Nimeingia choo cha kike ...........! (4)

Hahahahaha wadau mmenifurahisha kweli.
Story imenisisimua sana HP, njoo basi!
 
Hawa wenye majina ya akina 'enjo'.ok m naona tuanze na uchambuzi wa fani kisha maudhui,na tukikukubali tuangalie uwezekano wa kwenda kwa Shigongo au w wanaonaje!
 
HP Sikuamini kuwa nia yako ilikuwa ni kutuacha solemba namna hii.Binafsi nimeshindwa kujifunza chochote kuhusu kisa hiki
 
Niliendelea kusikia maneno na mawazo yakikizunguka kichwa changu. Moyo wangu na akili zangu zilikuwa katika vita vikali, moyo ukipenda na kutamani wakati sheria ya akili yangu ikijawa na tahadhari ,huruma na uzalendo juu ya uhusiano ninaotaka kuulazimisha. Wakati wote huo, Angel alikuwa mbele yangu, kajiinamia akijaribu kucheza cheza na simu yake ya mkononi. Ni dhahiri pia alikuwa ametawaliwa na aina fulani ya hofu kuhusiana na jibu alilonipa. “Asante angel kwa jibu ulilonipa …” Nilizungumza kwa utulivu “ni wadada wachache sana wenye uwezo wa kuzungumza ukweli kulinda mahusiano yao na wenzi wao, na wewe umekuwa mmoja wao ….. Nimefurahi kwa uaminifu wako ….” Niliongeza. Ni kweli HP, ni kweli kabisa, sasa mi naomba nikuache tutaonana jtatu kazini” alizungumza haraka haraka huku akiinuka na kuanza kuondoka. Sikutaka kumkatiza, nilimsindikiza, akaingia kwenye gari, akaniaga na kuondoka.

Kwa dakika 20 zaidi nilisalia Brajec Pub nikitafakari mchakato mzima ulivyokuwa. Maswali mengi yalinizunguka na kujikuta nikijijibu mwenyewe na kunifanya nijichanganye zaidi. Niliamua kulipia vinywaji, nikaingia kwenye gari yangu tayari kuelekea kwangu.

“Karibu Mkoa wa Pwani” kilikuwa ni kibao pembeni ya barabara ya kuelekea bagamoyo kilichonifanya nigunduwe kuwa nilikuwa nimepitiliza nyumbani kwangu. Ktk hali ya kawaida ilipaswa nipige breki maeneo ya boko CCM na kukunja kuelekea kwenye nyumba yangu. Nilijilaumu sana kwa kutokuwa mwangalifu wa kufikia hatua hata ya kupitiliza kwangu. Niligeuza na kurudi nyumbani kwa mwendo wa taratibu sana. Wazo lililonijiwa haraka haraka ilikuwa na kufuta hali hiyo iliyojijenga kwa siku mbili tu kichwani kwangu kwa kasi ya ajabu mno. Niliamua kujiliwaza kwa kuingia jamii forums na kupitia mada mbali mbali ambazo zimepostiwa na JF members mbali mbali. Nilipitia mada na comments za Mtambuzi, Bishanga, Masikini_jeuri, Judgment, The Boss, AshaDii, Smile,Obsesd, Badili Tabia, PakaJimmy, SweetyLady, Husninyo, Kongosho, Mwanakijiji, FirstLady1 na wengineo wengi. Kwa ujumla JF ilinifariji sana ktk hali niliyokuwa nayo. Lakini, haikusaidia kuniondoa ktk dimbwi la mawazo. Nilitafuta “Boring books” na kuanza kusoma ambazo zilinifanya nipitiwe na usingizi kwa haraka.

Jmosi nilishinda kwa rafiki zangu kadhaa tukibadilishana mawazo juu ya biashara mbali mbali tunazofanya nje ya kazi na kuangalia ligi za mpira wa miguu za nchi za nje, na kunipa ubize, uliofanya siku iishe mapema. Jpili jioni nilikuwa na laptop yangu nikiandaa report na kazi za kupambana nazo jtatu kazini. Nilisikia mlio wa sms nikaamua kuchukua simu na kuchungulia inbox “Mambo HP, kimya?” “Poa, tight na maandalizi ya kazi za kesho” Nilimjibu na kuendelea na kazi yangu. “Nakusumbua ?“ Aliuliza. Kwa kipindi kile nilikuwa nimedhamiria kukaa mbali na huyu binti. Nilijua wazi si vyema sana kumng’ang’ania mtu asiye wako. “Busy!” Nilimjibu. “Huwezi kuchat hata kwa dk moja?” Aliuliza. “Busy!” Nilijibu. “Umewahi kuwa na huruma?” aliuliza. Nilishtuka kwa hili swali na nilihisi kengele ikigonga kichwani pangu. “Huruma, una maanisha nini?” “Muenekano wako ulivyo na matendo yako kama tofauti vile …” Alijibu. Nilielewa wazi ni wapi anaelekea ni nilifahamu wazi hatari inayoanza kunikabili. “Hapana, nipo kama nilivyo” Nilijibu. “Unashindwa nini kupoteza five minutes or less kuongea na mimi? Mtu unayempenda?” Aliuliza. “Sipenda kujibizana na wake za watu usiku, si vyema na ni hatari kwa mahusiano yako”. Nilimjibu. “Wewe unajua niko wapi na niko na nani?” “Sidhani kama kuna umuhimu wa mimi kujua hayo, huo si wajibu wangu; yupo anyepaswa kufanya hivyo!” Nilijibu “Nilijuwa wewe ni katili sana, yaani hauhitaji kujua niko wapi? Je kama nadhurika?” Aliuliza “Mimi si katili, ila napenda kuheshimu mahusiano ya watu na isitoshe aliye ktk hali ya kudhurika hana muda wa kuandika meseji.” “una maanisha napretend?” aliuliza. “Naomba muda Angel, kuna kazi namalizia” Nilimjibu “Mbona leo umekuwa tofauti na juzi? Majibu yako kama siyaelewi hivi”? aliuliza. “Busy” Nilijibu. Ghafla nilisikia simu ilikianza kuita. Sikuweza kujua nini hasa kimenfanya anipigie simu. Nilishusha pumzi na kuinyanyua simu yangu ….

****** Naingia kwenye kikao nikitoka nitawapa mwendelezo wa yaliyonikuta ….******

You are such an amazing writer! Keep it up pal!
 
Back
Top Bottom