Nimemrudisha mke na mtoto ukweni baada ya kukosa kazi kwa miezi 3

Michael Ngusa

JF-Expert Member
Aug 4, 2014
1,637
458
Wakuu,

Habari za kushinda!

Naandika nikiwa na uchungu sana baada ya Breakdown ninayoipitia. Career yangu ni kwenye Media industry, tangu niache ajira yangu ya kwanza mkoani ambayo nilistawi kiasi cha kuoa na kuwa na kwangu, nikahamia Dar ambapo nilifanikiwa kupata kazi na kuendesha maisha lakini kwa mahangaiko makubwa kiasi cha mwaka mzima wa 2015 kuwa ni mwaka wa dipression kwangu.

Bahati mbaya, mwishoni mwaka jana nikapoteza ajira yangu, licha ya kutafuta huku na huko kwa njia zote na kuhudhuria interview nyingi, sijapata kazi hadi muda huu. Hivyo nikaona nisije kuadhirika ndani, nikaamua kumrudisha mke na mwanangu mchanga ukweni wanisubiri niendelee kupambana.

Nilibakiwa na Laptop na Smartphone yangu ambavyo nilivitangaza mnada hapa jamvini kwa bei ya hasara ili nisukume siku, sikupata mteja, mwisho wa siku vikaja kuibiwa vyote sebuleni kwangu na majirani wamekana kutofahamu chochote. Angalau freelancing ilikuwa inaniokoa na hicho kilaptop, pia kilikuwa na Data zote za kujiajiri kwa kufungua kampuni ya Web Design.

Nina elimu ya chuo, vyeti safi, uzoefu wa miaka 3 na Portfolio nzuri kabisa kwenye Print Media, TV Broadcasting & Advertising, lakini nimetumia kila senti niliyonayo bila mafanikio. Wakuu nimekata tamaa na nina uchungu bila kuwa na wa kumlaumu kwasababu sioni nilipokosea au sababu ya changamoto mfulilizo kiasi hiki.

Nilianza kuhoji uwepo wa Mungu na kwanini hajibu maombi yangu, kwakweli nikamezwa na hoja za kipagani na kuanza kuukana Ukristo wangu, kwamba kama kweli kungekuwa na Mungu, kwanini aruhusu hadi familia isambaratike kwa kukosa chakula na kushindwa kujiendesha? Ila baadae nikawaza kuwa unapokuwa kwenye shida sio kipindi kizuri cha kuanza kuquestion uwepo wa Mungu.

Siku za hivi karibuni nimeanza kugoogle njia za kujitoa uhai na nikaambulia ufahamu wa kwamba njia rahisi ni Drug Overdose, kwa jinsi ambavyo sitaki kuwapa watu shida, nafikiria kwenda kujioverdose msituni hata maiti yangu isiwape watu gharama za mazishi.

Nimechoka sana ndani, nimekuwa nikiwapigia simu watu mbalimbali hadi wale wa utotoni, angalau nimekuwa nikihisi faraja flani lakni mwisho wa siku bado nakuwa peke yangu. Nilikuwa ninasaza chakula, nilikuwa nina kila kitu na kazi ndio ilikuwa kitu kikubwa, sasa sipati hata kazi, kwamba nijijenge tena, afya yangu vibarua vya zege haivimudu, ndio maana nilikimbilia shule. Pole hazinisaidii, kwenda kanisani naona hiyo nauli bora iwe lunch, sijui nifanye nini.

Hapa mfukoni imebaki elfu 10 tu, nawaza sijui wiki ijayo itakuwaje. Nilikuwa nabrowse JF kwenye Smartphone, sasahivi nipo Internet Cafe niko down sana washkaji.

UPDATE:
Ndugu zangu,

Kwanza mfahamu kwamba natumia Kinokia cha Tsh 15,000 (true) kusoma jumbe zenu na kila baada ya muda flani ninalazimika kupanda gari kutoka Misheni hadi Mtongani kwenda kuwajibu Internet Cafe.

