Nimekosea ? Nipo sahihi? Please help-shukrani kwa wanajamii

mimi ai

Member
Apr 2, 2012
89
30
kuna siku nilipost hapa kuomba ushauri kuhusu mahusiano yasiyo rasmi niliyotaka kuyaanzisha na bwana mmoja hivi ilisomeka hivi in red
Nimekosea ? Nipo sahihi? Please help
Since nimeona ni ngumu kupata the perfect man to stay with for serias relationship. Nimedecide kuwa na mwanaume mmoja hivi kutoana upweke na kukidhi tamaa zetu za kimwili.
Ni mume wa mtu but yupo available....(divorced partialy)
ni rafiki yangu kwa muda mrefu ni mzuri sana. To me its better this way
hatuna commitment towards each other tupo tu kupeana raha.
Sijali kuhusu future cause future huwa siioni naishia tu kuumia
nimekosea? nashukuruni kwa ushauri mlionipa,
nilisitisha mahusiano na yule bwana ingawaje alisikitika sana.kwa sasa ndio nipo alone but najisikia vizuri sana na Mungu ananibariki mno.namshukuru mungu kwa kunipa akili na uzuri hili nitawaeleza siku nyingine
 
Hongera sana kwa kufanya maamuzi magumu. Mungu azidi kukupigania, ipo siku mambo yatakuwa kwenye mstari
 
Mungu aendelee kukubariki kwa kuchukua uamuzi mzuri wa kuachana na mume wa mtu. Endelea kumtumikia na kumtumainia Mungu kwani yeye ndo anajua ni yupi aliyekutayarishia ili awe wako wa milele.
 
Hongera kwa kuachana na uzinzi, cha kufanya sasa mtafute na kumjua Mungu wa kweli na baada ya hapo mwombe akupe wa kwako ili uepuke mtego wa uzinzi na uasherati. Nakutakia maisha mema
 
wanaume waliooa ni wazuri kwa wanawake walioolewa, inakuwa ni kukidhi kiu zenu tu halafu kila mtu anajiendea kwa mke/mumewe... kwa nyie ambao hamjaolewa tafuteni wa kuwao tu vinginevyo mtaishiaga kuumia roho tu
 
kuna siku nilipost hapa kuomba ushauri kuhusu mahusiano yasiyo rasmi niliyotaka kuyaanzisha na bwana mmoja hivi ilisomeka hivi in red

BWANA MMOJA OR MUME WA MTU??bora ,maana ulivyooandika ,ni rafiki wa mda mrefu,inaonyesha wewe ndiye uliyechangia kuvuruga ndoa yao,kama ni wewe ninayekufahamu,kwa ulivyoondika maelezo yako,basi wamesharudiana,alichokiunganisha MUNGU KAMWE USIKITENGANISHE,SUBIRI NA WEWE KULIPWA YOTE ULIYOYAFANYA,VITA NI WEWE NA MUNGU,USICHEZE NA NDOA ZA WATU ,WAWEZA WEHUKA SIKU MOJA,ULIZA WENZIO WALIOIBA WAUME ZA WATU.POLE.
 
Huyu Mungu jamani atatia akili. Yaani anakubariki kwa kuzini na mume wa mwenzio ambae hawajaachana officially? Huyo mama akikufumania ugoni uje hapa tumlaani huyo Mungu wako. Unajizibia baraka bureeee
 
kweli kabisa King'asti,Yaani bora mmi ai ukamuomba msamaha huyo uliyemwibia mume, maana hujamtendea haki kwa kweli.
 
Ulikosea ila madhali umeachana naye basi umefanya jambo jema sana.

Sasa ni kuhakiki hutorudia tena hilo kosa.
 
