Nimechoka kusubiri ajira za walimu

mimi ni kama tomaso kwa hatua iliyofikia labda ingetolewa press release ningeamini lakin majibu ya kisiasa ni kusema tu
 
SERIKALI inatarajia kumwaga ajira kwa askari na walimu katika mwaka ujao wa fedha huku ikisisitiza walimu kwamba watakaokaidi kwenda kuripoti kwenye mikoa ya pembezoni na baadaye kuamua kuomba tena, hawatapewa nafasi kama ambavyo imekuwa ikifanya.

Taarifa juu ya ajira hizo, zilitolewa jana bungeni kwa nyakati tofauti na mawaziri tofauti wenye dhamana na taaluma husika.

Akiwasilisha Makadirio ya Mapato ya Matumizi ya Wizara yake kwa mwaka 2016/17 kuhusu ajira za askari, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga alisema wataajiriwa askari wapya 3,700 katika mwaka wa fedha 2016/17.

Kwa upande wa ajira kwa walimu 35,411 wa shule za msingi na sekondari, Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jaffo alitoa taarifa hiyo kwenye kipindi cha maswali na majibu.

Ajira polisi Waziri Kitwanga alisema mbali ya kuajiri askari hao, pia watawapandisha vyeo askari 7,140, wakaguzi 1,325 na maofisa 991.

Alisema katika mwaka 2015/16, jumla ya askari polisi wapya 3,882 waliajiriwa, na askari wakaguzi na maofisa 4,065 wa vyeo mbalimbali walipandishwa vyeo kwa kufuata utaratibu wa ajira.

“Aidha, serikali imeendelea kuhuisha viwango vya mishahara na posho mbalimbali, ikiwemo posho ya chakula ambayo iliongezwa kutoka Sh 180,000 hadi kufikia Sh 300,000 kwa mwezi,” alieleza Waziri Kitwanga.

Alisema katika mwaka ujao wa fedha, Jeshi la Polisi litaongeza umakini katika kusimamia nidhamu kwa askari wake kwa kufanya uchambuzi wa kina (vetting) kwa kuchukua vijana waliomaliza mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), wanaoomba kujiunga na Jeshi la Polisi ili kuwa na askari wenye nidhamu na moyo wa dhati wa kulitumikia Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wa Jeshi la Magereza, alisema linatarajia kutoa mafunzo kwa maofisa na askari 4,975 katika ngazi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na yale ya Taaluma ya Urekebishaji.

Alisema ili kukabiliana na changamoto ya uchache wa miundombinu ya makazi kwa askari Polisi, serikali kupitia mkopo kutoka Serikali ya China inakusudia kujenga nyumba 4,136 chini ya usimamizi wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi.

Akizungumzia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, alisema jeshi hilo linahitaji vituo 152 Tanzania Bara, lakini kwa sasa lina vituo 57 na kati ya hivyo, 38 vipo katika miji na 19 katika viwanja vya ndege. Alisema huo ni upungufu wa vituo 95 hali inayosababisha maeneo mengi kukosa huduma za zimamoto na uokoaji.

Inategemea kujenga kituo kimoja cha zimamoto na uokoaji katika eneo la Kigamboni katika Jiji la Dar es Salaam na kuendelea na ujenzi wa Jengo la Makao Makuu Tazara - Mchicha, Dar es Salaam.

Aidha, alisema Jeshi la Polisi litaendelea kupambana na makosa yanayovuka mipaka hususani ugaidi, uharamia, biashara ya dawa za kulevya, biashara haramu ya kusafirisha binadamu, wizi wa vyombo vya moto hususani magari, wizi wa kutumia mitandao ya Tehama, bidhaa bandia, na biashara haramu ya silaha na uchafuzi wa mazingira.

Walimu kuajiriwa Kuhusu walimu 35,411 watakaoajiriwa, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tamisemi, Selemani Jaffo alisema uamuzi wa kuwaajiri umetokana na serikali kupokea maombi mengi ya kazi kwa walimu ambao mwaka jana hawakuripoti katika vituo walivyopangiwa pembezoni mwa mji kwa kutegemea kuajiriwa na shule binafsi, lakini hawakufanikiwa.

Jaffo alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali (CUF) aliyetaka kufahamu serikali inafanya nini kwa walimu waliopangiwa kwenda mikoa ya pembezoni na Lindi na kwingineko, lakini wakakataa kuripoti.

Alikiri kuwa walimu wengi hawakuripoti katika mikoa ya pembezoni na si Lindi pekee, bali mingine ikiwemo Katavi, Kigoma. Hata hivyo alisema, pamoja na kwamba mwaka huu wanaajiri walimu 35,411 , ambaye hataripoti katika mikoa hiyo na kuishia mijini pekee, hawataajiriwa tena serikalini kama ambavyo wamekuwa wakifanya kwa kuomba tena baada ya kukosa katika shule binafsi.

Awali, Katika swali ya msingi, Mbunge wa Viti Maalumu, LucyMlowe (Chadema) alitaka kufahamu mpango wa serikali uliopo wa kukabiliana na changamoto za uchache wa walimu kwenye shule za msingi na sekondari.

Naibu waziri alisema, ili kuboresha elimu nchini kwa kupunguza msongamano wa wanafunzi madarasani serikali imeendelea kutenga bajeti kila mwaka kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za msingi na sekondari.


Habari Leo
 
Sijakusomaa Mkuu!....

Sasa uandishi wangu unaingiliana vipii na kufeli kwa wanafunzi!?...
Au unataka kuniambia kuwa kwa namna nilinanyoandika naonekana kama mwalimu asiye na maarifaa amaa!?........

Maana bado sijaona kosa nililofanya katika hoja yangu ambayo inaonesha kuwa sina uwezo wa kuwafanya wanafunzi kufauluu!.......

Sometimes tunahitaji jicho la TATU kabla ya kuchangia madaa!......

Sent from my TECNO-Y4 using JamiiForums mobile app
....huu sio aina ya uandishi unaotakiwa humu,peleka facebuk wataluelewaaa zaidiii!!
 
Mwezi wa tano ndo unaisha hivi xo ondoeni shaka maana watatangaza mwezi ujao na mapema mwezi wa 7 kazi itaanza.

Serikali yetu inaona mwezi wa 07 ni mapema bado ila msijali maana neno mapema ni dhana telezi.
 
Kwel walimu wengi ni vilaza....yaan uneshindwa ata kuuza machungwa unalialia tu ...
Biashara inahitaji plan (short term na long term) sio sawa na wanaouza miili yao ambao hawahitaji mtaji zaid ya kusimama barabarani.

Ukiagiza mzigo wa machungwa kabla haujafika ajira zikatangazwa utaenda nao kureport au utampa nani ambae ulishampanga kwa hilo?

Mwalimu kakutoa ujinga na bado atakufundishia watoto wako alafu unaandika pumba.....

Labda uongelee biashara ya mtu mzembezembe ila sio msomi.
 
Biashara inahitaji plan (short term na long term sio sawa na wanaouza miili yao ambao hawahitaji mtaji zaid ya kusimama barabarani.

Ukiagiza mzigo wa machungwa kabla haujafika ajira zikatangazwa utaenda nao kureport au utampa nani ambae ulishampanga kwa hilo?

Mwalimu kakutoa ujinga na bado atakufundishia watoto wako alafu unaandika pumba.....

Labda uongelee biashara ya mtu mzembezembe ila sio msomi.
Samahani mwalimu mziray.......
 
