Nimemkuta yu mjamzito!

Ukiamua kulea mimba ya mbakaji wako mimi siwezi kuishi na wewe tena kama mume na mke. Nitakuacha niendelee na maisha yangu.

Ooh kama ni hivyo basi mbona atakuwa karahisisha kazi. Nitakachofanya ni kusepa na kusonga mbele na maisha yangu. Yeye hanipi uhai wangu. Nilikuwepo kabla yake na nitakuwepo baada yake.

Hudhani kama atakuja kukukosea tena? Kama hakushindwa kujizuia kukosea mara ya kwanza ni nini kitakachomfanya asikosee safari zijazo? Na kwenye kuchiti hakuna cha eti ulikosea mara moja maana hilo tendo la ngono ukiondoa kubakwa huwaga ni la kupangwa.

Kuna mchakato mzima unaolitangulia. Kuna kupapasana, kuna kuvua au kuvuana nguo, kuna kujiweka sawa katika mtindo mtakaotumia na kadhalika na kadhalika. Sasa hilo mtu unaweza ukaliita ni kosa la bahati mbaya? Abadani asilani, hilo ni kosa la kupangwa.

Ila mwisho wa siku, kilicho muhimu na cha msingi ni uamuzi wa mtu husika. Kama mtu akiamua kumsamehe mwenzake baada ya kutendwa hivyo basi huo ni uamuzi wake na ana haki ya kuamua alivyoamua. Binafsi siwezi kusamehe. Nitakuacha papo hapo pasipo hata na majadiliano. Wanawake wako wengi mno kuendelea kung'ang'ania kubakia na wewe kama vile sina options zingine maishani.

siwezi kukupinga utakavyoamua ila tukio kama hilo ni ngumu kuwa ushajua utafanyaje. Inawezekana yatakapokukuta utafanya tofauti na hayo.

siwezi kukupinga utakavyoamua ila tukio kama hilo ni ngumu kuwa ushajua utafanyaje. Inawezekana yatakapokukuta utafanya tofauti na hayo.

Hapana! Ninajijua nilivyo na heshima yangu kwangu ni kitu cha muhimu sana. Sipendagi kabisa kuvunjiwa heshima yangu. Niliyoyaandika hapa ndiyo nitakayoyafanya na sitashangaa kama nikifanya zaidi ya haya!

Mkuu..hiyo issue inakuuma kwa sababu ni 'Caught Red Handed' kwa nini usijiulize kati ya watoto 100 wanaozaliwa 25 si wa baba halisi.. Kwa nini usijiulize inawezekana mtoto mmoja unaosema wako lakini ukweli si wako? unawezaje kwa sasa kuendeleza tabasamu wakati kumbe ni mmoja wa wadau wa hii issue?

Kutatua hiyo issue...Jiulize

• Wewe ni msafi? umeshatafuna wazungu wangapi? Je mmoja ya hao wazungu kondomu haikutoboka na labda huyo mzungu umemwacha mjauzito bila kujijua?
• Jiulize kwa nini mama anajiamini hadi kukuachia uone ametoka nje na kukosa uaminifu..labda alikuwa anakusubiri ili mmalizane..
• Haina haja ya ku-panic..kwani mkeo ni binadamu kama wewe..
• Kuna asilimia 98% mtaachana lakini pia kuna asilimia 2% ya mwanaume wenye roho ngumu ambao watakubaliana na wake zao kulea huyo mtoto..kwa makubaliano maalumu..mmoja wapo linaweza kuwa kusahau yaliyopita..kumbuka unavyofikiri wewe sivyo navyofikiri mimi au yule'

Mkuu..hiyo issue inakuuma kwa sababu ni 'Caught Red Handed' kwa nini usijiulize kati ya watoto 100 wanaozaliwa 25 si wa baba halisi..

Hizi takwimu umezitoa wapi? Naomba chanzo tafadhali. Na "baba halisi" ni yupi? Ni yule atoae mbegu zake au yule aleae?

Wewe ni msafi? umeshatafuna wazungu wangapi? Je mmoja ya hao wazungu kondomu haikutoboka na labda huyo mzungu umemwacha mjauzito bila kujijua?

Wazungu wanahusika vipi hapa?

Ni vyema wakatengana ampe talaka maana inawezekana kabisa usiku mmoja akaamka na kuamua kunyonga hicho kichanga kitachozaliwa kwa uchungu, wakati kichanga chenyewe hakina hatia.

Si unasikia siku hizi imekuwa fashion huko vijijini baba akihisi tu kuwa mtoto si wake ananyonga, jee wewe mwenye uhakika?

