Nimefanikiwa Kupunguza Siku za Kuishi tena

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,180
85,339
Habari wana Jukwaa,
Poleni kwa makali ya mgao wa umeme ambao tunaambiwa haupo japo upo. Leo tarehe 30.03.2012 ni siku yangu nyingine ya kupunuza siku za kuishi ya Birthday, namshukuru sana MUNGU aliniweka hai hadi leo hii, nimeona mengi na amenipitisha katika mengi, magonjwa, shida na taabu kisha akaniinua toka uflame mmoja kwenda mwingine, Hakika namshukuru sana yeye Muumba.

Ni wengi walitamani sana waione leo, wasiione, walitamani wawe na afya njema lakini wako vitandani je mimi nimempa nini MUNGU hadi niione siku hii? Ni jambo la kushukuru sana

Nawaombeni tusherehekee pamoja kwa amani. Nawatakia weekend njema kwa kuzaliwa mtoto Elli
 
aaaaaaaaaaagr gharibu! yaani nilijua umekunywa sumu kama smile kumbe ni siku ya kuja matatizoni ndio inakuzuzua...

heri ya kuzaliwa..
 
Hahahaa Mpwa nimecheka hadi basi, kimsingi tangu siku ile ulipozaliwa ndio kifo kilianza kukunyemelea, hakuna tena siku ya kuzaliwa bali ya kufa, kwahio kusema birthday ni mazoea tu, haya asante sana sana Mpwa.
aaaaaaaaaaagr gharibu! yaani nilijua umekunywa sumu kama smile kumbe ni siku ya kuja matatizoni ndio inakuzuzua...

heri ya kuzaliwa..
 
Nitafute mkuu - Nina Nepi Dazeni 2 natumaini zitakuhusu! BY the way Happy B/DAY 2U!
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom