Mzee Kipara
Member
- Jan 3, 2011
- 83
- 43
Kiongozi hapendwi kwa kuitikia salamu, anapendwa kwa matendo anayoyafanya katika kuendeleza nchi. Mimi nilitegemea furaha yako ihusiane na jinsi ulivyomuona akishughulukia issues zinazolenga katika ustawi wa nchi, siyo kuitikia salamu. Upenzi wa bila sababu alionyeshwa Kikwete mnaona alipotufikisha. Inabidi tuweke wazi kwamba viongozi wetu tutawapenda kwa jitihada zao katika kuleta maendeleo, si vinginevyo, na inabidi viongozi wote akiwemo Slaa walitambue hilo, maanaake mnapoanza kumpamba mtu eti kwa sababu ameitikia salamu tu mimi naanza kupata wasiwasi.