Nimechoka kunyongwa usiku wa manane, tafadhali msaada wa haraka

Pole sana ndugu. Ni vyema ukatafuta KANISA linalohubiri Wokovu na kuamini miujiza ya Yesu Kristo AU MCHUNGAJI hili akushauri na kukufanyia MAOMBI bila shaka utapata msaada.
 
kama ni jini kuna dawa katika biblia, ambayo Tobia alielezwa na malaika kuitumia kumtibia mkewe mtarajiwa-Sara.

Tobiti 6: 3-8. Uje utupe mrejesho
 
Ndugu yangu sikiliza kwa makini usiende eti upate chanzo cha tatizo lako acha kupiga Ramli, kuagalia nyota kupiga ramli, faraki wote hao ni adui wa Mungu Baba!!! Watumishi wa Mungu aliye hai wapo wengi tuu hapo Dar, nenda makanisa ya kiroho uombewe upate uponyaji!!!! Usidharau makanisa ya Mungu aliye hai ya kiroho, nguvu ya Mungu kwa uwezo wa Bwana Yesu ipo tuu!!!! Majini na mapepo hayasimami kwa Yesu hiyo ni cha mtoto yapo mambo makubwa utajifunza utujua mengi na kuyafanyia kazi!!! Unapote za muda kutookoka ndugu yangu ili uufaidi uzuri wa Yesu, ubarikiwe!!!!


Aliyekuambia anakwenda kupiga ramli ni nani? Wewe unasumbuliwa na tamaa yako ya pesa. Nani asiyejua Makanisa mnayojiita ya Kiroho mnatumia nguvu gani. Siku hizi watu wameshawashtukia na hayo mauchawi yenu mnayonunua Nigeria. Apolonary, wewe ni Mkatoliki na utaponea kwenye Ukatoliki. Usikubali kudanganywa na hao wanaojiita makanisa ya Kiroho. Yangekuwa ya Kiroho wasingetapeli viwanja vya watu, wasingeiiba wake za watu (efatha), wasingedanganya waumini kutoa sadaka ya dhahabu walizovyaa (kakobe) na mambo mengine ya aibu wanayofanya. Nedha kwenye Dhehebu lako utasaidiwa.
 
NAOMBA KUTOA USHUHUDA WA KWELI:
Nilipokuwa kidato cha Nne nilikutana na hali ya kutisha , Kila ilipofika usiku nilikuwa nakutana na mambo ya kutisha sana, Kulikuwa na kundi la watu linanifuata na kutaka kunichukua ninapokuwa nimelala, ilikuwa ni exprience mbaya sana kwangu.Iliniathiri sana maendeleo yangu katika masomo kwa kuwa nilikuwa nahakikisha kuwa silali Usiku ili kuepukana na hizo ndoto.Matokeo yake nilikuwa nalala mchana darasani kila siku .

Mzee wangu alinipeleka Kwa Sheikh mmoja maarufu pale Tanga haikufaa kitu, Baadaye tena Visiwani kwa sheikh mwingine tena, haikufaa kitu na Mwisho kwa Yule Sheikh Tapeli wa Magomeni Naye alikula hela zetu bila mafanikio. Nililala na Biblia, Rozari na Mifupa ya Kiti moto, nimesali sana rosari haikusaidia kitu.Nilidhoofu kwa kukosa Usingizi muda mrefu. Siku moja katika matembezi yangu kule Kurasini nilikutana na kundi la watu linaelekea sehemu, na mimi nilitaka kujua kuna nini nikalifuata lile kundi. Kufika huko nikakuta ni Ibada ya Askofu Gamanywa nikakaa kusikiliza, Nilivutiwa sana na ile ibada kwa kuwa mimi nilikuwa Mkatoliki nikatamani kurudi tena. Kumbuka lile tatizo langu lilikuwa halijaisha na usiku nilikuwa silali.