Bila jumbe za kutia moyo humu ndani mimi leo nisingekuwepo. Nimekuwa nikisoma jumbe zenu huku nikibubujikwa na kujihurumia sana. Hadi jana saa 4 usiku, nilipokuwa nikiendelea kusoma jumbe za wanaJF, mke wangu alinipigia simu kunijulia hali (hatujaongea tangu aende kwao) nikafuta machozi ili niongee katika hali ya kawaida. Hakugundua lolote, basi tukatakiana usiku mwema.

Leo saa 9 mchana nikiwa najiandaa kwenda kwa baba mdogo huko Kitunda (ndio mtu wa mwisho ninaweza kulazimisha kwenda kufia mlangoni kwake), nikapokea simu ya mwanaJF, tukaongea, nikamweleza hali ilivyo, basi tukaagana. Baada ya dakika 2, Tsh 100,000 ikaingia kwenye simu! Kidogo nianguke.

Nikampigia kumshukuru sana, pia akasema niandike namba yangu. Ni Tigo: 0653 257566. Basi nimeahirisha kwenda kwa bamdogo niko Mtongani ninaandika. Hadi jioni tena, wacha nirudi nyumbani.

UPDATE 2:
Ndugu asanteni sana. Nimepokea msaada wa Tsh laki 1 ingine kutoka kwa mwanaJF ambaye na yeye anaishi nje ila ametumia mwenyeji aliye hapa Dar. Wakikubali nitawajulisha ID zao. Ila kikubwa ni shkrani za dhati kwa jumbe zenu na fedha zenu.

Asubuhi ya leo pia niliitwa na Afisa Jeshi mmoja ambae ni mwanaJF, nikamtembelea hapo kambini, kanitia moyo, kanipa chakula na nimepata tumaini. MBARIKIWE NDUGU ZANGU.
 
Pole sana...kujiua ni kumsaliti mkeo na mwanao
wewe mwenye akili timamu na elimu na uzoefu wa kazi ukijiua
mwanao afanyeje?mkeo nae afanyaje?

ulijiua ina maana wewe ni mbinafsi sana na unajisikia mno
hutaki kupitia 'mateso' yako ambayo karibu kila mtu huyapitia...
Soma historia ya Rais wa China wa sasa...
alidhalilishwa mno na serikali kwa makosa ya wazazi wake
almost alikuwa kama mfungwa
now ndo Rais wao...na hajaacha ku smile.....
 
I can feel ur pain!!,trust God he have a plan with you!!..
Kujiua sio Lengo lake!!,angetaka ufe tayari ungekuwa umekufa!.

Fikiria katika vipaji vyako!!,nini unaweza kufanya!!...
Pika chapati kwa kuanzia uza!!,kaanga mandaazi,
tafuta mkaa hata anza na gunia 1 linalipa...

Usione Aibu kwenye kutafuta!..
Ukifa wew Tumaini la familia yako linakufa pamoja na ww!!!
 
Pole sana...kujiua ni kumsaliti mkeo na mwanao
wewe mwenye akili timamu na elimu na uzoefu wa kazi ukijiua
mwanao afanyeje?mkeo nae afanyaje?

ulijiua ina maana wewe ni mbinafsi sana na unajisikia mno
hutaki kupitia 'mateso' yako ambayo karibu kila mtu huyapitia...
Soma historia ya Rais wa China wa sasa...
alidhalilishwa mno na serikali kwa makosa ya wazazi wake
almost alikuwa kama mfungwa
now ndo Rais wao...na hajaacha ku smile.....
pole hali yako inafanana na yangu tofauti ni kuwa wewe umesoma mimi hapana wewe unamke mimi hapana twende PM tukajue jinsi ya kumfunga ajira kengere
 
Mkuu take the positive part of it. Mshukuru Mungu kwa kila jambo ulipitialo halafu hakuna jipya ambalo wengine hawajapitia binafsi sina kitu chochote lakini nitaku PM.
Sina maneno Mengi sana ya kukufariji lakini take it as a Challenge and discover the opportunities from those challenges that are facing you.

Updates:

Nimeku PM tangu jana hadi leo tarehe 17 hujajibu.
 
Pole sana mkuu..ila usikate tamaa na endelea kumtumainia mungu anasikia vileo vyetu
 
Maisha yetu ni mfano wa boti iliyopo safarini....na wewe ndiye nahodha wa chombo chako....uelekeo wa boti yako kuelekea kwenye fukwe tulivu na yenye upepo mwanana unategemea na juhudi zako za kupiga makasia na kupambana na mawimbi makali ya bahari.....kuwaza na kusikitika au hata kulia hakujawahi kumsaidia nahodha kukiongoza chombo kufika salama bali uvumilivu na umakini pindi akumbwapo na mawimbi makali ndivyo vinavyomhakikishia nahodha uhakika wa kufika salama ufukweni.....kumbuka kuwa bahari tulivu haimpimi nahodha wa meli.....

Katika ulimwengu huu uliojaa misuko suko na mihangaiko ya kila namna kila mmoja anapambana na mahangaiko yake kwa style anayoona inamfaa na kumletea ushindi.....
Kuna wengine wamewekeza mapambano yao kwenye biashara na shughuli zingine za ujasiliamali pia kuna wengine wanapambana kwenye kilimo......pia kuna wengine wanapambana kwenye uchawi...lakini mapambano yote hayo lengo lake ni moja ni kujikwamua kutoka katka hali mbaya kwenda kwenye uhafadhali........

Habari njema ni kwamba katika kupambana huko tuna uhuru wa kufungua milango yote ya vita ....hivyo si vyema kukomalia mlango mmoja usiofunguka na kuuacha milango mingi iliyowazi kwa ajili yako.......Hivyo ni dhambi kwa kiumbe mwenye uhai na afya njema kukata tamaa.....kumbuka kuwa aliyefeli ni yule aliyefariki tu....ingali uko hai bado haujafeli....

Endeleza mapambano mambo mazuri yapo mbele yanakuja.......
 
kaka usijiue mkuu...kaza..mbuna ata sisi ajira atuna lakin tunakaza mkuu...kausha acha hizo fikra za kujiua mkuu...kausha bwana ...tafuta ata bidaboda urudishe mpira kwa kipa mkuu
 
Hayo hayajakukuta ww tu sshv dunia iko ktk crisis ht me nimepoteza kazi mwaka huu ila huwezi amin najipanga upya maana mungu hawezi kukupa mtihani ambao utakushinda by the way mlango 1 ukifungwa miwili hufunguka.kumbuka haupo mwenyew wapo wengi me mmojawapo ila naamin kwamba mungu ndo muweza wa kila kitu
 
Wakuu,
Habari za kushinda! Naandika nikiwa na uchungu sana baada ya Breakdown ninayoipitia. Career yangu ni kwenye Media industry, tangu niache ajira yangu ya kwanza mkoani ambayo nilistawi kiasi cha kuoa na kuwa na kwangu, nikahamia Dar ambapo nilifanikiwa kupata kazi na kuendesha maisha lakini kwa mahangaiko makubwa kiasi cha mwaka mzima wa 2015 kuwa ni mwaka wa dipression kwangu.

Bahati mbaya, mwishoni mwaka jana nikapoteza ajira yangu, licha ya kutafuta huku na huko kwa njia zote na kuhudhuria interview nyingi, sijapata kazi hadi muda huu. Hivyo nikaona nisije kuadhirika ndani, nikaamua kumrudisha mke na mwanangu mchanga ukweni wanisubiri niendelee kupambana.

Nilibakiwa na Laptop na Smartphone yangu ambavyo nilivitangaza mnada hapa jamvini kwa bei ya hasara ili nisukume siku, sikupata mteja, mwisho wa siku vikaja kuibiwa vyote sebuleni kwangu na majirani wamekana kutofahamu chochote. Angalau freelancing ilikuwa inaniokoa na hicho kilaptop, pia kilikuwa na Data zote za kujiajiri kwa kufungua kampuni ya Web Design.

Nina elimu ya chuo, vyeti safi, uzoefu wa miaka 3 na Portfolio nzuri kabisa kwenye Print Media, TV Broadcasting & Advertising, lakini nimetumia kila senti niliyonayo bila mafanikio. Wakuu nimekata tamaa na nina uchungu bila kuwa na wa kumlaumu kwasababu sioni nilipokosea au sababu ya changamoto mfulilizo kiasi hiki.

Nilianza kuhoji uwepo wa Mungu na kwanini hajibu maombi yangu, kwakweli nikamezwa na hoja za kipagani na kuanza kuukana Ukristo wangu, kwamba kama kweli kungekuwa na Mungu, kwanini aruhusu hadi familia isambaratike kwa kukosa chakula na kushindwa kujiendesha? ila baadae nikawaza kuwa unapokuwa kwenye shida sio kipindi kizuri cha kuanza kuquestion uwepo wa Mungu!

Siku za hivi karibuni nimeanza kugoogle njia za kujitoa uhai na nikaambulia ufahamu wa kwamba njia rahisi ni Drug Overdose, kwa jinsi ambavyo sitaki kuwapa watu shida, nafikiria kwenda kujioverdose msituni hata maiti yangu isiwape watu gharama za mazishi.

Nimechoka sana ndani, nimekuwa nikiwapigia simu watu mbalimbali hadi wale wa utotoni, angalau nimekuwa nikihisi faraja flani lakni mwisho wa siku bado nakuwa peke yangu. Nilikuwa ninasaza chakula, nilikuwa nina kila kitu, na kazi ndio ilikuwa kitu kikubwa...sasa sipati hata kazi, kwamba nijijenge tena, afya yangu vibarua vya zege haivimudu, ndio maana nilikimbilia shule. Pole hazinisaidii, kwenda kanisani naona hiyo nauli bora iwe lunch, sijui nifanye nini.

Hapa mfukoni imebaki elfu 10 tu, nawaza sijui wiki ijayo itakuwaje. Nilikuwa nabrowse JF kwenye Smartphone, sasahivi nipo Internet Cafe...niko down sana washkaji.
Ukijaribu kufatilia hakuna tajir ambae hakupata big failure ila sshv ndo wanaendesha dunia.dont worry about tommorow sbb hujui nn kitakuja.me nilichojifunza ktk maisha chchte kibaya au kizur kina mwisho na nimeshuudia kbs.life can have ups and downs,pull urself together good things are coming soon
 
Oooh it's very touching situation.
Anyway fanya kitu kimoja usifikirie sana maisha mazuri uliyokuwa nayo before kipindi hicho unamaisha mazuri.
Cha kufanya sasa angalia Katika watu ulio nao karibu chagua mmoja unaeona anaweza kukusaidia jiunge nae kwenye kazi anachofanya. For the time awe anakupa tuu hela ya kula ila huku ukijifunza hiyo kazi ili one day uweze kutafuta mtaji hata kwa kukopa uendeshe biashara hiyo ambayo utakuwa unajua.
Nilipitia situation kama yako miaka mitatu iliyopita nilitumia approach niliyokupa hapo juu. But believe me I am now very proud. Professionally mimi ni accountant with MBA nilisota sana bila kazi. Ila I am now owning construction company na nina mtaji wa kutosha kabisa.
Umeona from accountant to construction ni ngumu but I am very smart now in this new industry.
All the bests
 
Huwa napata shida sana kumshauri mtu ambaye anatamani kujiua. Kwa nini nijiue. Weye, nakuuliza upo tiyari kusoma ushuhuda wangu?? Haya nakuambia japo kwa kifupi sana. Ukitaka ni PM ntakupa namba yangu uni-beep tu nkupigie mimi. Kama ni mtu wa kujiua ilikuwa ni mimi 1990. Sintausahau mwaka ule. Ulikuwa mwaka mbaya mno mno mnooo.
Nilirushwa fedha taslimu 10 milion. (Ten million). Nilikuwa na mpango wa kununua mabasi 2 Scania, nianzishe biashara ya usafirishaji. Nikarushwa na rafiki yangu kipenzi mchana peupeeee.
Akaenda kufunga ndoa, akafanya tafrija ya kuua mbwa kwa shibe. Kumbuka, hakunialika, hakuniambia bali aliondoka kwenda kwao huko mikoa ya ziwa. Nikabaki kwenye ofisi yetu, nakodolea macho barabara kuwa atarudi lini. Akala mbinu na meneja mmoja wa Bamk waka draw fedha yote kwenye akaunti kwani walikuwa na saini yangu hivyo ya kwake haikuwa shida.
Aliporudi, bila hata aibu akanipeleka polisi, nikabambikiwa kesi kuwa nilikula pesa za ushirika. Mpakanichomoke, keshahama mji. Nikakosa mshitaki nikaachiliwa.
Wazo la kwanza, nikajiapiza kumuondoa sayari hii. Mungu akanionya kitendo hicho nisikifanye. Nilikuwa nataka kwenda kwao niufagie ukoo wote kwa shaba.
Mtoto wa kiume niliathirika mjini, nikauza kila kitu nilichokutana nacho ndani ya nyumba, mpaka nyumba. Kisirani nilichokuwa nacho, senti haikukaa nami. Nilibuni kila biashara, vyote vikaangamia.
Kumbe, ni wito wa kumtumikia Mungu ulikuwa unanisumbua. Leo, baada ya kumtii Mungu, maisha yangu safiiii. Usiwaze kujidhuru.
Tubu toba ya "Mavumbi na majivu" kama Ayubu weye. Usithubutu kuwaza ati hakuna Mungu. Mungu yupo, alikuwepo na atakuwepo milele.
Neno moja tu, Ulijua kama siku leo itapita?? Kesho inakuja nayo itaitwa leo. Tegemea muujiza wako. Tubu, mrudie Mungu aliye baba yako. Ndiye amekupa uhai wako wa leo, hata kesho yako ipo mikononi mwake.
Ukitaka ni PM nina mengi ya kukueleza. Sm yangu haifungwagi 24/7
 
Mie naamini ujasiri wa maisha unaanza jinsi ulivyolelewa.
We jiulise kuna watoto wale wa ombaomba ambao hukomaa na jua na mwisho wa siku wazazi wao wale.Na siku zinasonga.Itakiwa wewe msomi.
Issue ya kukomalia taaluma uliyosomea ndio iwe chanzo cha ajira yako ni janga la taifa.Sio wewe tu.
Kuna watu humu unaona wanaukabia mjini,ila maisha ni siri ya mtu,kuna wanaorudi makwao kwa mguu.

Tafuta sehem ijotolee kufanya kazi bure,then hapo utapata njia na mwanya,kisha tafuta rafiki wa karibu saana ndani ya sehem hiyo uwe muwazi kwake,basi unaweza kukuta unapata mwanga.
Asikudanganye mtu,mtu yoyote anaeshi Dar,na akiwa na uhakika wa kula mlo mmoja tuu,basi Jiji kaliweza
Sasa fanya urafiki na mshkajia angalau uwe unapita hata kwao kula,kisha unasongesha siku za mitego.
Wengine hapa Historia zetu zinatisha,mie nilisoma chuo fulani,basi huwezi amini pesa ya kula nilikuwa sina,ila mungu alichonisaidia nikwamba nilikuwa najua saana kupika,maana nimekaa sana na Bibi.Basi jamaa walikuwa wananikubali saana kwa kupika,huwezi amini ndio nili save kwenye maisha yale,wao wanakula Batamie ndio mpishi wao,na hali ngum ya maisha na ndio nilikuwa pia nawaburuza kwenye masomo pale chuo,maana wengi walikuwa na uhakika wa maisha,ila mie ile hali ilikuwa inanipa changamoto.
Baadhi yao walikuwa walevi,basi wakirudi tu,utasiki oyaa we Dada hujapika?yaani mie Mwanaume wananiita Sister kisa nawapikia,ila ikifika kesho mtu anakuomba samahani,na ukiwa muelewa unapotoezea.
Mkuu yapo mengi,we hayo yako cha mtoto saaana,komaa tu
 
