Nimechoka kusubiri ajira za walimu

Uhaba wa walimu hautaisha Tanzania hii,hata wakitoa ajira haitazidi 40% kwa watakaoreport kwenye vituo vya kazi,watu wengi waneajiriwa private schools na kwenye taasis binafsi na hivi MNA mpango wa kuwatupa pembezoni mwa nchi kwenye mazingira mabovu na mshahara mdogo sijui tu hii sekta ya elimu itaendelea lini...na hata wakaoenda watakuwa washasahau walichofundishwa.



ONYO: Serikali muache kulalamika kuhusu uhaba wa walimu maana ni unafki
 
Kusubiri miezi michache tu unalalama! Inaonekana hujui kama kuna waliowahi kusubiri ajira hiyo kwa miaka sita (6)!

Hii ilikuwa mwaka 1996 serkali ilipokuwa bunkrupt hivyo kutokuwa nauwezo wa kuajiri watumishi wapya na kuwalipa mishahara hadi ilipoanza tena kuajiri mwaka 2002 baada ya hali ya kiuchumi kutengamaa.

Ushauri: Usikae tu, tafuta namna yoyote ya kujishughulisha. Kwa kufanya hivyo si ajabu ajira zitakapo toka ukawa huzitamani tena maana unaweza kuwa ktk shughuli inayokulipa vizuri zaidi.
 
Inaonekana hujui kama kuna waliowahi kusubiri ajira hiyo kwa miaka sita (6)!

Hii ilikuwa mwaka 1996 serkali ilipokuwa bunkrupt hivyo kutokuwa nauwezo wa kuajiri watumishi wapya na kuwalipa mishahara hadi ilipoanza tena kuajiri mwaka 2002 baada ya hali ya kiuchumi kutengamaa.

Una uhakika? Wazoefu mtupe uhakika kuhusu hili kama ni kweli liliwahi kutokea(miaka 6 !!!??)
 
Tumechoka, watakapoamua kutoa watatoa, ila wasiwe wanadanganya watanzania.
 
heri yako ww kuliko yule aso na uhakika wa kuajiriwa had akatafte tulia utaajiriwa tu harakaharaka haina baraka
 
G. Simbachawene kesho 31.05.2
016 ni mwisho wa ahadi yako maana mwezi mei ndio huo unaisha.kama umeshinda omba radhi kwa usumbufu ulijitokeza kwa walimu tarajali
 
Back
Top Bottom