Nimemkumbuka Nyerere namlilia tena Nyerere.

Kaa la Moto,

Nakushukuru kwa kuleta topic ya kumuenzi baba wa taifa kama angekuwa hai asikuepo mtu wa aina yeyote anayeitwa fisadi na mtu alikosa maadili kwani angemtosa kabisa hasa wale watu wanaitwa maviga matatu na siyo mapacha matatu angekuwa tayari ameshughulikia kisawa sawa!
 
Si kweli kwamba haya mashirika yalikufa akiwa hai nadhani huu ni upotoshaji.
Anyway, ebu tuangalie vision aliyokuwa nayo. Huu uroho wenu baadhi ya watanzania ndio mwanzo wa kufa mashirika haya lakini vision yake ilikuwa perfect! Na walioua mashirika hayo ndio bado mko madarakani. Ole wenu siku watanzania tukiamka usingizini mtatukoma!

Unajua hata mimi ukinipa uongozi leo ujue naweza kutaifisha mali ya wezi wote wa raslimali zetu. Najua kuna watu wengi wamewaibia watanzania kwa nini wapete wakati watanzania wanatoswa? Hakika na mimi ningehukumiwa kwa dhambi hiyo ya kutaifisha.

Kama ni kweli mbona wakati wa utawala wake tulikuwa na uhaba mkubwa wa bidhaa?
 
Kwani hivyo viwanda aliweka wanaye au mkewe kuvimiliki kama wale waliojimilikisha kiwira na mengine mengi kama hayo? Je kuna mtoto wake aliye kuwa tajiri kupitia urais wake? Na wewe jiulize ni kwa nini alikuwa na akili ya kuondoka mwenyewe madarakani bila ya kusukumwa? Narudia tena, ‘The unconscious mind is often sentimental’.
 
Wapuuzi wachache leo hii ambao wanajidai wasomi wasio na msaada wa kuonekana kwa vitendo wanadai eti alitunyima TIVIII.....wengine wanadai eti alikua na udini kwa kuwabania waislam(upumbavu gani huu), mbona wengine wakiwamo na wazazi wetu walisoma kwa usawa tu na wakristo. Kikwete, Mwinyi na wengine kibao ambao ni waislam wangepata nafasi za uongozi enzi zake? Hata kama mashirika na viwanda alivyoanzisha vilitetereka walau basi tungetafuta njia ya kuboresha yaendelee vizuri kwani alikwisha tuonyesha njia. Tena kuna wapumbavu zaidi wanaongelea eti Uhuru hakuupigania yeye, kajivisha tu hiyo sifa, sawa hata kama ni hivyo, lakini mbona hakujirimbikizia mali kama watawala wengine waafrika tunaowashuhudia wakianguka kwa aibu kubwa ambao alikua nao kwenye utawala wa nchi za kiafrika? Mie ni kizazi cha Tanzania(naimani utanielewa kwamba nimezaliwa baada ya Muungano) lakini najaribu kulinganisha mema na mabaya yake naona mema ni mengi tena hao waliomfuata mema ni almost 0.001% ya matendo yao wakati mabaya ni zaidi ya 99%.

Sasahivi hakuna hata kwenye unafuu, ccm-wanajivua gamba, wananchi-hali ngumu ya maisha, serikali haina muelekeo tena hata hao mafisadi amani imeanza kuwatoka maana wanajua hatma yao haiko mbali.
 
Kama ni kweli mbona wakati wa utawala wake tulikuwa na uhaba mkubwa wa bidhaa?
Ni kweli kulikuwa ana uhaba wa bidhaa lakini hapa nimeweka wazi kwamba maono yake yalikuwa makubwa zaidi ya uhaba unaojaribu kuupaka rangi hapa. Hata leo tuna uhaba mkubwa wa bidhaa kwani ulishakwisha? Tumeongeza viwanda vipi ili kuuondoa?
Leo kuna kila aina ya takataka toka china lakini hata uimara ni zero. Uwezo wa kuvinunua hakuna.
Tulikwa na uhaba mwingi kwa kuwa hatukuwa na viwanda vya kutosha. Tulitakiwa kutumia nyakati hizi kuongeza viwanda na sio kuviua.
Naomba ujibu swali langu je kati ya viwanda vyote alivyoanzisha nilivyotaja havikuwepo kweli kwa juhudi zake?
 
Eeeeeeeeeeeee, tata ejo, uchungu jamani, nami namwaga machozi yangu jamani!:Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::help:
 
Back
Top Bottom