Hongera, utampata wa kwako atakayekufaa kwa wakati usiodhania. Usichoke kumuomba Mungu wako.
 
kuna siku nilipost hapa kuomba ushauri kuhusu mahusiano yasiyo rasmi niliyotaka kuyaanzisha na bwana mmoja hivi ilisomeka hivi in red

BWANA MMOJA OR MUME WA MTU??bora ,maana ulivyooandika ,ni rafiki wa mda mrefu,inaonyesha wewe ndiye uliyechangia kuvuruga ndoa yao,kama ni wewe ninayekufahamu,kwa ulivyoondika maelezo yako,basi wamesharudiana,alichokiunganisha MUNGU KAMWE USIKITENGANISHE,SUBIRI NA WEWE KULIPWA YOTE ULIYOYAFANYA,VITA NI WEWE NA MUNGU,USICHEZE NA NDOA ZA WATU ,WAWEZA WEHUKA SIKU MOJA,ULIZA WENZIO WALIOIBA WAUME ZA WATU.POLE.
urafiki wetu ulianza tayari walishaachana.wala sikuwai kumjua huyo mama.hata sasa hivi hana mke.hata ningependa anioe angenioa.mimi tu sikumpenda
 
Huyu Mungu jamani atatia akili. Yaani anakubariki kwa kuzini na mume wa mwenzio ambae hawajaachana officially? Huyo mama akikufumania ugoni uje hapa tumlaani huyo Mungu wako. Unajizibia baraka bureeee
hawajaachana officially lakini wameachana tena huyo mama kaolewa
 
kuna kitu nahisi nikashindwa kukielewa hapa, unamzungumzia Mungu muumba wa vitu vyote? au mungu mwingine tu?
 
urafiki wetu ulianza tayari walishaachana.wala sikuwai kumjua huyo mama.hata sasa hivi hana mke.hata ningependa anioe angenioa.mimi tu sikumpenda

sasa mbona hueleweki,mwanzo kabisa wa post zako ,ulisema ni rafiki wa mda mrefu,hapa tena wasema ulianza walishaachana,kumbuka ulisema ni mwaka tu ndio wametengena,wewe UNAMATATIZO MAKUBWA HUJIJUI,ETI NINGEPENDA ANIOE ANGENIOA ,KUMBUKA ULISEMA MKO KWA SIRI,SASA SIKIA HAKUNA SIRI,TUMESHAKUJUA SIKU NYINGI WE ENDELEA TU KUWA NAYE....NA KUVURUGA NDOA ZA WATU MPAKA UTAKAPOCHOKA,KILA LA KHERI NA WAUME ZA WATU.
 
Nahsi kama sijaelewa. Eitheir kwa ukilaza wangu au mhusika anadanganya au kuchanganya mambo.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
hawajaachana officially lakini wameachana tena huyo mama kaolewa

mhhh mara kamfumania hamtaki tena,leo huyo mke mwenzio kaolewa... jana hawajaachana officially,kesho wameaachana tena,keshokutwa sijui itakuwaje .....duuu haueleweki.....embu mimi ai kajipange tena ,nahisi unaongea uongo hapa????
 
sasa mbona hueleweki,mwanzo kabisa wa post zako ,ulisema ni rafiki wa mda mrefu,hapa tena wasema ulianza walishaachana,kumbuka ulisema ni mwaka tu ndio wametengena,wewe UNAMATATIZO MAKUBWA HUJIJUI,ETI NINGEPENDA ANIOE ANGENIOA ,KUMBUKA ULISEMA MKO KWA SIRI,SASA SIKIA HAKUNA SIRI,TUMESHAKUJUA SIKU NYINGI WE ENDELEA TU KUWA NAYE....NA KUVURUGA NDOA ZA WATU MPAKA UTAKAPOCHOKA,KILA LA KHERI NA WAUME ZA WATU.
huelewi nini? watu kibao wameachana na wake zao wakaoa tenambona mandela alioa mkewe alikuwa amekufa?talaka huwa ni za nini
 
mhhh mara kamfumania hamtaki tena,leo huyo mke mwenzio kaolewa... jana hawajaachana officially,kesho wameaachana tena,keshokutwa sijui itakuwaje .....duuu haueleweki.....embu mimi ai kajipange tena ,nahisi unaongea uongo hapa????
ukweli ndo huo usibishane na taarifa ya habari hutoshinda
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom