Nimekipata Kigori,wenye wivu jinyongeni,

Si utani NJ, hawa wawili wata make a wonderful couple ha ha haaaa.. :car:


sipo la kuukanusha,ila napinga uamuzi,
elia umeamusha,nguli jabali ye uzi,
samora ndo kakausha,kumalizia matanuzi,
Mimi jamani ninae,lazizi wangu Kigori,

kama mwataka ye judi,binti misi awe wangu,
hiyo nafasi siinadi,fisadi adui wangu,
uzinzi kwangu sio chudi,nalaani hilo egu,
mimi jamani ninae,lazizi wangu kigori,

Ngoja nimuulize judi,mama tamko lako mali,
sema wasije maindi,nakujua we kiamili,
hata twende saudi,pitia kule somali,
Mimi jamani ninae, lazizi wangu kigori,

judi sema siogope,mi si mchakachuaji,
nisije pakwa matope,kigori pale ujiji,
mambo yawe kweupe,kama ya mwanakijiji,
Mimi jamani niane,lazizi wangu kigori,
 
Magulumangu kama uko single na Miss J yuko single kaaeni chini myamalize kiutu uzima. Na pledge 20 kwa harusi. Naona zina click kinoma.

Nguli nimekusoma, kuhusu ya kwako rai,
Jabali nimekukoma, hakika kwako sikai,
Kama deni lauma, lako katu sidai,
Magu anacho kigori, mie ningali namisi

Magu kwa sasa haoni, hata avae miwani,
Kiumbe kakosa soni, hata pawepo ubani,
Haendi japo sokoni, eti avuna chumbani,
Magu anacho kigori, mie ningali namisi

Japo ningali namisi, tuli nimeitulia,
Hata ukija mkasi, mie sichoki tulia,
Hata ajaponimisi, machozi kunililia,
Magu anacho kigori, mie ningali namisi

Kuyamaliza siwezi, lau nipate jabali,
Japo upigwe mluzi, moyo hautokubali,
Ya bure hiyo mizizi, mie katu silali,
Magu anacho kigori, mie ningali namisi
 
Nguli nimekusoma, kuhusu ya kwako rai,
Jabali nimekukoma, hakika kwako sikai,
Kama deni lauma, lako katu sidai,
Magu anacho kigori, mie ningali namisi

Magu kwa sasa haoni, hata avae miwani,
Kiumbe kakosa soni, hata pawepo ubani,
Haendi japo sokoni, eti avuna chumbani,
Magu anacho kigori, mie ningali namisi

Japo ningali namisi, tuli nimeitulia,
Hata ukija mkasi, mie sichoki tulia,
Hata ajaponimisi, machozi kunililia,
Magu anacho kigori, mie ningali namisi

Kuyamaliza siwezi, lau nipate jabali,
Japo upigwe mluzi, moyo hautokubali,
Ya bure hiyo mizizi, mie katu silali,
Magu anacho kigori, mie ningali namisi

Wote bi wamekusoma,ingawa we ni wa kale,
rohoni mwangu daima,umechoma wangu shale,
nakujua wewe mama,kamwe hutumii chale,
Ulimuona mwenyewe,kwenye harusi kigori,

usilie sana mama,jabali katoa wake wosia,
sio kutekeleza lazima,japo kaja kugusia,
natamani iwe zama,za mawe nilisikia,
Ulimuona mwenyewe,kwenye harusi kigori,

leo nashinda nae,njoo pia ujumuike,
usije kupata mwae,yeye mtoto wa kike,
tulimalize ka mdae,twende wote kwake,
Ulimuona mwenyewe,kwenye harusi kigori,
 
sipo la kuukanusha,ila napinga uamuzi,
elia umeamusha,nguli jabali ye uzi,
samora ndo kakausha,kumalizia matanuzi,
Mimi jamani ninae,lazizi wangu Kigori,

kama mwataka ye judi,binti misi awe wangu,
hiyo nafasi siinadi,fisadi adui wangu,
uzinzi kwangu sio chudi,nalaani hilo egu,
mimi jamani ninae,lazizi wangu kigori,

Ngoja nimuulize judi,mama tamko lako mali,
sema wasije maindi,nakujua we kiamili,
hata twende saudi,pitia kule somali,
Mimi jamani ninae, lazizi wangu kigori,

judi sema siogope,mi si mchakachuaji,
nisije pakwa matope,kigori pale ujiji,
mambo yawe kweupe,kama ya mwanakijiji,
Mimi jamani niane,lazizi wangu kigori,

Nimeona lako swali, nitoe yangu kauli,
Japo wajua ni-mwali, sipo kwa yako samli,
Hata walio na mali, pia hao makuli,
Malenga kwishailenga, vipi ubaki na swali?

Nguli kachokonoa, elia kaidakiza,
Samora kakuopoa, hima waanza kimbiza,
Kigori atakitoa, mie sitakupoza,
Malenga kwishailenga, vipi ubaki na swali?

Heri uende Saudi, sio kubaki ujiji,
Huko unuse uudi, pia upande bajaji,
Mjue ni nani Judi, sio ucheze alaji,
Malenga kwishailenga, vipi ubaki na swali?

Kwa wako huyo kigori, nia iwe thabiti,
Sio kuwa doridori, kila onapo matiti,
Usijerudia pori, tena bila manati,
Malenga kwishailenga, vipi ubaki na swali?
 
Miss Judi na Magulu, Thanks so much guys you have made my day..yaani nilikuwa nimechoka ajabu...Again asanteni sana jamani...This is wonderful! Mbarikiwe sana na vigori wenu!

Ila watoto wanaosoma shule za akina academy..wanakosa mengi jamani..duh!
 
Miss Judi na Magulu, Thanks so much guys you have made my day..yaani nilikuwa nimechoka ajabu...Again asanteni sana jamani...This is wonderful! Mbarikiwe sana na vigori wenu!

Ila watoto wanaosoma shule za akina academy..wanakosa mengi jamani..duh!

thanks mpendwa. mi nilikuwa natest tu kumbe nami naweza! na magulumangu pamoja na unguli wake kaishiwa kakimbia! haha
 
thanks mpendwa. mi nilikuwa natest tu kumbe nami naweza! na magulumangu pamoja na unguli wake kaishiwa kakimbia! haha

Sikujaiweka chini,kalamu ila kifungo,
judith uwe makini,ijapo huna maringo,
niko kwetu kigamboni,nisije pata kibyongo,
Kigori ma kanifunga,kifungo chenye maana,

Vipo vingi hakamani,japo kesi mbalimbali,
changu kipo asilani,japo sio cha kimbali,
maji hayako shingoni,ni kifungo cha asili,
kigori ma kanifunga,kifungo chenye maana,

Wapo wengi mafungoni,japo kutofurahia,
hawapo ulaiani,wamefungwa masilia,
kwa wizi nao uhaini,wao sio asilia,
Kigori ma kanifunga,kifungo chenye maana,

nafurahia kifungo,japo uhuru ninao,
silitoi langu fungo,pingu iso liwalao,
usiwe ka kibunango,wajinga ndo waliwao,
Kigori ma kanifunga,kifungo chenye maana,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom