Nimehamia Njiro "Kwa Msolla"

Dear Preta.

Sanawari maji ni mengi kwasababu visima vimejengwa eneo hili.hata umeme ni nadra sana kukata najuuuuta kuhama Sanawari.Bibi wewe unaishi maeneo yapi ?.

huko kusiko na maji ni wapi?....au mi naishi Arusha ipi?....au idara ya maji wananipendelea mie tu....poleni sana wapenzi....
 
... On a positive note, upo karibu na samaki (kwa Nick)! I miss A-town alot!
 
Duh umenikumbusha mbali kwa Nick Pub ni maeneo ya Nane nane,kwa Msolla ni mbali kidogo.

... On a positive note, upo karibu na samaki (kwa Nick)! I miss A-town alot!
 
Sweetlady,

Nimeishi Sanawari,Kaloleni sijawahi kukumbana na hali mbaya kiasi hiki.
Na nikuambie tu kuwa hali kama hii haijawahi kutokea arusha, ni hali ambayo inawashangaza wakazi wengi wa arusha. Kiukweli arusha hapajawahi kuwa na tatizo kama lililopo sasa hivi, jaribu kutembelea maeneo tofauti tofauti utagundua arusha kwa sasa maji ni ya shida mno. Mianzini, sanawari, kaloleni, makao mapya, ungaltd, njiro, kijenge, mbauda, majengo, kwa mrombo, faya n.k kote huko kilio chao kikubwa ni maji...
 
Mkuu mwanao anasoma Shalom au Mt Meru ?.Nina watoto wawili moja Mt Meru na mwingine Shalom ni kichwa haswa mwaka juzi R Mengi alimpatia zawadi ya mwanafunzi bora.Hii pia ilikuwa nisababu kubwa ya kuhamia Njiro watoto hawana haja ya usafiri lakini mkuu wakati wa mvua kuna tope la kufa mtu unahitaji moyo mgumu kuishi Njiro.

Mkuu,
Hongera sana kwa hatua hiyo uliyofanya!

Hakika, Eneo la Njiro Kwa Msolla ni kati ya maeneo bora kabisa na ya kisasa, ukiacha shida ya maji!
Mnachoweza kufanya ni kuunganisha nguvu. Mtakapokuwa kama kundi ni rahisi kusikilizwa na mamlaka husika na kufanyiwa mpango wowote, kuliko kila mtu kufanya juhudi binafsi.
Off-records: Broda, Jumapili nilikuwa na shughuli ya mwanangu mtaani kwako hapo, ulikuwepo nini!...?...maaana niliona mtu 3 zinachatt kwenye simu non-stop, nikahisi hawa ni wanabodi!
 
Mkuu MM.

Mkuu hata Sanawari ni kwangu pia Njiro ni nyumba yangu ya nne.Niliamua kuondoka Sanawari kwasababu Njiro nyumba ilimalizika miaka miwili iliyopita kazi ikawa kupata mpangaji wa stahili ya Njiro [angalizo nililenga wafanyakazi wa UNICTR] bahati mbaya UNICTR wanamaliza mikataba yao nikaona bora nijitose mwenyewe.Sanawari wapangaji wako wa kumwaga kabla sijahama tayari nilikuwa na msururu wa wapangaji.

Mkuu AUWSA wameajiri watumishi wa kukabiliana na malalamiko si kwaajili ya kutatua matatizo sina muda wa kuchezea na warasimu sana sana najipanga kuchimba kisima changu.

Makaribisho ni desturi na mila ya mtanzania unakaribishwa sana Arusha.

Mkuu Ngongo,

Umesomeka, ahsante kwa ukaribisho vile vile.
The best solution ni kuwa na kisima chako mwenyewe.

Kama gharama ya kuchimba ni kubwa sana, ambayo inahitaji maandalizi namuda mrefu kidogo lazima utafute short term solution.

Kwahiyo hao watumishi wa AUWSA usiache kuwagasi, hata Sugu amesema walipoongea kwa upole na lugha laini hawakueleweka wala kusikilizwa. lakini baada ya kuongeza ukali kidogo wameanza kusikilizwa. Kwahiyo jitahidi kuwa mkali kidogo ili AUWSA wakusikilkize.

Vinginevyo unganisha nguvu na wanakitaa wenzako, ili mkiwa kundi kubwa kidogo ni rahisi kwa AUWSA kuchukua hatua haraka kuliko ku-fight peke yako.
 
Nimeongea na Eng Ruth Koya Ag Mkurugenzi Mtendaji anadai mota za kusukuma maji zimekufa.Matengenezo yanafuata taratibu za manunuzi eg tenda na mlolongo mwingine mrefu.Hawezi kutengeneza bila kufuata taratibu za manunuzi !!!!!!!!!.Hii sheria ya manunuzi ni kwaajili ya nani ?,Inamnufaisha nani ?.

Habari ndiyo hiyo.

Na nikuambie tu kuwa hali kama hii haijawahi kutokea arusha, ni hali ambayo inawashangaza wakazi wengi wa arusha. Kiukweli arusha hapajawahi kuwa na tatizo kama lililopo sasa hivi, jaribu kutembelea maeneo tofauti tofauti utagundua arusha kwa sasa maji ni ya shida mno. Mianzini, sanawari, kaloleni, makao mapya, ungaltd, njiro, kijenge, mbauda, majengo, kwa mrombo, faya n.k kote huko kilio chao kikubwa ni maji...
 
