Nimefunguliwa kwenye kifungo cha hofu na mashaka

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,278
6,672
Habarini wana JF, Tar.17.05.2002 Nilifiwa na mchumba wangu kipenzi. Toka wakati huo mpaka kufikia 05/06/2011 Nimekuwa mwoga wa kwenda kucheki Afya. Mwaka jana nilikimbia majibu yangu pale kituo cha Afya tabata shule. Mchumba wangu alikufa kwa TB lakini sikuamini kabisa. Muda mfupi uliopita nilikwenda kupima katika hospitali moja binafsi. Ni uamuzi ambao sikuupanga kabla, yaani limenijia wazo ghafla, nikaamua liwalo na liwe. NIMEPIMA HIV sijawahi kufanya hivyo hapo kabla katika maisha yangu, Jamani leo nimekuwa mpya ni vizuri kwa wale wenzangu waliobaki nao wakichukua hatua hii. Yaani kwa matokeo yoyote yanavyokuja unajihisi kama umezaliwa upya........... Twendeni jamani.... twendeni tukapime tuondoke kwenye kifungo cha hofu na mashaka.
 
Ubarikiwe sana Mpwa ila inabidi uende pia kwenye kituo kingine kwa ajili ya kuhakikisha, Hongera sana sana
 
Alafu ukute kipindi chote hapo kati kati umekua na mahusiano bila kujali kwamba ungekua mgonjwa ungemwambukiza mwingine!!

Nwy hongera!!!
 
Hongera mpendwa,
Jijengee tabia ya kwenda kupima kila baada ya mda fulani na kama umeishabaatika kupata mchumba mwingine mushauri mwende kucheki afya zenu wote kwa pamoja
 
Hongera rafiki,check up ni muhimu hope utaenda tena baada ya miezi mitatu,otherwise utulie na ucheze salama inapobidi.
 
Habarini wana JF, Tar.17.05.2002 Nilifiwa na mchumba wangu kipenzi. Toka wakati huo mpaka kufikia 05/06/2011 Nimekuwa mwoga wa kwenda kucheki Afya. Mwaka jana nilikimbia majibu yangu pale kituo cha Afya tabata shule. Mchumba wangu alikufa kwa TB lakini sikuamini kabisa. Muda mfupi uliopita nilikwenda kupima katika hospitali moja binafsi. Ni uamuzi ambao sikuupanga kabla, yaani limenijia wazo ghafla, nikaamua liwalo na liwe. NIMEPIMA HIV sijawahi kufanya hivyo hapo kabla katika maisha yangu, Jamani leo nimekuwa mpya ni vizuri kwa wale wenzangu waliobaki nao wakichukua hatua hii. Yaani kwa matokeo yoyote yanavyokuja unajihisi kama umezaliwa upya........... Twendeni jamani.... twendeni tukapime tuondoke kwenye kifungo cha hofu na mashaka.

Hongera mkuu umefanya lisilowezekana hongera sana
 
Hongera mpendwa,
Jijengee tabia ya kwenda kupima kila baada ya mda fulani na kama umeishabaatika kupata mchumba mwingine mushauri mwende kucheki afya zenu wote kwa pamoja
Ahsante, nimepanga siku inayofuata kwenda hospitali nyingine. Mchumba bado lakini sasa nimepata nguvu mpya ya kumtafuta.
 
umefanya uamuzi wa busara sana mkuu...nina amini thread yako itawatia moyo wana JF zaidi kwenda kucheki status zao.
Hakikisha basi status yako haibadiliki ili uzidi kujenga taifa hili
 
yaani ndugu yangu mimi sitakaa nipime naogopa kinoma
Nimegundua kuwa ukipima unakuwa na furaha zaidi kwa matokeo yoyote yale. Nenda tu mkuu usihofu, mimi mara tatu narudia getini na ya nne ndo sikurudi kabisa kuchukua matokeo. Tena sasa hivi simple sana damu wanatoa kwenye kidole!
 
ndugu yangu hayo unayosema ni serious?au kautani?lakini siamini kama nitaweza hata kufika pale getini
 
cdanganyiki! ht nishikiwe bunduki cpimi ng'o.
Nenda ukapime chwechwe utashangaa mwenyewe kwanini ulikuwa unachelewa. Pia utapata ushauri nzuri ambao utakufanya uishi kwa furaha kwani hata kama utakua (+) utashangaa kukuta unapata kampani zaidi ya hii ya JF, utapata marafiki wapya pia utajihisi kama uliezaliwa upya.
 
hongera mkubwa...umefanya jambo la mbolea.....big up sana...mi cjui ntafikia huo uamuz lini...nahic ntazmia mshauri nasaha akianza kuniuliza maswali tu....hahahaaaaaa....:becky:
 
Hapa siwezi kukuongopea yale maswali yanatisha ndugu yangu na usipokuwa jasiri unaweza kujikuta unabadilisha uamuzi wakati uleule wa maswali
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom