Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 10,114
- 35,121
UFAFANUZI.
1/Kama wewe ni mwalimu ujue una bahati kubwa sana ya kuja kuajiriwa na serikali. Wahitimu wa fani nyingine hawana hiyo bahati.
2/Ni jambo la kweli na uhakika kuwa serikali itaajiri walimu, Tatizo ni Lini wataajiri, wangapi wataajiriwa, wapi utapangiwa na utalipwa nini?
3/Upo uwezekano wa baadhi ya walimu wanaweza wasiajiriwe na serikali kama sio mwaka huu basi miaka michache ijayo. Kwanini? Serikali kwa sasa inaona watumishi wa umma ni wengi, ufanisi ni mdogo sana, gharama za kuwalipa ni kubwa sana. Kifupi kabisa serikali inaona wingi wa watumishi wa umma ni MZIGO na JIPU.
4/Mpaka sasa Serikali imeshasema kuwa haitawaajiri wahitimu wote wa Udaktari wa Binadamu. Kati ya madaktari zaidi ya 1000 waliohitimu Mafunzo ya Vitendo hivi karibuni, ni 400 tu ndio watakao bahatika kuajiriwa na serikali mwaka huu. Kwanini? Serikali haina pesa za kuwalipa wote.
Sasa jiulize suala la kuajiri walimu Elfu 40 kwa mkupuo mmoja kama linawezekana kirahisi rahisi mwaka huu?
5/Serikali imekuwa na vipaumbele vingi sana, na inataka vyote vitimizwe kwa wakati mmoja na hapo hapo mtizamo wa Rais kwa sasa ni kupunguza matumizi ya serikali na hapo hapo kukusanya mapato zaidi ili kujenga miundombinu na kununulia vifaa, na sio kuzifanyia matumizi ya kuwalipa watu Posho, mishahara mikubwa nk.
Katika hali hiyo, tegemea kabisa suala la kuajiri walimu litakuwa sio kipaumbele chake.
NI VYEMA UKIJIANDAA PIA KUISOMA NAMBA!!