Nimeoneshwa demu wa JF

Katika purukushani zangu za hapa na pale kuna memba mmoja wa JF wa zamani (jina kapuni) akanionesha demu wa JF. Kuingia JF na kuona avatar yake wache niumie mbavu kwa kucheka, ni vitu viwili tofauti, duhh japo kungekuwa kuna kamfanano kadogo nimgemsifu.

Nawaomba mijimama na mijibaba ya JF msizuge na kuwatia watu tamaa kwa avatar ambazo hamfanani nazo hata chembe.

Alaa ...

Mi nakushauri uende Facebook... Utakutana na saizi,na machaguo yako... Ukija huku huo kwetu ni ******..

Hatushindanii uzuri wa sura ndani ya JF... JF tunashindania nani mwenye idea bora ya kuijenga nchi yetu..,na kumkomboa kifikra mwanamke na wote wanaonyanyasika pasipo kujua haki zao...

Jukwaa la chit chat,ni jukwaa la mapumziko kwetu,baad ya kuichosha na kuifikirisha akili..

Watu ndani ya JF,wanajitambulisha kwa avatar na si picha,ingawa haikatazwi.. Ila lengo si kufahamiana humu na kuchat kama Facebook uliyozoea wewe..
Humu tunashirikisha zaidi akili zetu,ideas,...

Kama una akili,ungeomba usaidiwe kufutiwa thread thread yako toka jana!
 
Katika purukushani zangu za hapa na pale kuna memba mmoja wa JF wa zamani (jina kapuni) akanionesha demu wa JF. Kuingia JF na kuona avatar yake wache niumie mbavu kwa kucheka, ni vitu viwili tofauti, duhh japo kungekuwa kuna kamfanano kadogo nimgemsifu.

Nawaomba mijimama na mijibaba ya JF msizuge na kuwatia watu tamaa kwa avatar ambazo hamfanani nazo hata chembe.

tutaftane FB!!!hapa wapo kimawazo zaidi kuliko muonekano!kama wewe demu au dadako anataka mwanaume wa muonekano niPM.......
 
Lazima kuna mambo yalikukuta siyo bure. either mliwasiliana baada ya kuwaka tamaa tu ulipoiona avatar. matokeo yake baada ya kupanga miadi mlipokutana hukutarajia kukutana na sura halisi. acha kupotezea bana ulipelekwa pwani kusema ukweli
 
tutaftane FB!!!hapa wapo kimawazo zaidi kuliko muonekano!kama wewe demu au dadako anataka mwanaume wa muonekano niPM.......

FB ndio nini? Full Board? Hiyo avatar ni wewe? kama ndio, yanini dadangu, mimi nimesha kumaindi.
 
sasa mie hapo, ukioneshwa utamchagua nani kati ya hawa?

Mie nilivyo na ukame hata ubao naondoka nao mradi uwe na vigezo tu. Kigezo cha kwanza lazima ujuwe kula na uma na kisu, maana deti langu la kwanza dina la nguvu.
 
Lazima kuna mambo yalikukuta siyo bure. either mliwasiliana baada ya kuwaka tamaa tu ulipoiona avatar. matokeo yake baada ya kupanga miadi mlipokutana hukutarajia kukutana na sura halisi. acha kupotezea bana ulipelekwa pwani kusema ukweli

Ingekuwa hivyo si raha hizo, ukame nliokuwa nao hata kama ana sura ya rejao mie poa tu.
 
Back
Top Bottom