sembo
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 4,350
- 3,451
Tangu karne hii mpya ianze, mnamo mwaka 2000, mmoja kati ya wachezaji bora kabisa toka nchini kwetu Tanzania [kama si bora kuliko wote].. niliobahatika kumshuhudia ni "Mtalamu" Haruna Moshi Boban.
Boban alikua ni mchezaji mwenye akili nyingi sana za mpira pamoja na kipaji halisi alichojaaliwa na Mwenyezi Mungu.
Haruna alipata mafanikio makubwa katika uchezaji
wake wa soka alipokuwa katika timu ya Simba S.C kwani aliweza kuchukua makombe ya ligi kuu katika misimu ya 2003/2004.. 2006/2007.. pamoja na 2011/12 [Invincible Simba S.C ikimaliza msimu bila kufungwa mechi hata moja, kwa kumchapa mtani 5-0 katika mechi ya mwisho].
Boban ameitumikia Simba S.C kati ya miaka 2004 mpaka 2009 na 2011mpaka 2013.
Mambo yaliyofanya nimkumbuke.. Haruna Moshi Boban, ni haya hapa chini;
1. Uwezo mkubwa sana aliokua nao wa kutengeneza na kufunga magoli, pia alikua na jicho kali sana la pasi muhimu [kwake kutoa pasi mkaa ilikua ni mwiko].
Pia Boban alikua na uwezo wa kufanya vitu vya kustaajabisha [madoido] kila aingiapo uwanjani.. ambavyo viliwaacha mashabiki na maswali kibao.. kama vile.. "Amewezaje?!".. " Haiwezekani bhana!?".. "Boban ni wa ulaya!!".. " Duh.. Kama Gaucho vile?!" .. n.k.
2. Kipaji cha hali ya juu cha kuudhibiti, kukaa, na kuuamuru mpira ufanye anachotaka.. Hakua na papara wala kuogopa kupewa mpira na wenzie uwanjani.
Pamoja na uwezo huo hakupenda kukaa na mpira lakini pindi apatapo mpira [ndo utajua kwanini alipewa a.k.a ya Boban] kwani hujua nini cha kufanya juu ya huo mpira, kabla hata hujatua mguuni mwake.
3. Kama ilivyo ngumu kwa Ngamia kupenya katika tundu la sindano, ndivyo ilivyokua ngumu [tena sana tu] kwa Boban kupoteza mpira ulio mguuni kwake.
Boban alikua na uwezo mkubwa sana wa kuulinda mpira ukiwa miguuni mwake.. Na changamoto kubwa kwa wachezaji wa timu pinzani ilikua wanamdhibiti vipi Boban.. hivyo wakawa wanaishia kupokea kadi kama njugu.
4. Haruna alikua na mawazo ya ziada ya kujua wenzie wanawaza nini na hivyo kufanya kama wanavyotarajia. Kwa upande wa pili wa shilingi.
Haruna alikua akitofautiana mara chache na wenzake uwanjani.. na hii ilitokana na wenzake kushindwa kumuelewa anataka nini uwanjani [nadhani hii ni kutokana na kuwa dk. 3 mbele].
Japo nafahamu, Jua linaelekea kuzama kwa upande wa Haruna Moshi Boban.. Namtakia kila ya heri, yeye na timu yake ya Friends Rangers iweze kupanda daraja msimu ujao.. Ili tuweze kumshudia tena Living Legend huyu.
Long Live..
The Living Legend...
Haruna Moshi Boban.