Nimekuzimia Ewe Mtoto Malaika wa JF

Digaller

JF-Expert Member
Oct 20, 2009
745
427
Wakuu heshima mbele,

Katika pitapita yangu leo hapa jukwaani nimekutana na mtu mmoja ambaye mtima wangu umemzimia sana,
Ni mrembo mwenye sura nzuri, macho ya kuvutia na kifua ambacho mwanaume yeyote rijali kama mimi lazima atavutiwa na umbo la huyu binti.
Ukiiangalia avatar yake waweza dhani kama anakuangalia wewe au anakuita wewe ila ukweli ni pozi tu hilo.
Sijaona kama yeye hapa JF, kwakweli ni mzuri, mtamu zaidi ya asali, nahitaji ugali bila mboga kwani awapo yeye kwangu ni mboga iliyo kamilika.
Sintoacha kumsifia kwakuwa hata mmoja hapa JF hajafikia uzuri wa huyu mrembo, Khaki ya nani mungu alimuumba huyu siku ya jumamosi tena alikuwa wa mwisho kabla hajaenda kupumzika.
Popote ulipo, Popote usikiapo sauti hii, Popote uwazapo uwepo wangu na vyovyote unichukuliavyo tambua Nimekuzimia binti mrembo, Hakika hata nikipewa chopper bado ili mtima wangu uache kukuwaza wewe sintoweza.

Namzungumzia huyu hapa;


user-online.png
Feis Buku

avatar52988_2.gif


JF Senior Expert Member
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png


Karibu kwangu Mtoto malaika......!!! Upate tulizo la Mtima wako........!!!!



 
Ha ha FB hebu njoo haraka unatafutwa sana

Dena nazimia sana kwa msaada wako ambao huwa unautoa kwa member hapa jamvini, Plz popote umwonapo mwambie huku namsubiria kwa hamu sana, Natumaini yeye ndo atakuwa kila kitu kwangu, Shibe wakati wa njaa na amani wakati wa mateso.
 
Huyo dume huyo shauri yako ata kucameroon we cheka cheka nae

Hahahahaahaaahahahahahaahah!!! Wewe una ushahidi gani kama ni dume?????? Hata kama ni Dume yawezekana hiyo avatar hapo ni ya dadake kwahiyo nitamuomba anipe namba ya simu ya dadake ili nijijengee mwenyewe. Hakuna kilichoharibika!!
 


Hahahahaahaaahahahahahaahah!!! Wewe una ushahidi gani kama ni dume?????? Hata kama ni Dume yawezekana hiyo avatar hapo ni ya dadake kwahiyo nitamuomba anipe namba ya simu ya dadake ili nijijengee mwenyewe. Hakuna kilichoharibika!!

Mimi nakwambia kijana umeingia kichwa kichwa usichanganywe na avatar hiyo hapo hamna kitu.
 
Makubwa!
Vidude vya PM kwako vinagoma nini?

Mkuu upendo haufichwi, Ukiona unaficha upendo hujue hapo kuna walakini, Upendo huonyeshwa hadharani ili jamii ijue kuwa mwapendana. Nimemzimia na kumfia Feis Buku kwahiyo sina haja ya kuficha upendo wangu. Wapendanao always huwa wanaita watu na kufunga ndoa ndo maana nimesema hadharani kuwa nampenda sana ili wewe ujue usije tuma PM na wewe kuomba makazi.
 
Amelogwa na avatar lakini kumbuka (huyo ni wifi yako)

Kama si yeye basi huyu lazima atakuwa na Dadake, Mkuu huoni sura ya kibantu hiyo hapo??? Huyu ni wa hapahapa Tz, Usinikatishe tamaa, Nataka kuweka makazi ya kudumu hapo.
 
Huyu anitakii mema kabisa, yawezekana na yeye katuma PM hajajibiwa ndo maana ananikatisha tamaa mapema.

Atakavyo kucameroon usije kulalamika hapa watu wanatumia majina ya kike kumbe wao wanaume
 
Mamito feis watafutwa huku njoo uoke jahazi la Gbollin linazama jama, mwenzio hajiwezi juu fanya uje utulize mwenzio!
Usijali mkuu kwa sauti hizi zote ataibuka soon na we roho yako itapona lol!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom