Nimehuzunishwa: Msome Mwandishi Athumani Hamisi kisha Chukua Hatua Kumsaidia

...Aliporudi kutoka kwenye matibabu SAfrika walimpa jina la 'Mpiganaji' na kila mtu/taasisi mwenye jina mjini alijibainisha naye na kutoa ahadi kem kem. Miaka mitatu tu baadae wameishamsahau na kumuona sio Habari tena hadi yeye mawenyewe ameamua kuwa Habari ili kupata msaada. Pole Ndugu yetu Athumani Hamisi. Ndio binadamu walivyo. Mungu atakupitisha katika wakati huu mgumu unaopita. Nashauri pia uusome kwa makini Ujumbe muhimu wa muungwana Mtambuzi na ujaribu kuufanyia kazi. Utakusaidia. Pole Sana ndugu Yetu. Yote yatoka kwa Mungu.
 
Ndio nimeiona hii habari, naninakumbuka kwa usahihi kabisa juu ya ajali hiyo iliyompata mwenzetu.
Mimi sipendi unafiki, ninachoweza kumshauri ndugu yangu huyu ni kujaribu kupunguza bajeti yake......... ingawa wazo hili limechelewa, lakini hata hivyo anaweza kuangalia bajeti yake na kuipunguza.
Kitu cha kwanza ilitakiwa atafute nyumba za bei rahisi kidogo, Kukaa sinza kuna gharama kubwa sana, kwa mfano angeweza kuhamia Mwananyamala karibu na hospitali kwani pale anaweza kupata nyumba nzuri kwa bei nafuu kidogo, pili gharama za shule za watoto nazo zinamkamua sana, najua alikuwa na lengo la kuwasomesha wanae shule nzuri za English Medium, lakini kwa hali yake kwa sasa inabidi ageukie shule za akina Kayumba...... (najua utakuwa ni uamuzi mgumu),
tatu, ajishughulishe na shughuli za kiuchumi, kuna namna nyingi za kujiongezea kipato, kwa mfano kwa kuwa taaluma yake ni mpiga pisha wa magazeti, basi angejifunza uandishi wa makala hata kwa njia ya mtandao na angekuwa anafanya kazi akiwa nyumbani....
kingine labda angetafuta ujuzi wowote wa kazi za mikono, sidhani kama angetangaza kupitia vyombo vya habari kwamba anatafuta mwalimu wa kumfundisha kazi za mikono angekosa.... Naamini angepata na hata gharama za kumlipa wangejitokeza wafadhili....... Kutegemea wafadhili kwa misaada ya kila siku huku ukiwa na maisha ghali ni shida kidogo.....
Naamini kamaatafuata ushauri wangu anaweza kuvuka mtihani huu mgumu.....
Nakumbuka wakati fualni niliwahi kuandika makala kuhusu tajiri mmoja wa kule Colorado nchini Marekani, yeye alimudu kusimama na kuwa tajiri mkubwa nchini humo pamoja na misukosuko ajali alizowahi kupana na kuwa mlemavu kama alivyo Athumani.

Ukitaka kusoma habari hiyo unaweza kubofya hapa:

https://www.jamiiforums.com/jf-chit...dia-zaidi-wale-waliokata-tamaa-ya-maisha.html

Asante sana Mtambuzi nimeupenda ushauri wako, kuukwepa unafiki kunaweza kusaidia kupata ufumbuzi kwa urahisi zaidi. Natumaini hapa JF kuna watu wanaomfahamu kwa ukaribu na wanaweza kumpa ushauri ulioutoa.
 
Last edited by a moderator:
... Watu wanaweza kuchangia pesa na hizo pesa badala ya kuzitumia zote ashauriwe namna ya kuzifanyia mradi ambapo pia atashauriwa namna ya kupata wasimamizi wa huo mradi maana yeye katika hali yake hataweza kusimamia na mawazo mengine ya kumsaidia ili mradi aondokane na huu utegemezi mkubwa aliyotumbukia baada ya ajali.

mwaJ Ushauri huu nimeupenda sana! Uko very practice na unapungaza utegemezi! I hope atawezeshwa na wanahabari wenzake kupta michango hii inayotolewa hapa ya kiushauri na kumpa moyo! Ona mawazo yako yakiunganishwa na ya Mtambuzi hasa point no Nne na Tano yatakavyokuwa very enlightening!

Kitu cha kwanza ilitakiwa atafute nyumba za bei rahisi kidogo, Kukaa sinza kuna gharama kubwa sana, kwa mfano angeweza kuhamia Mwananyamala karibu na hospitali kwani pale anaweza kupata nyumba nzuri kwa bei nafuu kidogo,

Pili gharama za shule za watoto nazo zinamkamua sana, najua alikuwa na lengo la kuwasomesha wanae shule nzuri za English Medium, lakini kwa hali yake kwa sasa inabidi ageukie shule za akina Kayumba...... (najua utakuwa ni uamuzi mgumu),

Tatu, ajishughulishe na shughuli za kiuchumi, kuna namna nyingi za kujiongezea kipato, kwa mfano kwa kuwa taaluma yake ni mpiga pisha wa magazeti, basi angejifunza uandishi wa makala hata kwa njia ya mtandao na angekuwa anafanya kazi akiwa nyumbani....

