Nimechoshwa na maisha ya upweke

Sikuhizi mambo ni tofauti kabisa, ktk juhudi za serikali kupunguza tatizo la maambukizi ya VVU, Mtu alie athirika anaweza kumuoa/kuolewa na mtu mzima ambaye hana hata maambukizi, muhimu ni kwamba ukibahatika kumpata mwenza mwende kwa mshauri ambaye atawaeleza jinsi yakuisha na kushirikiana kimapenzi pasipo kupeana maambukizi, sijaanza na POLE kwasababu ntakuwa kama nakukatisha tamaa wakati wewe huna tofauti na mtu mwingine yeyote...
 
Waungwana naomba msaada wenu, naishi na virusi vya ukimwi yapata miaka 7 sasa,mwenzi wangu ametangulia mbele za haki miaka 4 iliyopita.
Nahitaji kuowa tena, nitampataje atakaye nikubali na hali yangu?

mzelokotwa kwel we muungwana, utajaaliwa tu hata usihofu kama n kwel
 
Back
Top Bottom