Nikachukua ratiba ya ile Ibada na nikawa nahudhuria pale. Nikahudhuria kama mara 5 kabla ya kuamua kuokoka. Nikaokoka . Baada ya Hapo hilo Tatizo limekuwa Historia. Lakini nina mambo mengi ambayo hata nikiyaeleza humu ndani ni vigumu mtu kuelewa na kuyaamini. Tokea hapo mpaka sasa huyu Yesu amekuwa LIVE Katika maisha yangu.
 
Ndugu pole sana kwa yanayokukumba, wapo wengi ambao wameteseka kwa namna hiyo ila walipochukua hatua ya kubadili life style ya maisha yao wamewekwa huru kabisa.
Piga moyo konde chukua hatua zifuatazo na kwa kumaanisha ndani ya moyo wako utawekwa huru kabisa.

1.Amini katika Jina la YESU, Yohana 1:12, tubu dhambi zako zote popote pale ulipomkosea Mungu yeye ni mwaminifu atakusamehe kabisa, Isaya 1:18, Isaya 43:25, Zab 103:3,11,12, Mkaribishe ROHO MTAKATIFU awe ndani yako na kuyaongoza maisha yako, Wagalatia 4: 6,

2. Kwa kumwamini Bwana YESU, kutubu dhambi zako zote, na kumwalika Roho Mtakatifu kuwa ndani yako, unayo mamlaka na nguvu za Mungu kushinda ulimwengu wote wa giza. Muda wowote utakapo jisikia hiyo hali tumia mamlaka ya JINA LA YESU kukemea hizo nguvu za giza wala hazitakuwa na uwezo juu yako. LUKA 10:19, MARKO 16:17-18,

3. Jiwekee utaratibu wa kusoma na kutafakari neno la MUNGU ndani ya Moyo wako popote pale utakapokuwepo. Kumbuka ibilisi atakuletea hofu ya kukunyonga kama kawaida yake, chukua hatua ya kukemea hiyo roho ya hofu, na mtafakari Mungu na uweza wake katika Jina la YESU badala ya kuwaza hizo hofu za ibilisi. Wakolosai 3: 1-2.

4. Ukifanya maombi usifanye maombi legelege, fanya maombi ya vita ya kujikomboa kutoka katika utawala wa shetani, tumia silaha zote za UFALME WA MUNGU kumpinga na kumpiga shetani ili asikufuatilie. Uhuru haupatikani kilegelege ni kwa vita ndugu. 2-Wakorintho10: 4-5

5. Acha dhambi yoyote ile inayokuzinga ambayo ibilisi anaweza kuitumia kama njia ya kuendelea kukushambulia. Kumbuka MUNGU ni Mtakatifu na anawatetea wale wote wanaoishi katika njia zake. Wagalatia 5:20-21.

6. Hakikisha unahudhuria vipindi vya maombi na kujifunza neno la Mungu katika kanisa linalohubiri Injili ya kweli na kuamini katika karama zote za ROHO MTAKATIFU na si ubabaishaji.

Ndugu, Bwana Yesu akusaidie na kukuweka huru kabisa.

Huu ndio msaada wako haaasa""Mpokee YESU awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako.utapata uhuru
mbali na hayo mateso yote.usiendelee kutubu na kuomba kwa namna ya desturi na mzoea tu.
Na kama uko tayari kupokea msaada wa Mungu fuatisha sala hii
"MUNGU BABA,NATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA KUZIACHA,NAOMBA ULIFUTE
JINA LANGU KATIKA VITABU VYA HUKUMU NA KULIANDIKA KTK KITABU CHA UZIMA MBINGUNI,
NIPE UWEZO WA KUSHINDA DHAMBI.KTK JINA LA YESU AMEEN"
Kama umefuatisha sala hii kwa dhati utasaidika,kisha tafuta kanisa linalohubiri wokovu fuatilia
mafundisho.
 
shida yako kubwa itakuwa jinsi unavyolala. jaribu kubadilisha staili na chumba chako kiwe na hewa ya oxygen ya kutosha. ondoa hofu nawe utakuwa salama na utapata usingizi bila kunyongwa.
 
