Nimekudondokea sana Halima Mdee!

Status
Not open for further replies.

mayenga

JF-Expert Member
Sep 6, 2009
4,118
1,966
Mheshimiwa sana,

Pole na Majukumu.

Kawaida ya binadamu makini na mahiri ni kuthubutu kufanya kile anachoamini ni sahihi.Kuikweli mtazamo wangu kuhusu wewe Mheshimiwa ingawa ni wa kiharakati lakini upande wa pili wa shilingi ni kwamba unaniacha hoi sana.Huwa najiuliza kwanini hisia zangu kwako hazikomi lakini sijui ila inatosha kusema kuwa nimekudondokea.

Ndoto zangu niziotazo kwako ni kwamba nikibahatika kukubaliwa ombi langu ,mtoto wetu wa kwanza atasoma shule za kata lakini zilizoboreka,kwani hata kama sisi tukishindwa mtoto huyu kwa harakati zake hatakubali kukalia mawe au kusomea chini ya mti.Ndoto hii haikomei hapo,inaendelea kueleza kuwa utakuwa mama wa mfano wa kuigwa ukiwa nami.Kwa uchunguzi wangu wa haraka inaonesha tuko fani moja,ubishi na harakati hazitaishia mjengoni bali hata nyumbani,utadai haki unayostahili na utapewa.

Juhudi zangu za kukupata na kukutana nawe live zimegonga mwamba,inaonekana wengi wao hasa ambao nimejaribu kuwaeleza wanipatie contacts zako walinibania,nadhani lengo lao ni kama langu lakini wenyewe ni midomo zege hawawezi kuongea na kujieleza.Mheshimiwa nina uhakika hautaniacha kwenye foleni,kiukweli nimekudondokea!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Maombi yako nina wasiwasi nayo, inabidi yaundiwe tume isije ikawa unataka kupata tu umaarufu kupitia kweke, au uliposikia wamepewa mil. 90 za magari udenda unakutoka.
 
hahahaaa yani ili jukwaa lina mambo kweli
aya kila la heri namba yake kuipata cjui
kwann km kiukweli umedondoka ivo,usiende dodoma?
 
nimeukumbuka ule wimbo wa 20% .....'tamaa mbaya'!
 
Kitendo cha kumwambia umemdondokea basi inaonesha kabisa kuwa huna uwezo wa kuwa nae kwa mchanganuo uliotupa hapa,kwani maneno yako yanaonesha tayari umedondoka kwake na utakuwa tayari kuwa chini yake.
Ukipata nafasi ya kumpata basi tujuze tukupe hongera.
 
Hivi bwana mkubwa upo serious mbona unanitisha lakini jaribu yasiishie humu we mtegee akiwa kwenye shughuli zake za kawaida kisha itoe kauli yako
 
sikiliza njoo Kinondoni B mt ufipa 32. Makao makao makuu ya cdm. mh. Huyu anakuja mara kwa mara kwa shughuli za kichama.bt kwa sasa wapo mjengoni.
 
jaribuni kumuelewa mleta mada...amefikisha ujumbe ambao wengi hamjaelewa ila mnakimbilia kudhani ni yale
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom