Nimemuacha lakini naumia mimi

Kuwa wewe bila yeye. Huyo hakukupenda hata chembe, na amekuwa akitafuta chance ili umuache ulikomaa.

Ushauri, ishi wewe kama wewe, siyo wewe kama yeye.
 
ndugu zangu naombeni msaada wa kimawazo

nilikuwa na girlfriend ambaye nilimpenda sana, lakini kwa bahati mbaya nilichukuwa uamuzi wa kumuacha kutokana na kuona ananitesa sana katika mahusiano. sijawai mkuta na mvulana lakini kwakweli hakunieshimu kabisa kama mvulana, yaan muda mwingi wa maisha yangu katika kipindi chote cha mahusiano nae nilikuwa naumia kutokana na tabia yake, nimejaribu mueleza mara kadhaa bila mafanikio, pia hata kuwatumia ndugu na rafiki zake wa karibu bila mafanikio. kwa kweli nilikuwa naumia sana kwani mwenzangu alikuwa haoneshi kunijari wala kunionea huruma kama mimi nilivyokuwa kwake

tisa, kumi ni pale aliponidanganya anasafiri anaenda kufanya kazi mkoani ambapo aliniambia, huko arusha anakaa kwa mvulana ambaye amemtafutia kazi, akaniambia tena kuwa huyo mvulana aliwai mtongoza hapo nyuma. kwa kweli niliumia sana for three weeks, nilishindwa kabisa kufanya kazi 'imagine boyfriend/girlfriend wako unaempenda sana' anakuambia anakaa na mtu aliyewai mtongoza huko nyuma wawili tuu kwa muda wa zaidi ya mwezi. nilishindwa fanya kazi kabisa ofisin. mwisho wa siku nilipombana aliniambia alikuwa ananidanganya. kwa kweli niliumia sana tena sana. na nilichukua uamuzi wa kuachana nae

TATIZO/MSAADA
tatizo langu sasa ni kuwa toka nimemuacha bado naumia sana Moyoni, naona kama sijamtendea haki, yaani nashindwa nifanyenini jamani!
nilikuwa na dream nyingi sana juu yake lakini naona nateseka muda wote wa mahusiano yetu. JE NIMEFANYA KOSA KUMUACHA??

Bwana mdogo Gonga Mbili;
Naona kama unatafuta justifications/excuses za kurudiana naye. Nimeshawahi kuona wasichana wa tabia ya namna hiyo uliyoitaja, japo si katika mahusiano kati yao na mimi. Wamekuwa wakihusiana na watu wengine halafu bahati mbaya au nzuri mahusiano yao yanatokea kuwa exposed kwangu either kama rafiki au ndugu wa karibu. Sikushauri umrudie au usimrudie ila jua kuwa ukimrudia uwe tayari kwa mojawapo tu ya mambo mawili yafuatayo:

1. Uhusiano ulioimarika sana na kubadilika kwa mpenzi wako kiasi kwamba utampenda kuzidi hata ilivyokuwa awali;

2. Uhusiano wa ajabu utakuja kutokea aidha immediately au baada ya mda kidogo. Anaweza kukutegea hadi akawa na uhakika kuwa umeamini kabadilika halafu umerudisha tena moyo wako kwake kuliko hata mwanzo, halafu ndiyo anakuja kukulipua vizuri, analeta za masika ukilinganisha na za sasa.

Wasichana dizaini hii huwa ni malimbukeni halafu wana akili kama imefyatuka kidogo, na mara nyingi wanakuwa ni waropokaji.

Anyway, just in case utashindwa, unaweza ukanitaarifu nirudiane naye mimi!
 
Wenzetu wazungu wanamsemo wanasema 'Pain is love'. Najua hali uliyonayo na unavyojiskia, kwasababu na mimi yalishanikutaga hayo zamani, ila usije ukafanya kosa ukamrudia huyo mwanamke, achana naye. Usiwe muoga kuanza upya, na anza upya sasa, yaliyopita si ndwele, utampata ambaye atakupenda na kukuthamini na atakayekuwa my wife wako.
 
Pole sana ndugu hayo ni mapito 2 binafsi nilipitia kipindi kama cha kwako niliacha kama wewe ilinipa wakati mgumu sana kwa kile kipindi lakini namshukuru Mungu nimesahau yote na maisha yanaenda kikubwa mwombe Mungu akusaidie uvuke salama kwasababu hapo ndipo wengi wanapoaribikiwa
 
mh huo mzaha sasa hakuna mapenzi ya kweli hapo huyo msichana anakuchezea, maana minavyojua msichana akiwa yuko siriazi na mtu hawezi kuwa na mzaha kiasi hicho
 
Back
Top Bottom