Cha kufanya na cha busara ambacho ninamshauri kila binadamu afanye ni kwanza kuuliza ni yepi yaliyomsibu..., Ni vibaya sana kuhukumu mtu bila kujua chanzo au sababu..., just imagine kama alibakwa....? Hivyo basi atakuwa anamuhitaji mtu wa karibu yake (wewe) ili kumsaidia katika hili janga, na nyie wawili mnaweza mkaleta kiumbe duniani ambacho otherwise kisingepata mapenzi ya kutosha...

Kwahiyo cha kufanya ni kumuuliza ni nini kilitokea na kama ni mtu unaemjua na unajua tabia zake itakuwa rahisi kujua kama anakudanganya au ni kweli yaliyompata hayakuwa kwa idhini yake..., Na kama amekuchoka basi atakwambia hivyo basi kila mmoja kuchukua hamsini zake

Nikipunguza sample na ku-focus Tanzania wigo unaongezeka toka 25% niliyosema hadi 60% hivyo basi Tanzania kati ya watoto 100 wanaozaliwa 60 tumezingiziwa. na 40 tu ndio wa ukweli. soma thread hapo chini ambayo ilipita hapa JF ..utapata chanzo ..

https://www.jamiiforums.com/mahusia...he-biological-fathers-nendaeni-mkapime-2.html

Asante.

Wewe ni msafi? umeshatafuna wazungu wangapi? Je mmoja ya hao wazungu kondomu haikutoboka na labda huyo mzungu umemwacha mjauzito bila kujijua?

Na hii ya wazungu inahusika vipi?

Nikipunguza sample na ku-focus Tanzania wigo unaongezeka toka 25% niliyosema hadi 60% hivyo basi Tanzania kati ya watoto 100 wanaozaliwa 60 tumezingiziwa. na 40 tu ndio wa ukweli. soma thread hapo chini ambayo ilipita hapa JF ..utapata chanzo ..

https://www.jamiiforums.com/mahusia...he-biological-fathers-nendaeni-mkapime-2.html

Nimeisoma hiyo makala na wewe unapotosha hapa! Hiyo idadi ya asilimia ni yale wale waliokuwa na utata tayari na wakayapeleka matatizo yao kwenda kutatuliwa kwa vipimo na si ya watoto wote wazaliwao Tanzania.

Hebu soma hiki kipande kwa utaratibu halafu ulinganishe na ulivyoandika

The Government Chemist Laboratory Agency has said that among the 250 deoxyribonucleic acid (DNA) samples it received for disputed parentage cases in the year 2005/2006, at least 60 per cent of the cases proved that the male parents were not the biological fathers of the children.

Na hii ya wazungu inahusika vipi?

Ah..nilisahau ya wazungu .. hiyo ni nadharia ya uandishi kwani mtoa mada alisema
Hebu tuchukulie kwamba umekwenda kusoma nje ya nchi,
kwa walio wengi kule uswazi ..nje ya nchi sio Malawi au Burundi ni "Ulaya" hata ikiwa United States of America.. ..

Kikubwa umeelewa..'kabla ya kuona kijiti kwenye jicho la mwenzako..toa kwanza boliti kwenye jicho lako!

Jamani tuwe wakweli sawa alishindwa kuvumilia miaka 2 lakini mimba hapana haikubaliki,mi mjomba wangu ilimtokea hii baada ya kurudi maskini aliugua hajachukua hata mwezi akafariki yaani inauma saaana.

Ah..nilisahau ya wazungu .. hiyo ni nadharia ya uandishi kwani mtoa mada alisema kwa walio wengi kule uswazi ..nje ya nchi sio Malawi au Burundi ni "Ulaya" hata ikiwa United States of America.. ..

Hata Uchina na Japan?

Hebu tuchukulie kwamba umekwenda kusoma nje ya nchi, au umekwenda mbali sana na nyumbani kwako kikazi. Umekaa huko kwa miaka miwili . unaporudi, unakuta mkeo ni mjamzito! Hebu niambie ungefanya kitu gani?

Je na wewe huko ulikoenda hujaacha mtoto virtualy or physically ? teh teh teh inawezekana ulisusa kwa kipindi akajua umeshadwkaa na wakati akiwa down akapata wa kumliwaza.

Utakuwa muongo uksiema vitually huko ulioenda usoma hujaacha watoto japo kwenye condom.

Ingawa ni mamuzi magumu lakini inabidi uzingatie vitu vingi sana . lakini kwa maamuzi ya haraka haraka ndo hayo divorce

Ndio msamahe, tatizo ni mimba au? Kama ni udanganyifu hata wewe utakuwa umeufanya. Kwa hiyo samehe 2 jifanye mlipeana mimba via bluetooth......

Back
Top Bottom