Nimeitwa kutoa "Mawaidha" kwenye bag party...

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,178
7,319
baba mmoja amemuandalia kijana wake bag party (sijui ndo zinaitwa hivyo!), kwa ajili ya kumpa mawaidha ya mwisho, kabla hajaoa hivi karibuni. Katika hali ambayo sikuitarajia,amenialika kama mmoja wa watoa mawaidha kwa kijana siku hiyo eti kama kijana mwenzake, niliyeoa miaka ya karibuni. Sasa najiuliza nikaongee nini? Asprin, Roya, Teamo, Finest na wengine, hebu nipeni point... Baba Askofu naomba uzichuje vizuri watakapozitoa, zisiende kumuharibu kijana...
 
Haaaaah wataalamu wamegoma!!!!!!!!!!!!
Labda waulize upande wa pili labda watakuwa na mawazo mazuri tafadhari akina Nyamayao, Rose1980, FL1, n.k muokoeni jamaa kwa kumpa pointi, maana timu ya akina ASPRIN wamemchunia!!
 
nenda kamwambie huyo kijana mwenzio akishikwa ashikamane......ooops sry namaanisha akashikamane na mkewe aache infiiii.........sory usije haribu anyway mwambie ndoa ndoano.....and usiwe much talking utaharibu
 
Hahaha
pamoja namwaidhaa yooote. umnong'oneze kijana kuwa kuna chama cha maINFIDELITY anapaswa kujiunga nacho the same week anapokuwa amepata jiko.
huko ndo atakapopata elimu mbadala ya kumkinga na masaibu ya wanawake wenye kimbelembele cha kufumania
 
we!
 
Haaaaah wataalamu wamegoma!!!!!!!!!!!!
Labda waulize upande wa pili labda watakuwa na mawazo mazuri tafadhari akina Nyamayao, Rose1980, FL1, n.k muokoeni jamaa kwa kumpa pointi, maana timu ya akina ASPRIN wamemchunia!!
mmh sa kwan mimi mwwanaume...
mwambie tu uhaminifu +upendo ndo ngao ya ndoa
 
Kamwambie from day one aanze kurudi home saa nane usiku, maana hawakawii kusema "mume wangu siku hizi amebadilika"
 
huyo mnaetaka kumpa mawaidha mjue anayajua yooooote ndio kafika bei anataka kuhalalisha tu lakini 'kablia' alishaanza kitambo! in fact mambo yakumpa mtu mawaidha kwa miaka ya leo ni almost hayana maana watu wanakuwa wameshajipa mawaidha yao wenyewe wakakubaliana ndio wanapooana inakuwa kama mtu anaoa mke/mumewe walianza kityambo sana. mwambie aendelee kumpenda mkewe hata baada ya kumuoa maana wengine after ndoa upendo hupoa! akiwa na mapenzi nae ya dhati mengine yote yatapatikana ndani ya upendo. kumbuka upendo haujivuni, hauhesabu mabaya, hauhusudu, hauhukumu n.k. n.k.
 
Feedback; Nawashukuru wale wote walionipa ushauri, ingawa mwingine ulichelewa sikuuona. Actually shughuli yenyewe ilikuwa jana. Kwa kweli hata mimi nilijishangaa jinsi nilivyoumbiwa kipaji cha kushauri. Maneno yalikuwa yanabubujika sijui hata yalikuwa yanatoka wapi. Unajua tofauti na wengine waliokuwepo pale ambao walikuwa wanasema kuhusu upendo, kuzungumza, kutoshelezana n.k mi niliamua kumwaga point zangu katika topic kuwa mume na mke wanaungana lakini kama vein diagram. Yaani ingawa kunakuwa na kuungana lakini lazima kuna maeneo yakabaki free kwa kila mtu. Sio kila kitu unachofanya au anachofanya yeye mna ulazima wa kuambizana. Lazima waheshimu privacy katika mambo machache, na hapo ndo nilikuwa nasisitiza namna ya kuyahandle 'kwa usalama' yale mambo ambayo atakuwa anayafanya na haitakiwi mkewe kuyafahamu...
 
mkuu ingekuwa vyema kama ungeyaeleza yote hapa kama ulivyotaka kuelezwa mkuu tupate na ss mchango
 
Mafanikio ya ushauri wako (na yaa wengine waliosema chochote) yatapimwa huko mbele - ndoa itakavyodumu au vinginevyo.
 
baba mmoja amemuandalia kijana wake bag party (sijui ndo zinaitwa hivyo!), kwa ajili ya kumpa mawaidha ya mwisho, kabla hajaoa hivi karibuni. Katika hali ambayo sikuitarajia,amenialika kama mmoja wa watoa mawaidha kwa kijana siku hiyo eti kama kijana mwenzake, niliyeoa miaka ya karibuni. Sasa najiuliza nikaongee nini? Asprin, Roya, Teamo, Finest na wengine, hebu nipeni point... Baba Askofu naomba uzichuje vizuri watakapozitoa, zisiende kumuharibu kijana...
Hivi, wahudhuriaji wa hii party Ni Ke au Me?
 
Back
Top Bottom