Nimejiletea balaa mwenyewe?

HorsePower

JF-Expert Member
Aug 22, 2008
3,612
2,566
Jamani mwenzenu ninafanya kazi kwenye ofisi moja hapa DSM. Kwa Bahati nzuri au mbaya, niko ofisi moja na my wife, lakini kwenye idara tofauti.

Nimezoeana na wadada kadhaa wa hapa ofisini husasan wa idara moja nami, utani na maneno ya hapa na pale mara nyingi huwatawala ofisi yetu! Asubuhi alikuja dada mmoja ambaye huwa tumezoea kutaniana tu – Kamwe hatuna mahusiano yoyote aliniletea mafaili ya kufanyia kazi. Nilipomuangalia nikagundua kuwa kwa bahati mbaya alijichafua na vumbi kwenye kiti alichokalia huko ofisini kwake, na nilipogundua nikamfahamisha kuwa amechafuka. Alinirushia leso yake, akiomba nimfute, nami bila hiyana nikamfuta vumbi.

Wakati zoezi likiendelea wife akaingia na mafaili mengine kunipitishia, na kunikuta nikimalizia kumfuta dada huyu. Kwa kuona hivi, wife kaja juu kwa nini nimfute dada maeneo hayo kama kweli sina uhusiano wowote naye na limezuka zogo kubwa nyumbani kwangu.
Jamani, hivi ni kosa kumfuta mtu vumbi? Au ndo nimejiletea balaa mwenyewe?
Naomba ushauri, mahusiano ya ndoa yangu yameingia doa!

**** Kuna ndugu alituma malezo haya kuniomba ushauri, nami nimeamua kuwaletea kama ilivyo, kwa pamoja tumshauri ndugu yetu. *****

Wenu,
HP
 
Muulize huyo 'ndugu', akimkuta mkewe anamfuta mfanyakazi mwenzie wa kiumbe makalio vumbi, ama anamfunga zipu ya sarawili kwa sababu imenasa kwenye underwear; atajiskiaje? Kama ni sawa amuambie mkewe its no big deal, na wewe futa wanaume makalio huko idarani kwenu. Mke ata-calm down na kujiachia
 
kwanza hapo naona zoezi la kumfuta vumbi lilichukua muda mrefu pili umeyataka mwenyewe
 
Pole,lakini anahaki na kukasirika kwani sio yeye tu hata wewe ungemuona yeye anafanya hivyo usinge penda.. muombe msamaha na tabia hiyo uwache utani gani wa kiasi hicho.
 
HP nina wasiwasi umefungua biashara ya ushauri wa masuala ya mahusiano na inalipa vizuri tu. Kila siku wewe unaletewa kesi tu!!! Tugaie chetu bana!
 
hapo umekosea tena sana, utani gani wakufutana vumbi kwenye makalio kama ndo wewe umemkuta wife ndo anafanya hvo ungejisikiaje?
 
Hebu hio ishu ifanye vais vesa,
Na mtuhumiwa awe mkeo ungejisikiaje?
Ukijibu hapo hope utajua mkeo anastahili kukasirika au?
Then utajua cha kufanya,
Punguza utani usio na maana na wanawake coz unajua uko ofic moja na mkeo.
 
Jamani mwenzenu ninafanya kazi kwenye ofisi moja hapa DSM. Kwa Bahati nzuri au mbaya, niko ofisi moja na my wife, lakini kwenye idara tofauti.

Nimezoeana na wadada kadhaa wa hapa ofisini husasan wa idara moja nami, utani na maneno ya hapa na pale mara nyingi huwatawala ofisi yetu! Asubuhi alikuja dada mmoja ambaye huwa tumezoea kutaniana tu – Kamwe hatuna mahusiano yoyote aliniletea mafaili ya kufanyia kazi. Nilipomuangalia nikagundua kuwa kwa bahati mbaya alijichafua na vumbi kwenye kiti alichokalia huko ofisini kwake, na nilipogundua nikamfahamisha kuwa amechafuka. Alinirushia leso yake, akiomba nimfute, nami bila hiyana nikamfuta vumbi.

Wakati zoezi likiendelea wife akaingia na mafaili mengine kunipitishia, na kunikuta nikimalizia kumfuta dada huyu. Kwa kuona hivi, wife kaja juu kwa nini nimfute dada maeneo hayo kama kweli sina uhusiano wowote naye na limezuka zogo kubwa nyumbani kwangu.
Jamani, hivi ni kosa kumfuta mtu vumbi? Au ndo nimejiletea balaa mwenyewe?
Naomba ushauri, mahusiano ya ndoa yangu yameingia doa!

**** Kuna ndugu alituma malezo haya kuniomba ushauri, nami nimeamua kuwaletea kama ilivyo, kwa pamoja tumshauri ndugu yetu. *****

Wenu,
HP

naona unajichanganya,
hapo kwenye redi imekuwaje wakati imetokea leo hii
tena ofisin.
 
Horse itakuwa imepasuka
Be serious

Mshikane makalio ofisini?
Yarabi tobaaa!
 
ni kama heading inavyosema AMEJILETEA BALAA MWENYEWE HUYO.
amuombe mkewe msamaha , ndio kakosa tana kosa kubwa.
ukiwa ofis moja na mkeo jiheshimu jaman mmh.
 
Punguza utani bwana muheshimu mkeo...,......nakusìhi muombe msamaha mkeo
 
naona unajichanganya,
hapo kwenye redi imekuwaje wakati imetokea leo hii
tena ofisin.

Nafikiri haujanielewa mpendwa, maelezo haya nilitumiwa mimi last week 29/12/2011 mchana, na nilichokifanya ni copy paste ili tumsaidie mawazo. Hakuna kujichanganya hapo, labda umeelewa tofauti. Ni mambo yaliyomkuta huyo aliyekuwa akisimulia asbh ya siku ya hilo tukio. Pole.
 
Back
Top Bottom