Ngongo,

Uliza kwanza kabla ya kwenda kujichomeka Njiro. Hivi unaijua njiro kweli wewe
Kwanza hilo eneo halina watu ingawa kuna majengo mengi ya kisasa yamejaa, mafisadi yamejenga halafu yakaterekeza huwa yanakuja kuishi kipindi kuna mikutano tu na wanakunywa Dasani wenzako.

Hebu teremkia hapo kituo cha Amani bar ukapate ile roho inapenda ukitaka maji teremka chini Seminari watu wa kanisa wana visima vya kutosha.
Sanawari au Maeneo ya Ngurero kwa nini hukutaki au Philips, wenzako tukitia timu maeneo kama hayo toka Rocky City tunaishi Sakina hakuna tabu kubwa za maji.

Nakukumbusha tu kwa maana leo ndo umelikumbuka shuka, siku zote unaifagilia CCM laeo yamekukuta acha ujifunze.

RockyCity MWAUWASA yalikatika maji siku tano wiki iliyopita lakini aahh Mungu anatupenda ziwa liko karibu tunajizolea bwerere
 
mkuu Ngongo

nikisoma A leve pale Ilboru 1992 palichimbwa visima (water rigs) vya nguvu sana, yaani vilikwenda chini sana, nakumbuka ulikuwa ni msaada wa DANIDA kama sikosei, je yale maji hayapatikani Arusha mjini
 
Mkuu LAT,

Ni kweli Ilboru,Sanawari,Kimandolu,Enaboishu na Elerai visima vilichimbwa kipindi cha nyuma,idadi ya watu,viwanda na mashamba ya maua yameongezeka sana.Mradi mpya pekee ni ule wa mto Nduruma ambao kwa kweli haujatosheleza mahitaji makubwa hata kidogo.

Tatizo la sasa ni kuharibika kwa mota za kusukuma maji.Sheria ya manunuzi inataka taratibu zote zifuatwe bila kujali hadhaa wanazokumbana nazo wananchi.

mkuu Ngongo

nikisoma A leve pale Ilboru 1992 palichimbwa visima (water rigs) vya nguvu sana, yaani vilikwenda chini sana, nakumbuka ulikuwa ni msaada wa DANIDA kama sikosei, je yale maji hayapatikani Arusha mjini
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Mkuu Spencer,

Salaam,

Napenda kukusahihisha Njiro ya leo ina wakaazi wengi kuliko unavyofikiri labda ulifika Njiro miaka ya 90s.Nyumba nyingi unazoziona zina watu chache sana hazina watu.

Mkuu wangu sijawahi katika maisha yangu kuifagilia CCM ila akitokea kiongozi wa CCM kafanya jambo jema sioni haya kumsifia na mambo ni hivyo hivyo kwa CDM akitokea kiongozi kafanya jambo la maana namsifu bila choyo.Juzi nilimsifu sana Waziri wetu wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Samwel Sitta kwa kukataa kutia saini mkataba wa kuruhusu ardhi ya Tanzania kuingizwa EAC.Mkuu kwa vyovyote utakuwa unachanganya mambo hasa ninapokosoa mapungufu ya CDM.Fikra zako zinakutuma kwamba anayekosoa CDM ni MwanaCCM au anayekosoa CCM ni mwanaCDM hapana mkuu wangu mimi ni mtu huru sijafungwa na minyororo ya chama chochote.

Ukiondoa uhaba wa maji Njiro ni sehemu bora sana ukilinganisha na maeneo mengine ya jiji la Arusha lenye ukosefu mkubwa wa miundombinu kama barabara,masoko,mitaro na mifereji ya kuondoa maji barabara hasa kipindi cha mvua.

Ngongo,

Uliza kwanza kabla ya kwenda kujichomeka Njiro. Hivi unaijua njiro kweli wewe
Kwanza hilo eneo halina watu ingawa kuna majengo mengi ya kisasa yamejaa, mafisadi yamejenga halafu yakaterekeza huwa yanakuja kuishi kipindi kuna mikutano tu na wanakunywa Dasani wenzako.

Hebu teremkia hapo kituo cha Amani bar ukapate ile roho inapenda ukitaka maji teremka chini Seminari watu wa kanisa wana visima vya kutosha.
Sanawari au Maeneo ya Ngurero kwa nini hukutaki au Philips, wenzako tukitia timu maeneo kama hayo toka Rocky City tunaishi Sakina hakuna tabu kubwa za maji.

Nakukumbusha tu kwa maana leo ndo umelikumbuka shuka, siku zote unaifagilia CCM laeo yamekukuta acha ujifunze.

RockyCity MWAUWASA yalikatika maji siku tano wiki iliyopita lakini aahh Mungu anatupenda ziwa liko karibu tunajizolea bwerere
 
Mkuu mwanao anasoma Shalom au Mt Meru ?.Nina watoto wawili moja Mt Meru na mwingine Shalom ni kichwa haswa mwaka juzi R Mengi alimpatia zawadi ya mwanafunzi bora.Hii pia ilikuwa nisababu kubwa ya kuhamia Njiro watoto hawana haja ya usafiri lakini mkuu wakati wa mvua kuna tope la kufa mtu unahitaji moyo mgumu kuishi Njiro.

niliwahi kukwama mwaka juzi siku nzima nikahamia pale matongee kusuuza roho kwani nilichoka sana
bei ya viwanja imefika ngapi kuna changu hapo nimeweka fance nataka bei ikiwa juu niuze!
 
Back
Top Bottom