Wakuu maji yamenifika shingoni,mwaka jana mwshoni,nlikutana na binti mmoja,mwanafunzi wa mwaka wa pili chuo kikuu kimoja dodoma,baada ya siku kadhaa,nikatembea nae,lakini sikuwa na mapenzi kwake,lakini yeye alinipenda sana,akanisumbua kwa muda mrefu,nikaamua kumweleza ukweli kuwa mimi nina mchumba,lakini yeye hakuridhika,siku moja akang'ang'ania kuja kwangu usiku,alipokuja kwa bahati mbaya siku hiyo akashika ujauzito,sasa anawasiliana na mpenzi wangu baada ya kuiba namba kwenye simu,na ameng'ang'ania anataka kuzaa na mimi,kweli sina mapenzi naye na ninamchukia sana kwa haya alotendea,kanitegea mimba akidhani ntamuoa,siwez kumpenda kamwe,jamani nisaidieni kunishauri.