Ndugu yangu Pole Sana,Mungu ndio Mlinzi zaidi ya Walinzi wengine.Mtegemee Yeye Atakulinda na hayo mauza uza hutoyasikia tena,na Elewa Kutokukuonyesha au kukusaidia ulipoanza Kusali pengine anaangalia na Kukupima Imani Yako.Keep On Pray Ngugu Usikate Tamaa.
 
Kuomba sio ishu,ishu ni je waombaje? Isije kuwa unatoka baa ukiwa chakari ndio unaomba...ila nakushauri fanya mfungo wa dhati kwa mwezi mmoja,narudia tena kwa dhati na maombi ya nguvu..sidhani kama shetani atasimama kwa hapo.
 
Kuomba sio ishu,ishu ni je waombaje? Isije kuwa unatoka baa ukiwa chakari ndio unaomba...ila nakushauri fanya mfungo wa dhati kwa mwezi mmoja,narudia tena kwa dhati na maombi ya nguvu..sidhani kama shetani atasimama kwa hapo.

.
Kufunga kwa siku nyingi sidhani kama inawezakuondoa mapepo. Kwa hilo kuna probability, ama uyaondoe au uyaongeze. Kuna jambo moja tu kwa mtu kuweza kujiweka free nje kabisa na kila aina ya pepo. Ni kuyasalimisha maisha ya mhusika ndani ya Bwana Yesu. Kwa Bwana Yesu hakuna hakuna kilichowahi kushindikana. Kuwa ndani ya Yesu ni pamoja na kuachilia yoote ya kiuovu katika maisha yako. Kuungama kwa yeyote uliyemtendea kwa hila, kuondoa maagano yote na kuzimu ikiwa ni pamoja na kuondoa hirizi zote kama zipo katika mazingira yanayokuhusu, kurejesha mali zote za wizi kwa wenyewe kama zipo na wenyewe wapo na kujitenga na kila aina/makundi ya ubaya. Hapo nafsi yako itakapokuwa kwa haki haishitakiwi kwa ubaya wowote hapo una ujasiri na mamlaka juu ya kila pepo wa sheitwan. Hayo ndiyo maisha ya ushuhuda wa ukiri kwa Yesu wa kweli. Usijaribu kung'ang'ana kufunga siku arobaini kumshinda shetani ilhali una vyake utaumbuka kweli. Hapa ndipo watu wanapoingiwa na pepo mbaya kuliko wote na kuwa wakaidi kupita maelezo wakifikiri wapo na Roho wa Mungu kumbe ni yule adui amewajaa tele.
Tukumbuke kuwa kama matendo ya sheria kama kufunga, kutawadha, kushika siku nk yangeliweza kumshinda shetani na mapepo yake kusingelikuwa na sababu ya Yesu kuja. Hivyo Yesu amekuja na kumwamini yeye yatosha kumshinda shetani. Hivyo tu!!
.
 
Labda unasali juu juu tu, huamini kwamba
sala zako zitakusaidia. maana kila kitu (ikija kwenye sala ) unasema umefanya.
 
Tatizo langu si la kitabibu bali ni la kiimani zaid kwan kama ingekuwa ni maradh ya moyo ishara zingekuwa nyingine mimi ndio mwenye tatizo na hakuna awezaye kuisemea nafsi yangu kwani iko ndan yangu na nashuhudia ukwel kwamba si ugonjwa ila ni mambo ya magician,s
 