Subiri wewe kuajiri maelfu ya watu sio mchezo lazima serikali ipangilie mambo yake, tena miaka michache ijayo hakutakuwa na mass employment kama saiv, ila kwa waalim wa sayansi na masomo maalumu tu,
 
Kwel walimu wengi ni vilaza....yaan uneshindwa ata kuuza machungwa unalialia tu ...
Acha kutukana walimu wewe ulifundishwa na nani? Na kama ni walimu haohao huoni kuwa wewe ni zao la hao unaowaita vilaza? Na kama ni zao la unaowaita vilaza, je wewe sio kilaza??? Je kibaya huzaa chema? Mawazo yako jitahidi yawe na maana sio kuandika kufurahisha umma,

*Ulienda shule hujui kufunga hata vishikizo vya shati lako, mwalim alikuelekeza bila hiana.
*hukujua kusoma wala kuandika, sasa unatumia mbinu na ujuzi waliokupa kurudisha fadhila za matusi?
*mwalimu alikufundisha mema na mabaya, nidham pia utii, leo umejua zaidi hadi unaandika hivi?

Hata kama unaamini walimu hawana maendeleo lakini jua wamewekeza mda wao kuifundisha jamii ikiwemo wewe, watoto wako, na ndugu zako.
MHESHIM SANA ALIEKUPA MAARIFA.
 
Subiri wewe kuajiri maelfu ya watu sio mchezo lazima serikali ipangilie mambo yake, tena miaka michache ijayo hakutakuwa na mass employment kama saiv, ila kwa waalim wa sayansi na masomo maalumu tu,
Kwa taarifa yakoo sasaa!...
Suala la ajira tena za ualimu ni process isiyozuilika,Kila mwaka walimu wanastaafu na nchi yetu, idadi ya wanafunzi wapya wanaoandikishwa inaongezeka kila mwaka!...
Kwa logic hiyo tuu...unafikiri kuna atakaye zuia kuajiri waalimu wapya!?..

Acha zako kabisa!.

Na kuhusu kusubiri!...Ajira zetu tayari bajeti yake iliishatengwa bajeti iliyopita yaana 2015-2016...
Wanahitaji muda mrefu kiasi gani kujipanga nikikuuliza fedha iliyopangwa 2015-2016 kwa ajili ya ajira IMEKWENDA WAPI unaweza kujibu!?..(nafikiri hujui)...
Tunaolalamika kuchokaa ni kweli watu wamechoka kusubir!maana kawaida ajira za ualimu hutoka January hadi April! Unafikiri Watu kulalamika kuchoka kusubiri #hawajielewi!?
Hakuna anayefurahia jambo hilii maana wanafunzi wanatuhitaji tukawasaidie(na/wakati shule nyingi zinauhaba wa walimu) lakin mamlaka husika wanaingiza usiasa ndani ya jambo muhimu kama hili na bado MTU unasimama na kuwatetea!..

 
Kwa taarifa yakoo sasaa!...
Suala la ajira tena za ualimu ni process isiyozuilika,Kila mwaka walimu wanastaafu na nchi yetu, idadi ya wanafunzi wapya wanaoandikishwa inaongezeka kila mwaka!...
Kwa logic hiyo tuu...unafikiri kuna atakaye zuia kuajiri waalimu wapya!?..

Acha zako kabisa!.

Na kuhusu kusubiri!...Ajira zetu tayari bajeti yake iliishatengwa bajeti iliyopita yaana 2015-2016...
Wanahitaji muda mrefu kiasi gani kujipanga nikikuuliza fedha iliyopangwa 2015-2016 kwa ajili ya ajira unaweza kujibu!?..(nafikiri hujui)...
Tunaolalamika kuchokaa ni kweli watu wamechoka kusubir!maana kawaida ajira za ualimu hutoka January hadi April! Unafikiri Watu kulalamika kuchoka kusubiri #hawajielewi!?
Hakuna anayefurahia jambo hilii maana wanafunzi wanatuhitaji tukawasaidie(na/wakati shule nyingi zinauhaba wa walimu) lakin mamlaka husika wanaingiza usiasa ndani ya jambo muhimu kama hili na bado MTU unasimama na kuwatetea!..

Kama unadai bajeti imetengwa na hawajaita kazini, ni sahihi ulaumu, lakini kama bado na wenyewe wanapangilia mipango ikae njema haihitaji lawama maana hili taifa letu sote, nadhani rais na timu yake wana nia nzuri kwa taifa letu tusubiri july ifike kitu kitaitika tu,
 
Back
Top Bottom