Nimekua msomaji hapa kwa muda ila nimetia timu kabisa

Mheshimiwa sana mama Parliament,karibu sana jamvini, kwetu tunasema 'gijemu' na wewe unaitikia 'waitu shangwage'.
 
Karibu saaaana,ila achana na wale wenye majungu sijui JF inatumiwa sijui nini,karibu uone mwenyewe!
 
Wakuu wa JF,

Nimekua msomaji hapa mda mrefu na hasa kwenye siasa ila nimeamua kuingia rasmi kwa kuvutiwa na hoja kadhaa.Hata hivyo sitawaeleza chama changu ni kipi ili niwe na mawazo huru.Hili jukwaa la mapenzi/uhusiano na Urafiki huwa nalihusudu sana.Tuwe pamoja jamani
Tutajua itikadi ya chama chako utakapochangia kwa uhuru!
 
Ushakaribishwa sana, umeshazoea sasa, huu ukumbi ni wako mwongozo soma masharti ya JF, longolongo na story za kutunga hazina nafasi hapa, anza kazi
 
Mh mbona jina na avatar vina kataliana au uko chama ambacho hubalansi kazi na starehe kua na uzito sawa?

Karibu.
 
Ushakaribishwa sana, umeshazoea sasa, huu ukumbi ni wako mwongozo soma masharti ya JF, longolongo na story za kutunga hazina nafasi hapa, anza kazi



Kabla hajaenda huko atoe walau thanks basi kukaribisha kote huku bado yuko kimya.
 
karibu sana msafiri,pole na uchovu wa safari
za utokako utupe habari,taratibu usilete shari
MMU kama bahari ,kuna kanuni usivuke mstari
najua hauna kiburi,karibu ufaidi yetu mazuri.



wallah NIMEKUTAMANI WEYE BINTI!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom