Nimekuta chupi ya mke wangu chumbani kwa mdogo wangu wa kiume

Kwani mkeo akifua chupi zake huwa anazianika wapi? Nimejifunza kuepuka kufikia hitimisho bila kufanya utafiti wa kutosha. Jitahidi ushahidi wako usiwe ni wa kuacha mashaka.

Njia nzuri ingalikuwa kumuuliza mkeo hiyo chupi unayoiona kwa mdogo wako kama ni ya kwake na kama ndio imefikaje huko? Kunaweza kuwa na maelezo mazuri tu yanayoeleweka. Cha muhimu sikiliza.
 
Some guys are making jokes on a serious issue! Be calm ..Fanya uchunguzi kwanza utajua tu

Uchunguzi wa nini? kwani anataka uthibisho kwamba dogo kalia vyake, hapa ni kuonya isijirudie kama imeshatokea, mke haachwi kwa hilo tu, wala hahukumiwi kwa hilo bali huonywa asirudie, atakaporudia ndio hapo sasa mengine yafuate.
 
Jamani Leo ni Siku ya saba tangia nikute chupi ya mke wangu chumbani kwa mdogo wangu wa kiume. Nimekaa nalo moyoni naona niwashikirikishe wenzangu nione mnishauri nini.

Ni hivi, ninaishi na mke wangu mwaka wa nne sasa, tuna mtoto mmoja, nina Mdogo wangu anaishi hapa tangia January niliponunua bajaj ili awe anaendesha ili kusaidia wazazi wetu nyumbani kijijini.

Sasa jumapili iliyopita wife aliwahi sana asubuhi kwenda kanisani pamoja na mtoto, Mimi nilibaki nimejilaza mpaka kama SAA moja na nusu Hivi, nilivyokumbuka kuwa nilikuwa na Ahadi Fulani, katika kufanya maandalizi sikiweza kuiona pass, so nikaenda straight chumbani kwa dogo katika kuitafuta ndo nilipokutana na chupi ya mke wangu ambayo Mimi mwenyewe nilimununulia so imechoka choka kiasi chake.

Nilishikwa na butwaa kwani namwamini sana wife, dogo mwenyewe heshima kwa sana, ilichukua simu na kupiga picha kadha na kuzificha kwenye private vault, ile chupi nikaiacha palepale.

Wife hajasema chochote mpaka sasa, nawaza namna ya kuanza kumuulizia japo ameshahisi kuwa siko normal, coz nikimuona usoni nakuta hasira imepanda sana.

Kwa kifupi naogopa ukweli kuwa mke wangu amenisaliti kwa mdogo wangu, mpaka sasa simuoni kama mke wangu tena, namuona kama bundi kajificha chumbani kwangu.

Naomba mnishauri kwani Mimi kwa haraka haraka naona nimwite kaka yake aje amchukue kabla sijamfanya kitu mbaya, tatizo hasira zangu hupanda pole pole sana, kuzishusha ni kazi sana.
Mkuu wangu hebu tuliza hasira kwanza. Inawezekana wakati wife anaanua nguo alijikuta ameichanganya kwenye nguo za dogo, na kwa kuwa dogo ni full heshima, amebaki ameduwaa asijue la kufanya. Hebu muulize wife kwanza hiyo kitu imefikaje kwa dogo kama asipotoa majibu mujarab ndipo ufanye maamuzi mengine.
 
Lakini mkuu jiridhishe kama kweli hiyo chupi ndiyo ile ya wife au la. Inawezekana dogo aliingiza mchepuko uliokuwa na chupi inayofanana na ya wife na kisha akaisahau huko. Usichukulie haya mambo kirahisi na kwa mihemko...tuliza akili kwanza. Najua unafahamu mahali wife anatunza chupi zake...isake kwanza hiyo chupi isipopatikana ndipo umuulize wife mahali ilipo na ilifikaje huko.
 
Hivi unamuacha mwanamke kwa jambo jepesi km hilo!??? Kuhisi tu!!! Hapana, kwan wewe hujawahi kumsaliti??? Tuliza mawazo fanya uchunguzi na hata ukigundua mtimue mdogo wako then ndoa iendelee

Yaani mdogo wake amtimue ajili ya mke? mke atapata mwingine, mdogo wake atampata wapi mwingine? udugu haufi mke anaachwa.
 
Hayo mambo yanatokea sana siku hizi. Wanandoa wanatembea na ndugu wa karibu wa mke au mume. Hata watoto wanaozaliwa wengi ni wa ndugu wa karibu wa mume. Ila yanaleta madhara kijamii. Nashauri tafuta sababu ya kumuondoa mdogo wako hapo nyumbani. Halafu tafuta mtu mzima ambaye unamheshimu au mchungaji/padri mzee utafute ushauri wa karibu kuhusu mke wako. Kama una hasira sana basi bora tafuta sababu ya kuwa mbali nae kwa muda usije ukaleta madhara.
 
Sijaingia tena,kuna kila dalili kuwa wife anajua kuwa najua
Kama wife keshajuwa kuwa umejuwa basi hapo si salama. Kama angekuwa panya ndo kapeleka wala wife asingekuwa na fikra yoyote juu ya hilo jambo na angekuwa wa kwanza kukuhoji kwa nini hauko sawa na angekuuliza mara kwa mara maana ni mkeo. Ila kama ana waswasi ni hatari. Pili kumuuliza mdogo wako jambo hilo ni kujidharaulisha yaani una muuliza mdogo wako eti unagegeda shemeji yako? Noma. Sijui mambo mengine magumu.
 
mkuu ni hivi inawezekana mke hajachepuka kabisa, tatizo ni Huyo dogo kachkua chupi ya mke wako avutie hisia inawezekana anampenda sana mke wako,na anashindwa cha kufanya akaamua achkue chupi akaenayo, ainusenuse, angalau apate mzuka baada ya hapo akimbilie bathroom

juzi tu hapa niliskia kwenye radio dogo mmoja hivi kaanza kubarehe na ajui aganyaje, akachkua chupo ya Dada yake akawa ananusa then anakimbilia bathroom kujikamua


so brother don't be nervous kuhusu mke wako huyoo dogoo huyooo
 
Uskute dogo wako anaifanyia kupigia nyeto...sometimes mawazo mabaya hayakusaidii kama vipi tafuta ki camera cha siri weko korido na sebuleni kisha usabye safari ya siku mbili ukirudi utapata majibu kupitia hizo camera.
Watu hatuna mapenzi ya dhati japo ikitokea mdogo wako amekula inabidi umuonyee na ukaushee kibingwa tu.
 
Kwahiyo unaona alichokifanya mdogo mtu ni sahihi?
Wote (mke na mdogo mtu) hawafai

kwanini hawafai wakati wakikanywa wataacha na haitojirudia? japo walichokifanya si sahihi hata kidogo kama kweli wamekifanya maana bado ushahidi haupo, chupi kaichukua dogo anaivaa ajili hana chupi za kutosha.
 
Back
Top Bottom