Nimeletewa mchumba na wazazi wangu, nimemzidi miaka 14

Mwanamke hana umri Africa,maadam anazidi miaka 18 anafaa tunaangalia akili tu
 
Nataka kuoa wadau ila binti walionilitea wazazi wangu namzidi 14 years...naona kama ni gap kubwa sana.

Naombeni ushauri.
nini 14,watu wanapishana hadi 30 na life inakwenda,la muhimu ni maelewano tu.na kubwa zaidi kama wewe mwenyewe umeridhika naye
 
Hapo cha kuwa makini nacho ni tabia walau na background yake. Habari za miaka achana nazo maana wewe huend kuishi na miaka. Utaishi na characters tu.

Kuna wengine wanaishi na wenza wao ambao umri unaendana lakini maisha wanayoishi Mungu anajua
 
Ke kumzidi me kwa miaka 14 si kawaida kwakua kikawaida me ndiye anayetakiwa kumzidi me kimiaka.
 
Kwani mzee machache kamzidi miaka mingapi yule binti...??
Au kwa kuwa yeye hakuletewa kama wewe....??

Kwani mzee Mugabe amemzidi miaka mingapi...mama Grace Mugabe.....??

Mwanamme hazeeki bali anaongezeka umri....mwanamke mwenye umri wa miaka 28 akisimama na kijana wa kiume mwenye umri huo ni kama mtu na mama yake mdogo.....
 
Age ain't nothing but a number!! Ila unatakiwa uwe mbunifu maana ukizembea kidogo tu lazima ugongewe
 
Wee jamaa humpendi huyo mwanamke na unatafuta sababu.

Wazazi wamekosea kukutafutia mke ila utakosea zaidi kama utamuoa huku humpendi.
 
Back
Top Bottom