Apolinary...sikia! Sala ni muhimu sana kwetu binadamu kwani ni chakula cha roho. Ila pia kuna kitu kinaitwa mizimu nayo ni hatari na lazima izingatiwe. Kama wazazi wako wamefariki uliza ndugu waliobaki ufanyeje ili utekeleze matakwa yao la sivyo utaishia kuhama hama kila kukicha! Kingine, je uliwahi kumdhulumu mtu mali yake? Nakuuliza hivi manake kuna yanki mtaani alijiua miaka ya nyuma baada kuteswa kijinsia kila siku. Sikutishi ila huyu yanki alikuwa anajivinjari na mke wa mtu then jamaa alipogundua akamuonya lakini yule marehemu alinogewa na vya bure. Kwa hiyo mwenye mali akafanya yake ya jadi na yule yanki akaanza kuweweseka usiku kila akienda kulala. Jamaa akawa anapata mateso ya kila aina mpaka mwishoni akawa anafilwa kabisa akiamka asubuhi ****** una muuma na anakuta kinyesi kitandani, jamaa akachoka na mateso akahamua atangulie mbele ya haki na kuacha barua kwa nini alichukua ile hatua. Kwa hiyo bwana kama umemlalia mtu tafadhali omba msamaha wakati muda bado upo!

Kwa taarifa yako mizimu ni department ya shetani, ni mapepo au mashetani ambayo yanafuata familia/koo za wanadamu. Mizimu/mapepo hayo yanaishi yakifuata koo. Ikitokea mtu amekufa kwenu yanawatokea wanandugu usiku yakiwa yamevaa sura za marehemu.

Mapepo yana uwezo wa kuvaa maumbo mbalimbali, yanafanya hivyo kuwadanganya wanadamu kuwa watu waliokufa wanakuja usiku. Na mapepo haya yanatoa demands kwa familia either kuchinja kuku au kufanya rituals ambazo ni kinyume kabisa na maagizo ya Mungu.

The ultimate goal ya kufanya hivi ni ili kuwafanya wanadamu wakiuke maagizo ya Mungu na mwisho wa siku waende Jehanum siku ya hukumu.

Hivyo epuka kabisa ibada za mizimu ni machukizo kabisa mbele za Mungu.

Kinachomsibu ndugu yetu si chakula cha usiku wala nini, anatakiwa afahamu kuwa ndoto ni bayana, Biblia imewaeleza watu wengi sana ambao waliota ndoto na ikawa true, Yusuph, Elimelek, Daniel, Yakobo, mfalme Nebukadneza, n.k wote waliota ndoto na ikawa true.

Tambua kuwa uchawi upo na wachawi wapo, na usiku ndio wakati wao wa kufanya kazi za kichawi, kama kukalia watu, kunyonga watu, kulisha watu vyakula vya kichawi, n.k.

Dawa ya haya yote ni kumpa Yesu maisha yako kwa kutubu dhambi zako na kumuomba akae ndani yako. Kitakachotokea ni kuwa utakuwa na ulinzi wakati wote, wachawi hawataweza tena kufanya makao kwenye maisha yako. Utaanza kuota ndoto za ushindi, na yawezekana ukaota unawachapa watu waliokuja kwako usiku.

Wewe ni roho, hivyo unapolala usiku roho yako hailali, inaona lakini wewe unadhani ni ndoto. Wachawi wanakuja wakiwa katika roho na roho yako inawaona coz mpo kwenye same wavelength, na wanaofanya hivyo unawafahamu na ndio maana wanavaa maumbo tofauti ili usiwafahamu.

Ushauri wangu, kama upo Dar nenda kwa Pastor Gwajima (Viwanja vya Tanganyika Parkers, Kawe) ana ufunuo mkubwa sana wa mambo hayo, utafunguliwa kabisa na utapona kabisa.

Kuna mtu alishawahi kuniambia kuwa huwa anaota nyoka anampigania usiku, wakija watu kumvamia nyoka anawakimbiza, akitumbukia kwenye shimo nyoka anajiviringisha mwilini mwake na kumtoa. Nilimwambia kuwa umezindikwa na nguvu za shetani, nikamshauri aende kanisa la watu waliookoka awaeleze hizo ndoto. Baada ya kuwaeleza aliombewa kisha akatapika vitu vya ajabu sana kwa muda mrefu, na akaona kuna kitu kikubwa kimeondoka kichwani mwake, akajiona mwepesi na hakuota tena ndoto za majoka.

