Elections 2010 Nimeibiwa kura zangu - Mwantumu Mahiza

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,906
22,052
Jamani nimesoma magazeti ya sikumbili tatu huyu mama ati anadai kaibiwa kura nahisi awakumchagua na ni mmoja wa waheshimiwa wa sasa wanaokimbia mashangingi ya uwaziri/unaibu
anyway mama pole sana nimeona magazeti manne yanakuongelewa wewe yawezekana wewe ni mmoja tu ama robo ya waathirika tuwaachie nec walete upupu wao so far mama karibu chadema upate haki yako ya kikatiba kama pesa ushakula za kutosha mama njoo na huku tukupe uwaziri kamili sio kila siku unaibu unaibu...polen hii ndido chichiem aliondoka nayo nyerere
 
Jamani nimesoma magazeti ya sikumbili tatu huyu mama ati anadai kaibiwa kura nahisi awakumchagua na ni mmoja wa waheshimiwa wa sasa wanaokimbia mashangingi ya uwaziri/unaibu
anyway mama pole sana nimeona magazeti manne yanakuongelewa wewe yawezekana wewe ni mmoja tu ama robo ya waathirika tuwaachie nec walete upupu wao so far mama karibu chadema upate haki yako ya kikatiba kama pesa ushakula za kutosha mama njoo na huku tukupe uwaziri kamili sio kila siku unaibu unaibu...polen hii ndido chichiem aliondoka nayo nyerere

Kama wametenda hivi kwa mti mbichi, itakuwaje kwa kijiti kikavu???:A S-confused1:
 
Na kidomo domo chake chote still watu hawakuangalia makunyanzi!!
Siasa hizi!!
Piga chini tu, kwenda kule.
 
anavuna alichopanda! yeye si alisema walimu kama hawawezi kazi watafute kazi nyingine.

ama kweli saa ya ukombozi ni SASA.
 
Twamwomba atuambie idadi ya wanachama wa CCM waliojiandikisha katika hilo Jimbo, Pili watupe idadi ya wana ccm walioenda kupiga kura na atuambie ni idadi ipi hawakwenda kupiga kura na atuambi ni idadi ipi aliyo pata yeye na ipi aliibiwa?

Me sina wasiwasi na kura za maoni ila Ethics zake(ktk Kura za maoni) ndio zilikuwa na shida nashangaaa wengi kuli kuwa wameibiwa kura na pale walipokuwa wanaanza huu mchakato mbona hawakuhoji kutaka kujua athari zake ni zipi?

Last week nilikuwa nikisikia PB ktk Clouds FM Gerald Hando anasema matatizo na vimbwanga vyote na madudu yote yaliyotokea katika chaguzi za kura za maoni ndani ya CCM wajijibu na wajisuruhishe wao wenyewe kwani wao ndio waliojitakia wasiyalete huku nje kwanini wao hawakujua hilo hawakuwa na tahadhali kwa mchakato huo mzima.
 
CCM wakiibiana kura wao kwa wao ni nafuu ya UPINZANI, maana washabiki ya ambaye ataona hajatendewa haki watapiga kura ya chuki kwenye uchaguzi mkuu. Subirini kwanza CC na NEC waweke mambo hadharani na mwaka huu hakuna kurudia nominations maana mara ya 14/8, wateule wanatakiwa kuchukua fomu Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Kwa hiyo wale watakaotendwa itakuwa imekula kwao.
 
Uyu mama confidence lilizidi kisa zamani alikuwa bosi wa mama Salma imekula kwake.
Nae atafute kazi ingine kama alivyowaambia walimu
 
Kwani lazima ashinde kura za maoni za CCM 2010? Wanawake wengine bana, akili za mbayuwayu
 
"Walimu kama mnaona mshahara huu tunaowalipa hautoshi acheni kazi hii na nendeni kutafua kazi ingine"Nanmkuru mama Mwantumu Mahiza akiwaambia walimu wa serikali ya Muungnano wa TZ alipokuwa kwenye ziara ya kikazi Mkoani Mtwara/Lindi mwaka jana!

Kama Mama huyu kwa kauli hii angekuwa anagombea kwenye jimbo la watu wenye msimamo mikali kama vile Mtera(Dodoma),Kyela(Mbeya)hata jimbo lolote lililopo ZNZ hasa Pemba siku ile ya kuchukua fomu angekutana na wananchi wenye hasira nje ya ofisi za CCM na kumtaka ili kutuliza hasira zao aichane pale pale fomu ya kugombea aliyoichukua!

Kumuachia hadi kushindwa na Danstan Kitandula ni udhaifu ungine waliouonyesha wana Tanga;kauli ya kukera na hovyohovyo kama ile bado anajaribu hata kushika nafasi ya pili?Huyu alistahili akose hata sifa ya kuchukua fomu;"wazee"walitakiwa watumwe kumuambia kuwa hata fomu hatakiwi kuchukua maana ataleta mpasuka mkubwa ndani ya CCM wilayani, wananchi wasio wafuasi wa CCM na familia za walimu alio wasimanga!

Mama Mahiza;kazi zipo nyingi tu mbona,kazi sio tu lzm uwe mbunge!
 
Nadhani Mwantumu analalamika tu kwa sababu labda anataka kuwa-fool NEC wamwokoe. Kuna baadhi ya kata alidai kuibiwa kura na uchaguzi umerudiwa week end hii lakini bado kashindwa. Inasemekana aliwatolea mbofu mbofu wananchi na wameapa kutomsamehe. Nasikia aliwambia kuwa wadigo hawana lolote kwani msambaa mmoja ni sawa na wadigo 10. Pia aliwaeleza kuwa lazima ashinde kwani suala hilo ni sawa na msemo wa kiswahili unaosema kuwa "heri punda afe lakini mzigo wa bwana ufike". Kwa hiyo wananchi wanalazimika kumchagua yeye. Na pamoja na kutoa rushwa nje nje (nasikia kuna mama alikamatwa na 600K akakiri kuwa amepewa na Mwantumu) lakini bado wamempigaa chini. Kwa hiyo anaweza kuendelea kulalamika ila inabidi ajilaumu mwenyewe. Na NEC wakipindisha matokeo inaweza kuwatokea puani!
 
CCM aka Deep Green kweli ni noma. Ili ufanikiwe ni lazima uwe:
  • Mzandiki na mfitini
  • Usiwe kidomodomo
  • Uwe ndumilakuwili
  • Associate of EL and RA
  • Hela iwe imepiga kambi kwako
  • Uwe kimbelembele
  • ... mengine jazieni :becky:
 
Nyerere aliwahi kusema CCM sio mama yake anaweza kutoka wakati wowote sasa hawa wanaolalamika na kubaki humo wanauchungu gani na CCM walioikuta?
 
Back
Top Bottom