Nne, kingine labda angetafuta ujuzi wowote wa kazi za mikono, sidhani kama angetangaza kupitia vyombo vya habari kwamba anatafuta mwalimu wa kumfundisha kazi za mikono angekosa.... Naamini angepata na hata gharama za kumlipa wangejitokeza wafadhili.......

Tano Nakumbuka wakati fualni niliwahi kuandika makala kuhusu tajiri mmoja wa kule Colorado nchini Marekani, yeye alimudu kusimama na kuwa tajiri mkubwa nchini humo pamoja na misukosuko ajali alizowahi kupana na kuwa mlemavu kama alivyo Athumani. Ukitaka kusoma habari hiyo unaweza kubofya hapa:

https://www.jamiiforums.com/jf-chit...dia-zaidi-wale-waliokata-tamaa-ya-maisha.html

Ushauri huu pamoja na Kuchangiwa na marafiki na ndugu amabako hakutadumu, utakuwa wa manufaa na wa dhati!

Lets hope ushauri ataupata!
 
Last edited by a moderator:
Sorry mpenzi, mi nipo ila naona mada imekaa ndefu sana
Mi sipendi kusoma, hua nasinzia katikati, kabla sijamaliza
Tafadhali nipe summary kwanza, kwa kifupi what is the issue?

Acha uvivu Mwali somo tu, mie naona ngumu kutengeneza summary bana. Lakini shosti mbona kule MMU unajibu vikomenti hata mia hausinzii?
 
Last edited by a moderator:
Acha uvivu Mwali somo tu, mie naona ngumu kutengeneza summary bana. Lakini shosti mbona kule MMU unajibu vikomenti hata mia hausinzii?
Nasoma vipost vifupi vifupi kule, sio kama hii.
We hujanistukia tu, mwenzio ni chit chat zaidi
Haya ya kufikiria sana naona niwaachie nyinyi
But kwa vile umeniomba wewe ngoja nisome...
 
mwaJ, Nimesoma thread mwanzo hadi mwisho
Ila niseme tu ukweli si rahisi kuisoma yote :confused2:

Mchango wangu huu hapa (for what its worth):
  1. Aandike (aandikiwe) thread fupi zaidi watu waweze kusoma (I did this)
  2. Aipost jukwaa la sheria, na iwe intended for lawyers and legal advisers
  3. Aweke wazi matatizo yake, na aweke wazi anacho hitaji toka kwa viewers
  4. Binafsi sidhani kama anahitaji msaada wa kifedha ila ni legal advice zaidi

Kwa kurahisisha usomaji na mchango nadhani ni bora tungeweka
post kama hii jukwaa la sheria: kama ni sawa just copy-past it
Kumbuka kuwaambia mods wasiunganishe hizi threads mbili
ili misaada ya kisheria kwa ndugu Athumani ipatikane kirahisi:

JF members, kuna thread nimesoma jukwaa la Habari na hoja mchanganyiko, nimeona nii lete huku:

Kuna ndugu yetu anaitwa Athumani Hamisi. Sasa ni miaka minne tokea apate ajali, Septemba 12, 2008 eneo la Kibiti Mkoani Pwani akiwa na wenzanke, wakiwa njiani kwenda kazini Kilwa mkoani Lindi kikazi.Katika ajali ile, alivunjika shingo naku-damage spinal cord iliyopelekea kupooza mwili wote kuanzia shingoni. Ailipata msaada wa moja kwa moja toka Ikulu (Mhe Jakaya Kikwete), Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, kampuni alio kua akifanyia kazi yamagazeti ya serikali (TSN).

Sasa tatizo lake kubwa ni kukabiliana na gharama za maisha zinazo sababishwa kwa kiasi kikubwa na ulemavu alo upata baada ya ajali ya kikazi. anahitaji pesa ya matibabu, pesa ya kuwalipa wahudumu, pesa ya kuwasomesha wanae watatu na pesa ya matumizi mbali mbali ya nyumbani, sikiongozwa na gharama za kodi ya nyumba pamoja na chakula mbazo kazikadiria kufika laki tisa kwa mwezi (900,00 Tsh)

Kwa bahati mbaya, leo miaka minne baada ya kupata ajali hiyo inaonekana TSN na wafadhili wengine wameanza kuonesha dalili ya kugeuka wajibu wao wa kumsaidia mfanya kazi wao huyu, alie jeruhiwa katika safari ya kikazi. Nadhani hali hii inarahisishwa na kutokuwepo kwa makubaliano ya msingi (na yakuandikwa) kati ya Ndugu Athumani na tajiri wake (TSN). Leo amekua omba omba na msaada ulokua ukitoka kwa urahisi na kwa kufunika mahitaji ya mwaka au zaidi sasa unatoka kwa tabu, na unakuja kufunika mahitaji ya wiki kadhaa tu.