Fuata ushauri huu na utashangaa jinsi Yesu alivyo mkuu.
 
Ndugu yangu tubu dhambi zako kwa kumanisha kuziacha (Mithali 28:13). Kwa kuzaliwa wanadamu ni wenye dhambi (Zaburi 51:5). Msamaha a dhambi unapatikana kwa Yesu pekee ambaye hakuwa na dhambi hata moja (Waebrania 4:15; Ayubu 26:2). Kama unakubaliana nami fuatisha sala hii; Mungu Baba mimi ni mwenye dhambi kwa kuzaliwa na kwa kutenda, ninakuomba unisamehe dhambi zangu zote, lifute jina langu katika vitabu vya hukumu na liandike katika kitabu cha uzima. Unipe uwezo wa kushinda dhambi kama wewe ulivyoshinda hapa duniani. Asante kwa kuniokoa na kunipa uwezo wa kushinda dhambi katika Jina la Yesu, Amen. Kwa sala hii hakuna atakayekukaba tena na utafute mtu aliyeokoka akufundishe kuukulia wokovu.
 
Dah mi napita tu jamani, nimekumbuka enzi zile miaka ya 80 huko kijijini kwetu mdogo wangu alikuwa anachapwa viboko usiku kucha na mtu haonekani na purukushani nyiiingi usiku mwingi.
Aaaaah lakini kule ni jino kwa jino tu kuna wachawi na waganga pia, kama vipi njoo nikupeleke ukirudi utamuona live anaefanya mambo hayo na kumkamata, tayarisha nauli tu na labda zawadi ya shati la mtumba kule waganga c wasanii kama wa town, anakutibu kwanza ukipona ndo unajisachi mwenyewe umpe ngapi kama shukrani.
Mi naamini sana dini ila kuna sehemu tusidanganyane dini hua inachemka hasa kama huna imani ya kivileee !
 
Dah mi napita tu jamani, nimekumbuka enzi zile miaka ya 80 huko kijijini kwetu mdogo wangu alikuwa anachapwa viboko usiku kucha na mtu haonekani na purukushani nyiiingi usiku mwingi.
Aaaaah lakini kule ni jino kwa jino tu kuna wachawi na waganga pia, kama vipi njoo nikupeleke ukirudi utamuona live anaefanya mambo hayo na kumkamata, tayarisha nauli tu na labda zawadi ya shati la mtumba kule waganga c wasanii kama wa town, anakutibu kwanza ukipona ndo unajisachi mwenyewe umpe ngapi kama shukrani.
Mi naamini sana dini ila kuna sehemu tusidanganyane dini hua inachemka hasa kama huna imani ya kivileee !

Dini ni dini na Yesu ni Yesu. Tunamzungumza Yesu na sio dini. Dini ni utaratibu wa kibinadamu tu ndio maana shetani haogopi dini, anamuogopa Yesu.

Ushauri wangu ni kuwa achana na waganga, ni moja ya departments za shetani. Kwa kufanya hayo anayoyafanya anafanya kinyume na maagizo ya Mungu na siku ya mwisho atahukumiwa.

Waganga wa kienyeji, wanaoagua na kupiga ramli ni maagents wa shetani, wanatumia mashetani ya uaguzi ili kuwadanganya wanadamu waingie mikataba na shetani. Na ndio maana unatakiwa utoe kafara, kuku, mbuzi, mkono wa Albino, n.k. Hizo ni ibada za kishetani ambazo Mungu amezikataza.

Chagua moja, kwenda kwa Yesu au kwa waganga wa kienyeji ambao wanatumia nguvu za giza na wana mawasiliano na kuzimu. Nakushauri uchague kwenda kwa Yesu, ana watumishi wake hapa duniani, tafuta watu wanaoutangaza wokovu, you will never be the same.
 
Back
Top Bottom