Dah iyo hali naijua vizuri sana ila jikaze usijitoe uhai pambana bro ndio dunia yetu hii nilishawai kuwa na mawazo hayo maisha yalipokuwa magumu ila si vyema jitahidi ufanye biashara yako mwenyewe achana na biashara za kuajiriwa
 
Pambana kaka .....maisha ni mapambano
Kingine take risks ....jaribu kufanya jambo jipya linajitokeza mbele yako
Grab any opportunity you come across ... Ukijituma utafika mbili Sana ..... Usikate tamaa ....you were not born to quit ..... Usife moyo .
 
I know you really don't want to die, but you are in pain and you just can't cope with the pain. Unahitaji ile "relief" tu ili ujisikie kawaida tena. Inawezekana ikawa ni maneno ya kukutia moyo especially kutoka kwa watu ambao wamepitia/wanapitia magumu zaidi yako

Kuna muda unahisi kama umemkosea Mungu vile, yani kama Mungu hayupo, otherwise kwa nini hakuoni wewe, usikufuru mpendwa. Chochote unachopitia jua Mungu ana makusudi kukupitisha huko, na ana kitu kikubwa anachotaka wewe ujifunze katika mapito hayo, otherwise asingekupitisha huko. Na amini tu ule muda ambapo umekata tamaa kabisa, unahisi huna ulichobakiza, huoni tena reason ya wewe kuishi,... basi amini "Upenyo wako upo karibu"

Hakuna kitu kibaya kama kuishi bila kazi, let alone kukosa hela. Kila mtu anapenda aishi with a "purpose", unaamka, unafanya kitu chenye faida unarudi nyumbani. Lakini wakati wewe unaona ujiue kwa sababu huna kazi, jua kuna mtu on his/her sickbed anaomba maombi yote Mungu asimchukue, amuache tu aishi hata kama hatokuwa na uwezo wa kunyanyuka, kujinyoosha, kutembea etc.
Badala ya kulaumu Mungu kuwa huna kazi, em kaa chini afu anza kulist vile vitu ambavyo Mungu amekupa. Afu jiulize ni watu wapo salama muda huu.. wana afya nzuri, wana peace of mind (ingawa hii hauna kwa sasa), wanabreath, wanatembea, wanaona, wanaweza kujua nini kinaendelea duniani. Wangapi wanatamani wangekuwa na mke, wangekuwa na mtoto, familia nzuri, etc. Usione watu wanacheka, Kila mtu ana mapito yake anayoyapitia kimya kimya. Kuna watu wana hela lakini wapo vitandani na hela zao hazina chochote cha kuwasaidia. Wewe hivyo ulivyo je ni zaidi ya hao wengine?


Please you just need to talk to a person ambaye atakupa ushuhuda wa magumu yake, mcheck hata mangatara hapo juu . Au fanya hivi nenda kwenye hospital yoyote karibu yako, Jitahidi kuwatembelea wagonjwa wengi as utakavyoweza. Afu uone kama utajisikia kujiua tena. Please usiwaache mkeo na mwanao wateseke, uwepo wako kwao hata bila pesa ni muhimu kuliko kitu chochote kile, usiwanyime hiyo haki yao please
 
Back
Top Bottom