Nimefiwa na mtoto jana muhimbili!

Bwana ametoa, na Bwana ametwaa. Jina la Bwana libarikiwe.
Pole sana na Mungu akupe nguvu katika kipindi hiki kigumu.
 
sisi wengine wa MOROGORO hatutaweza kujumuika kwenye msiba kimwili lakini kiroho tutakuwa nanyi huko Ukonga. Poleni sana.
 
pole spika..kijana wetu apumzike kwa amani? na juzi si ulifiwa na mama mkwe? nayo pole kaka
 
Habari wana JF,nimefiwa na mtoto jana Muhimbili hospital.
Mazishi ni leo saa7 mchana,msiba upo banana ukonga!


Aisee pole sana; Mungu ailaze roho ya mwanao mpenzi mahali pema peponi! Amina
 
Pole sana sana, Mungu akutie nguvu sana kipindi hiki cha matatizo
 
Pole sana kwa msiba. . .wewe na familia yako yote.
Mungu awajalie faraja.
 
Pole sna kwa kufiwa na mtoto wako naomba uwe na subira husani kipindi iki na muombe muumba na ukubali kuwa hakuna mwengine zaidi yake kwa shida na raha hakika atakusikia na kukufariji
 
Nazidi kutoa shukrani zangu kwa wana JF wote wanaozidi kunitumia salaam za rambirambi.
Inshaallah ALLAH atawalipa kila mtu kwa wakati wake inshaallah.
 
Back
Top Bottom