Nimelazimishwa kutumia jina la ukoo

sekulu

JF-Expert Member
Jan 17, 2011
988
157
Nimeenda hospitali moja huku Kaskazini, nilipoambiwa kutaja jina langu nikawatajia majina mawili ambayo yanatokeaga ktk oficial documents zangu zote. Wakanambia wanataka majina matatu na ni lazima kitu ambacho sijazoea, nimebaki kujiuliza ni kwa nini ilikua lazima.
Na je lina faida gani?
 
Haaa! Ngoja tu niheshimu maoni yako. Sasa wewe umeona nini cha ajabu? Haujui kama jina la ukoo ndilo linalokufanya uweze kutambulika kwa urahisi?
 
Jina la tatu muhimu sana kwa sababu majina mawili tu hayawezi kukupambanua na watu wengine manake wapo akina Emmanuel Massawe wengi sana lakini tukisema Emmanuel Joseph Massawe hii inawapambanua akina Emmanuel Massawe waliobakia, ni mfumo rasmi na muhimu kabisa au ulifikiri kuna chembe za ubaguzi/ukabila/ukoo?
 
hataki ajulikane mtu wa wapi huyu jamaa. ndo wale wale akina richard john unadhani mzungu ukikutana naye au ukiongea nae kwenye simu utasikia nyela kamweneeeee! taja jina la ukoo mzee
 
Jaribu ku-Google majina yako hayo mawili harafu utaona kama kuna wengine wanayatumia hayo? Kama ndio, basi utaelewa maana yake!
 
Dah, Sikatai kujulikana natokea wapi, Nadhani nimeeleweka vibaya


Je kwani ni Lazima Kutumia Majina Matatu?
 
hataki ajulikane mtu wa wapi huyu jamaa. ndo wale wale akina richard john unadhani mzungu ukikutana naye au ukiongea nae kwenye simu utasikia nyela kamweneeeee! taja jina la ukoo mzee
Mnogage....madzengo! Teh teh teh umenifurahisha sana mkuu
 
Taja majina yako! Hata Yosefu baba mlezi Wa Yesu Kristu alikuwa na kwao na ndiyo maana alifunga safari toka Nazareth kwenda Bethlehem kwenye mji Wa Daudi kwenda kuhesabiwa kwa amri ya Kaisari Augustus. Isingekuwa hivyo angehesabiwa palepale Nazareth alipokuwa anafanya shughuli zake za Useremala na pengine Yesu Kristo angezaliwa palepale Nazareth na siyo Bethlehem. Kwa hiyo identity ya jina au kabila siyo ku promote ukabila bali ni kuonyesha roots
 
Back
Top Bottom