Msaada anao hitaji ni wa kisheria (for a sustainable life, in the long term), na wa kifedha (to implement the legal advices and to cope with the daily expenses as he works on the long term plan)
Msaada wa kisheria unao hitajika:

  1. Ufafanuzi wa haki zake kama mfanya kazi alie pata ajali akiwa kazini
  2. Ufafanuzi wa uwajibikaji wa TSN kama tajiri wake (ukizingatia walianza kulipia huduma na sasa wanaacha)
  3. Hatua za kuchukua ili haki na uwajibikaji vizingatiwe kwenda mbele
  4. Ufafanuzi wa compensation scheme inayo weza kutumika hapa (monthly allowances au one off package)
  5. Msaada wa kisheria (free of charge or at very accessible cost given the situation)
  6. Msaada wa kimawazo au kifedha toka kwa msomaji wowote atakae guswa na habari hii.

Kwa walio tayari kuchangia kimawazo/kisheria, tafadhali weka mawazo yako kwenye thread hii au tembelea http://www.8020fashions.blogspot.com/

kwa walio tayari kuchangia kifedha, misaada ipitie katika

  • account No 01J2027048800 ya CRDB na
  • Account No 010-00090488 ya Postal Bank

​Kwa wanaotumia mitandao ya simu, wanaweza kutumia

  • M-pesa 0757 825 737,
  • Tigopesa 0655 531 188 na
  • Airtel Money 0784 531118;
  • M-Pesa 0767 298 888 ya Chris Mahundi na
  • Airtel Money 0686 710 977 ya Ephraim Mafuru.
​
Asanteni kwa michango.
 
Nasoma vipost vifupi vifupi kule, sio kama hii.
We hujanistukia tu, mwenzio ni chit chat zaidi
Haya ya kufikiria sana naona niwaachie nyinyi
But kwa vile umeniomba wewe ngoja nisome...
Mwali nimekupendajeeee? Yaani wewe ni zaidi ya "mwali"! Nadhani umenipata.
Asante sana pia kwa kutengeneza summary. Ngoja niipost jukwaa la sheria kama ulivyoshauri.
 
Last edited by a moderator:
Azimio Jipya ukiliangalia hili suala kisheria utajiuliza maswali mengi sana kuanzia kwenye malipo ya bima - ajali iliyosababisha kupoteza uwezo wa kufanya kazi, suala la kuumia kazini, je? bado yupo kwenye ajira ya TSN? Kama jibu ni ndio je, mwajiri wake anajukumu gani katika kumhudumia mfanyakazi wa aina yake in terms of accommodation (kumbuka amezungumzia nyumba za staff) n.k.

Njia za kumsaidia zaweza kuwa pamoja na hiyo aliyoomba mwenyewe yaani kumchangia pesa. Lakini hii kwa maoni yangu haitakuwa endelevu maana watu hawataweza kuchangia kila mara anapopungukiwa na ndio maana amesema baadhi ya watu aliowategemea wamechoka na hawapokei hata simu zake.

Lengo la kuileta hii habari JF ni kupata michango ya wana JF ya hali, mali na mawazo pia namna huyu ndugu atakavyoweza kutoka katika hali aliyomo. Watu wanaweza kuchangia pesa na hizo pesa badala ya kuzitumia zote ashauriwe namna ya kuzifanyia mradi ambapo pia atashauriwa namna ya kupata wasimamizi wa huo mradi maana yeye katika hali yake hataweza kusimamia na mawazo mengine ya kumsaidia ili mradi aondokane na huu utegemezi mkubwa aliyotumbukia baada ya ajali.

Najaribu tu kufikiria wako wapi wadada na akina kaka wa JF akina Bishanga Saint Ivuga Bujibuji Mtambuzi Pasco Senetor Mwali Preta sweetlady Kipipi kisukari Smile Michelle charminglady BADILI TABIA na wengineo waje wasaidie mawazo yao katika hili.
mwaJ mpendwa nimeshindwa kumalizia kusoma habari......ni ndefu ntarudi baadae kusoma then ntachangia kile ntakachoelewa!
 
Last edited by a moderator:
Nimesoma taarifa kwenye issamichuzi blogspot na kuona mwajiri wa Athumani (TSN) anatoa ufafanuzi na kuonyesha kuwa hawajamtelekeza Athumani, na wametumia fedha nyingi mpaka sasa na wanaendelea kumhudumia. Sasa sielewi nani ni mkweli Athumani au TSN. Ukisha soma mada katika post hii hapa JF ebu rejea link ifuatayo nawe ujisomee uone zipi mbivu na zipi mbichi.


MICHUZI: TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: TSN HAIJAMTELEKEZA ATHUMANI HAMISI
 
Kuna wanaoshauri apunguze gharama za maisha yake.. Kwenye nyumba itashindikana maana anatakiwa kukaa karibu na hospitali...
Labda kwa gharama za house girl,nurse,na gharama za ada za watoto wake maana wanasoma English Medium schools.. Haya anaweza kushauriwa cha kufanya kwayo..

Once again.. Pole sana Athuman Hamisi
 
hakuwa upande wa mafisadi ndio maana,angekuwa upande wao hangepata shida hivi
 
Back
Top Bottom