Nimejisikia kuwaandikia waraka huu ...

HorsePower

JF-Expert Member
Aug 22, 2008
3,612
2,565
Dear Wana MMU,

Shukrani za kipekee ziwafike kwa michango yenu ambayo binafsi, naamini imemnufaisha kila mmoja wetu si tu kwa mada ziliopostiwa hata kwa comments za wadau zenye ushauri mzuri wa kufariji, kuelimisha sometimes na jokes za hapa na pale za kukufanya uipende JF!

Kuna wengine wamenufaika kwa kupata marafiki, wachumba, kazi, deal za pesa, kuondoa upweke, msongo wa mawazo nk, lakini pia wapo waliokuwa addicted sana na JF kiasi hata cha kushindwa kumaliza kazi zao muhimu za kiofisi kwa wakati, na kuzorotesha performance za makampuni yao! Kuna wengine wamekuwa wakichelewa hata kulala kwa ajili ya JF!
Wapo waliotoa ushauri mbaya kwa kukusudia au kutokukusudia na kujikuta wamevunja mahusiano ya watu. Binafsi sikufurahia, ila tunawaombea maana kwa uhalisia kila mtu ana mtazamo wake na kila alifanyalo mtu ni sahihi sana mbele ya macho yake mwenyewe hata kama ni baya!

Tunapoelekea kwenye Christmas na mwaka mpya, wana JF tumuombe Mungu atusamehe kwa yote mabaya tuliyoyafanya kwa mwaka huu na kuyaacha. Tujitahidi kuwa watu wema, waungwana, tusio na hila wala lawama mioyoni mwetu.
Tushauri ktk kujenga na kuimarisha ndoa na mahusiano ya watu huku tukijitahidi kuondoa infidelity na fikra za maovu.Comments zetu zisitazame hoja imepostiwa na nani bali msg iliyomo bila kuipinga hoja ya mtu kwa kuendekeza chuki binafsi.

Tujichunge na UKIMWI, tujitume makazini, tuache ubinafsi, tupige vita rushwa, tuchukie na kupiga vita ufisadi, tuwe wazalendo kwa nchi yetu, tuchague viongozi wachapa kazi wenye sifa, tuache dharau, na tuweke mipango ya maendeleo ili tuweze kuwa na maisha bora na kuijenga nchi yetu.

Na kwa wale Kupe waliozoea kusoma humu topics za wengine na kucopy na kuwatumia wengine kwenye emails kana kwamba wameziandika wao bila kutoa mchango wowote hapa jukwaani, mjirekebishe, msilitumie jukwaa hili kwa manufaa yenu binafsi, huo ni unyonyaji!

Nawataki kila lililo jema na mafanikio mema ktk mwaka ujao. Mfanikiwe makzini,kwenye biashara na shughuli binafsi. Mungu akutane na mahitaji ya mioyo yenu. Baraka zake, upendo na ulinzi wake uwe nanyi daima.

Kila la kheri,

HorsePower :A S 465:
 
ahsante kwa waraka maridhawa.
Ila mkuu kwenye ishu ya infii i beg to differ,infii ina starehe yake bana!ile excitement ya woga wa kukamatwa,ni mzuka tu aisee,pure exihilation,mi siachi infiii,lol!
Yaliyobaki swadakta nakubaliana nayo.
 
ahsante kwa waraka maridhawa.
Ila mkuu kwenye ishu ya infii i beg to differ,infii ina starehe yake bana!
Yaliyobaki swadakta nakubaliana nayo.
Du!
Hakyanani, hii kali!...Bishanga hivi ulishaoa, au unaongelea infi wakati unamiliki demu?
 
ouh dis z awesome jaman.
tnx horsepower kwa ujumbe mtamu mzur na wakuelimisha pia.
same 2 u lkn. wish u mary x mas n prosperous new year.
gud luck.
 
ahsante kwa waraka maridhawa.
Ila mkuu kwenye ishu ya infii i beg to differ,infii ina starehe yake bana!ile excitement ya woga wa kukamatwa,ni mzuka tu aisee,mi siachi infiii,lol!
Yaliyobaki swadakta nakubaliana nayo.

Bishanga, kwa nini usiwe na wako ukawa na hati milki? Kwa nini uendekeze maisha ya kula raha kwa woga? excitement gani unayoipata ukila raha kwa woga? Huogopi mambo mabaya ukikamatwa?
 
tuwe wazalendo kwa nchi yetu, tuchague viongozi wachapa kazi wenye sifa, tuache dharau, na tuweke mipango ya maendeleo ili tuweze kuwa na maisha bora na kuijenga nchi yetu.


HorsePower :A S 465:

Ahsane sana ndugu HP,

Ujumbe wako mzuri sana....Ila kwenye hilo eneo, napata shida kwani nchi yenyewe tunayotakiwa kuwa na uzalendo nayo ni kama imeshauzwa......Sasa kama ni hivyo, tunaanzia wapi??

Mubarikiwe sana,...pamoja na Bishanga Bashaija wetu!!

Babu DC!!
 
@HorsePower, asante mkuu kwa walaka wako mzuri uliojaa maneno ya busara! Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema na atujaalie sisi sote baraka zake!!
 
Bishanga, kwa nini usiwe na wako ukawa na hati milki? Kwa nini uendekeze maisha ya kula raha kwa woga? excitement gani unayoipata ukila raha kwa woga? Huogopi mambo mabaya ukikamatwa?
cheating ingekuwa movie mimi ningekuwa
tom cruise,ingekuwa golf ningekuwa tiger woods na ingekuwa kabumbu ningekuwa Ryan Giggs!
 
Ahsane sana ndugu HP,

Ujumbe wako mzuri sana....Ila kwenye hilo eneo, napata shida kwani nchi yenyewe tunayotakiwa kuwa na uzalendo nayo ni kama imeshauzwa......Sasa kama ni hivyo, tunaanzia wapi??

Mubarikiwe sana,...pamoja na Bishanga Bashaija wetu!!

Babu DC!!
ahsante kwa dua Mkuu,i am trying to tell it as i see it.
 
Thanx,lakini mngekua mnakumbushana daily,mi nawatakia mafanikio siku zote,i dont care about ex-mas or new year!!
 
@HorsePower, asante mkuu kwa walaka wako mzuri uliojaa maneno ya busara! Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema na atujaalie sisi sote baraka zake!!
ahsante Kipipi nitamfikia salam maana saa hizi kalala maana baada ya kupost uzi alirudi kwenye blanket,si unaona kamvua?
 
Back
Top Bottom