Nimemeza pin imenikwama kooni nifanyeje

OME123

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
1,498
605
Wanajamvini naomba msaada wenu kuna siku nilikuwa nachokonoa meno na stepple ikawa kipande cha stepple pin likavunjika nikaimeza imenikwama kooni napata maimivu makali sana nifanyeje ni wiki ya pili sasa maumivu yananitesa nombeeni msaada ndugu
 
kwanza wahi hospitali kwani inashangaza kumeza pin na kukaa nayo kwa wiki 2 bila kupata ushauri wa dokta.
pia huu ni uwanja wa siasa so post kwa JF doctor
 
Nenda hospitali, na binadamu anatumiaje vyuma wakati kuna tooth pick? Au ulikuwa unatumia vifaa vya ofisini isivyo ili userve? hahahahahaaaa kaaazi kwelikweliiiiiiiiiiiiii
 
Subiri itaoza!!!Kwa wiki mbili unayo na unaandika thread mstarehe??Wai hsptl kwani ikifika katika utumbo then ikasukumwa na chakula bahati mbaya utumbo ukakwaruzika matatizo yake yatakuwa makubwa kuliko uliyo nayo sasa!!
 
JF doctor ndio pahala pa hiyo thread...otherwise pole na hapo ni kuwai hospital............
 
Mazee ume 'bahatika' mpaka kuwa na access ya internet lakini unachokonoa meno kwa pini?Pini imekwama kooni kwa wiki 2 nzima,na wala hushtuki na kwenda hospitali?

Sasa kama wewe ambaye naamini ni among 'the middle class' or even 'upper-middle' wa nchi hii,huoni umuhimu wa kuchukua hatua za haraka unapopatwa na tatizo la kiafya linaloweza kukusababishia tatizo kubwa zaidi baadaye,vipi kuhusu ndugu zetu wengi wanaoishi vijijini?Unataka koo livimbe,litengeneza usaha,lizibe na ushindwe hata kula,halafu uende ukamsumbue babu-loliondo?
Fanya hima uende hospitali bro!
 
Nenda hospitali, na binadamu anatumiaje vyuma wakati kuna tooth pick? Au ulikuwa unatumia vifaa vya ofisini isivyo ili userve? hahahahahaaaa kaaazi kwelikweliiiiiiiiiiiiii

hahahaaaaa mishahara hii!
 
Wanajamvini naomba msaada wenu kuna siku nilikuwa nachokonoa meno na stepple ikawa kipande cha stepple pin likavunjika nikaimeza imenikwama kooni napata maimivu makali sana nifanyeje ni wiki ya pili sasa maumivu yananitesa nombeeni msaada ndugu

horror tale

peleka jukwaa la jf doctor
 
Labda hamaanishi pini tunayoijua sisi, anatumia lugha ya picha ndo maana analeta hoja kwenye jukwaa hili.
 
Sasa tunaionea JF! Kweli ndugu yangu mtu mzima umekwama na pini kooni kwa wiki 2 sasa bado unakuja kuuliza JF ufanyeje??? Tuiache JF kwa ajili ya mambo makubwa zaidi na haya ambayo ni personal issue tunazoweza ku-solve wenyewe, tufanye hicyo! Kha!
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom