Nimekataa posa ya Myao kwa mpwa wangu…………………!

Mama Ngina alinidokeza kuwa kuna siku alimsikia akizungumza na huyo Mhyao wake kwa simu akiwa nyuma ya nyumba na inaonekana walikuwa wanapanga mikakati fulani..............kitu alichosikia ni kama vile anataka kufunguliwa biashara ya Saloon ya kike sijui ili kumuwezesha...............nasubiri hilo litokee, kama sijamuachisha shule na kumrudisha kijijini................yaani najuta kumleta mjini.......
lol.... usijute mtambuzi, ww timiza wajibu wako tu na umpige vita haswaa atakusoma tuu.
 
mimi niko makini, hata hawa wnangu kina ngina unafikiri wataolewa tu na mijianaume isiyo na malengo.............lazima niwa -interview kwanza na kama hawana tembo card..........posa haipokelewi
dahhh! Nimeamua ww ukue baba angu wa ubatizo niliekua nae namtupilia mmbali!!!
 
Huya muoaji anafanya kazi gani? Na umemuuliza anataka kumuacha huyo mwanamke wa kwanza kwa kosa gani?
 
Heshima mbele mkuu,
hii inaonyesha kuwa binti yako tayari
alishaanza kuvunja amri za Bwana na huyo mkweo mtarajiwa,
Je itakuwa rahisi kuwatenganisha kweli mkuu,
kuna hatari ya kupata tena kajukuu kapili.
 
Huya muoaji anafanya kazi gani? Na umemuuliza anataka kumuacha huyo mwanamke wa kwanza kwa kosa gani?
Mpwa anadai jamaa ni mfanyabiashara lakini hajui ni biashara gani anafanya. Na sababu anayodai ya kumuacha huyo mwanamke anayeishi naye kinyumba eti ni mbinafsi na hajishughulishi katika kujiongezea kipato, na sababu lukuki tu zisizo na msingi................
 
Heshima mbele mkuu,
hii inaonyesha kuwa binti yako tayari
alishaanza kuvunja amri za Bwana na huyo mkweo mtarajiwa,
Je itakuwa rahisi kuwatenganisha kweli mkuu,
kuna hatari ya kupata tena kajukuu kapili.
Hebu nikumbushe kajukuu ka kwanza ni kapi hako................LOL

Kuvunja hiyo amri walishavunja kitambo maana mama Ngina anajua mengi, lakini nimemtuma mke wangu na mama yangu mdogo anayeishi huko Tambuka Reli wazungumze naye na wamweleze tatizo analolipalilia halitamsaidia na litamletea maumivu makubwa huko mbeleni. Mtu kweli aishi na mwanamke miaka sita na watoto juu, hata kama hawajafunga ndoa, halafu anakwambie atakuoa na kumuacha huyo mwanamke................Miaka yote sita aliyokuwa akiishi naye hakuziona hizo kasoro, azione leo baada ya kukuona wewe umependeza kwa Carolight.....................! Anachekesha kwa kweli
 
Mama Ngina alinidokeza kuwa kuna siku alimsikia akizungumza na huyo Mhyao wake kwa simu akiwa nyuma ya nyumba na inaonekana walikuwa wanapanga mikakati fulani..............kitu alichosikia ni kama vile anataka kufunguliwa biashara ya Saloon ya kike sijui ili kumuwezesha...............nasubiri hilo litokee, kama sijamuachisha shule na kumrudisha kijijini................yaani najuta kumleta mjini.......

Yaani akikuzingua mrudishe tu,! we mbona ulirudishwa kijijini , na majeraha juu bahada ya kuwaambia dada za watu eti "wauzaji si wanajulikana".
 
Hebu nikumbushe kajukuu ka kwanza ni kapi hako................LOL

"Ingawa alifaulu kwenda sekondari ya serikali wakati huo, lakini aliishia kidato cha pili baada ya kumimbishwa na mkware mmoja".
 
Mpwa anadai jamaa ni mfanyabiashara lakini hajui ni biashara gani anafanya. Na sababu anayodai ya kumuacha huyo mwanamke anayeishi naye kinyumba eti ni mbinafsi na hajishughulishi katika kujiongezea kipato, na sababu lukuki tu zisizo na msingi................
Alafu siku hizi mambo ya uwazi na ukweli, Hakuna kuficha ficha mnaweza kumtumbukiza mwanenu kwa jambazi au mzungu wa unga akawa mjane kabla ya siku alafu shida ikarudi kwenu wazazi.
Kama ni mfanyabiashara ijulikane ni biashara gani na wapi, kama mfanyakazi ni kazi gani na wapi? Haijalishi hata kama ya kuuza kahawa lakini iwe inamuingizia kipato halali. kushney.
 
Yaani akikuzingua mrudishe tu,! we mbona ulirudishwa kijijini , na majeraha juu bahada ya kuwaambia dada za watu eti "wauzaji si wanajulikana".
zamani enzi ya mabasi ya TTBS ilikuwa rahisi kurudishwa kijijini, lakini siku hizi mtu anakutorokea Ubungo na kesho utasikia anaishi Kwa Mtogole kapangiwa chumba.............................
 
Usikubali kabisaa,kwanza mwambie asome kwa bidii...nimechukizwa na hao mashangazi wanaotaka binti yao aolewe na mtu anayeishi na mwanamke tayari na mwenye watoto nae.....itakuwa ngumu kwa huyo binti sana. Mkuu,usikubali kabisa,binti asome kwa sasa!
 
Duuuuu, maamuzi sahihi ila hapo kuna kila dalili ya mimba nyingine toka kwa hicho kidume feki chake. usiishie hapo, endelea kutoa darasa ili akili imrudie huyo mwanao kaka. Vinginevyo unaweza ukajikuta 'umezalisha' mtoto mwingine hapo hapo kwako, na ndo hali itakuwa mbaya zaidi. Si unajua mashangazi hawatachelewa kudai eti umemzibia riziki huyo mpwa wako...........

Ni hayo tu mkuu!
 
Mkwanja kwa aunt, saloon kwa mpwa aka wife (kishakuwa mke huyo-jamaa kamaliza kila kitu) mhusika mwenye yupo interested, lazima uzungukwe tu! Angalia atamimbishwa tena.
 
Hongera maana hapo unamtengenezea binti maisha bora sasa sijui kama yeye analielewa hilo. Ila kama ni binti mwelewa hatakuwa tayari kukimbilia. Mimi pia niliwahi chukua ndugu walivyoanza tu kumtafutia mchumba nikapata taarifa, nikamwambia binti naomba uchague kwenda kuolewa au kusoma nisipoteze hela.Binti akachagua shule sasa anakazi yake mchumba mwenyewe sijui alikwenda wapi kaja olewa na mwingine kabisa.
 
Back
Top Bottom