufanya atakavyo. mfumo au sheria ya kazi inakutaka ufikishe miaka 2 then ndo uombe kwenda kusoma, wewe unataka uende kusoma wakati muda bado haujafika eti kisha umepata shule na mkopo juu yake. hilo suala mwajiri hawezi kuliona kama ni tishio ili atoe ruhusa. kinacho takiwa ni kufuata sheria na makubariano ya kazi uliyo isaini.

Kwa ushauri wangu, ni vizuri uwaombe friendly kabisa waweze kukujadili kuona kama wanaweza kuvuja sheria hiyo au la! kama itashindikana na wewe ndo umeamua kusoma angalia kazini kama wanaruhusu kutoa ruhusa ya kwenda kusoma bila malipo. kama inakubalika wakupe barua ukaende kusoma lakini bila malipo ya mshahara.

Ikishindikana na wewe ndo unataka kwenda kusoma, njia pekee ni kuacha kazi. hauna pa kwenda kulalamika kwasbb sheria ya kutimiza vigezo bado inakubana.
 
Hivi mtumishi anaponyimwa ruhusa na mwajiri wake kuwa asiruhusiwe kwenda kusoma eti hajakiz vigezo hasa kuwa kazin miaka miwili na huku chuo kapata na loan tena asilimia 90 ni halali. Na pia mtumishi huyo hahitaji kugharamiwa chochote na mwajiri wake lakini bado ananyimwa ruhusa. Je afanyeje ili aruhusiwe kwani anataka kusoma. Ushauri wenu jamani ni mhimu sana

ni halali kabisa,labda iwe tu kwa huruma ya mwajiri wako.unataka sheria za kazi ziwe kama unavyotaka wewe?sheria inasema miaka 2,sasa wewe kusoma kwako na huo mkopo wako unamuhusu nini mwajiri?
 
Kazi unaipenda na shule unaitaka.....resign nenda kasome
 
Pole mjomba,mimi nimetimiza miaka 2 na zaidi lakini nimenyimwa ruhusu coz sikuwa kwenye mpango wa halmashauri tena nitaje ni makete,viongozi wanaukilitimba ile mbaya hawataki tupige shule tutawapita kielimu.kwenye mpango waliingizwa 7 wa idara yetu pasipo makubariano mwisho wa siku wameenda wanne,wengine hawakuomba kuingizwa,kwa upande wangu niliomba lakini hola.du ajiriwa makete uje ona viigizo vya wakuu wa idara na mkurugenz sumbua na ndio maana watumishi wakipata nafasi ya kuja huku hawaji kabisa wanaona bora waache kazi.duuu.mimi nimeinua mikono nafasi nimepata lakini nimegaili so nitajua mbele kwa mbele,ningepata mkopo ningeomba ruhusa isiyo na malipo.ning'esepa kaa lowasa.
 
je,ni vigezo gan unatakiwa kuwa navyo ili upate ruhusa isiyo na malipo????
 
Soma open mtu ang fanya transfer mapema..mm yamenikuta kama haya nikaamua kuomba open..coz siez acha hii nafasi
 
Hiindo nchi yetu mtuwangu nahizo ndo sheria zake utafanyaje sasa. kama unaweza kuacha kazi uende kusoma bila kuruhusiwa labda ila kumbku mshahara ndo bas tena
 
Hivi mtumishi anaponyimwa ruhusa na mwajiri wake kuwa asiruhusiwe kwenda kusoma eti hajakizi vigezo hasa kuwa kazini miaka miwili na huku chuo kapata na loan tena asilimia 90 ni halali ?

Na pia mtumishi huyo hahitaji kugharamiwa chochote na mwajiri wake lakini bado ananyimwa ruhusa.

Je afanyeje ili aruhusiwe kwani anataka kusoma.

Ushauri wenu jamani ni mhimu sana

Wewe ni mwalimu japo hujasema kitengo chako cha kazi, maana walimu kunyimwa ruhusa na kufanya maamuzi magumu ni waoga, Sasa mi nakushauri acha hiyo chaki nenda kaanze masomo chuoni mapema na haraka sana, maana hiyo 90% hutoipata tena ukiahirisha masomo bila kujisajili kwenye chuo husika. Kazi zipo utafanya ukigraduate tafadhali usiwe mtumwa, jikomboe kwa fikra pevu. Nchi hii inaharibika vibaya kwenye mfumo wa elimu ya juu na upatikanaji wa mikopo kujisomesha.
 
Back
Top Bottom