Nimemwaga mboga...lakini nafsi inanisuta.

Wewe ni lichawi kabisa,kwa nini umemfanyia hivyo huyo dada?kukusaidia imekuwa kosa?sasa je unakijua kilichoendelea huko nyumbani kwao?wewe hufai hata kidogo SHAME ON YOU.
 
Wewe ni lichawi kabisa,kwa nini umemfanyia hivyo huyo dada?kukusaidia imekuwa kosa?sasa je unakijua kilichoendelea huko nyumbani kwao?wewe hufai hata kidogo SHAME ON YOU.

Wewe malaika, mimi mwanadamu tupo dunia tofauti kabisa.
 
wala hujamwaga mboga,yule jamaa ndo kamwaga mboga wewe ukamalizia na ugali tena wa muhogo
 
Huyu mwanaume amepata kile alichostahili kwani alikuwa hana sababu ya kukujia wewe na kukuuliza ju ya wewe kuzungumza na mkewe; yeye alikuwa na jukumu la kumkabili mkewe na kumueleza kuwa hakupendezewa na huo ukaribu aliodhani mkewe alikuwa nao kwako. Hata hivyo kitu ulichowafanyia hawa jamaa sio cha kiungwana; tafuta njia ya kuwasiliana nao na uwe mkweli kwanini uliwafanyia hivyo pamoja na kukili kuwa hukuzini na mkewe.
 
sasa anger ya nini na wewe ndie unaewasiliana na mke wa mwenzako? umefanya vibaya sana na hiyo itamcost huyo dada sana
 
Dah, kaka umeharibu sana. Ok any way ulikuwa unajihami lakini hili limekaa vibaya. Dah, ngojea nifikiri kidngo mkuu!
 
Wewe kaka muuaji kabisa na mbinafsi,ukamuondoa mkeo.Wapigie simu hiyo familia na uwaeleweshe
 
Jana nilifanya kitu kinacho ninyima raha sana, stori yenyewe ipo hivi.

Kuna msichana tuliwahi kuwa na uhusiano zamani kabla sijaoa na yeye kuolewa, kwa sasa anafanya kazi RITA. Kutokana na uhusiano mzuri tuliokuwa nao na pia tuliachana kwa roho safi kabisa kwa kuwa wote tulijua hatukua chaguo sahihi la kuishi hadi kifo kitakapo tutenganisha mimi na yeye bado tunawasiliana inapobidi. Mwezi uliopita nilikuwa nataka cheti cha kuzaliwa cha binti yangu kwa haraka nilipoenda pale RITA wakanizungusha wee hadi nikaamua kumtumia huyu dada ambaye ni X wangu.

Sasa nadhani wiki hizo mawasiliano yaliongezeka kidogo hasa kuhusu cheti cha binti yangu,mume wa huyu dada akaanza visa ikiwa ni pamoja na kumpigia simu mke wangu akimuambia anionye kuhusu mke wake. Mke wangu nili muelewesha lakini pia na yule dada nikamuambia aongee na mume wake. Yule mume wake akaona atumie nafasi hii kuniabisha, basi jana tukapanga tukae mimi mke wangu na yeye na mke wake tuweze ku clear hii issue. Tulipopanga kukutana kwa mstuko jamaa alikuja na mke wake lakini pia alikuja na jamaa zake ambao wengine mimi ninafanya nao kazi akilazimisha tuongee mbele yao. Kuona hivyo nikajua lengo lake lilikuwa kuniaibisha ndipo nikamstua wife aondoke.

Wife alipoondoka nikawaambia nipo tayari kwa mazungumzo ndipo jamaa kwa makeke akaniuliza kwa nini nawasiliana sana na mkewe, nilimuambia kuwa nilikuwa nimegundua nimeambukizwa ugonjwa wa zinaa na kwa kuwa pia nilikuwa nimetembea na mkewe basi tulikuwa tumeanza matibabu pamoja Marie stopes. Jamaa aliishiwa nguvu na kuondoka kwa hasira kubwa, mke wake naye aliishia kunimwagia maji na kuondoka. Sijui nini kimeendelea kwenye familia yao lakini sasa hivi najisikia vibaya mno. Hebu nisaidieni ni jinsi gani nitaweza kurudisha amani kwenye hii familia maana si kweli kama nimetembea na huyu msicha ila nilitaka ku get back kwa kutaka kunidhalilisha.

Huko kwenye red unafikiri alikuwa anataka kukuaibisha na kukudhalilisha kwa kitu gani? Kama mawasiliano na mke wake yalikuwa tuu kwa ajili ya cheti cha mtoto wako, angekuaibisha au kukudhalilisha kwa kitu gani? Kuna kitu kitu kingine cha aibu au cha kudhalilisha ambacho umeshawahi kufanya lakini bado umemficha kumwambia mke wako?

Halafu hapo kwenye blue unajua the root cause ya hilo tatizo ni nini? Then, linganisha na unayoandika kwenye jukwaa la siasa. Unaona jinsi huduma mbaya kwenye vyombo vyetu vya umma inavyoharibu mahusiano, mapenzi na urafiki? Kama ungehudumiwa ipasavyo unafikiri haya yote yasingetokea?
 
Tuko pamoja Igwe...ila nduka asilani usirudie tena, una bahati..kwani m'ume anapohanith.wa mbele ya mkewe anaweza fanya chochote..usionane naye anaweza kuwa kapata walimu wehu utaumia.
mhhhhhhhh!..yaani hapo ndipo ninapokiri keli Mungu katuumba tofauti_maake mimi nilivyo na kislani hata ex_wa girlfriend wangu sitaki kukaa naye karibu(thanx God hata simfahamu na wala sitaki kujua habari zake..hope hata wenzangu wenye hulka kama zangu hawataki kujua).,,sembuse mwanamke niliyemuoa alete ex wake eti tuongee,.....yaaani sijui
<br />
<br />
 
Wewe malaika, mimi mwanadamu tupo dunia tofauti kabisa.
<br />
<br />
Kitendo ulichokifanya ni cha kishetani kabisa kabisa,nenda kawaombe msamaha nakumueleza jamaa ukweli,ili unusulu ndoa yao othorways huyo dada atakulaani na laana yake lazima ikupate.
 
hivi ilikuaje hadi mkajuana....i mean nduka na mme wa x wake.
 
Back
Top Bottom