Nimechoka kunyongwa usiku wa manane, tafadhali msaada wa haraka

pole ndugu ila jiulize kama hujawahi nyonga mtu kwa maneno au vitendo na pia kama hujawahi sababisha utoaji mimba kama ndivo basi malipizi ndio hayo kwa sasa yanakuandama
 
a. Inawezekana ni ndoto mbaya tu, na shughuli nyingi

b. Soma Quran kabla ya kulala hakikisha unaoga kabla ya kusoma..

c. Mtafute sheikh akusomea dua, huenda Allah akakusaidia

d. Hakikisha hujadhulumu mali za watu..
 
a. Inawezekana ni ndoto mbaya tu, na shughuli nyingi

b. Soma Quran kabla ya kulala hakikisha unaoga kabla ya kusoma..

c. Mtafute sheikh akusomea dua, huenda Allah akakusaidia

d. Hakikisha hujadhulumu mali za watu..

Nakupa maksi kwa A.

B. Hii Quran anasoma sehemu yeyote tu? Vipi kama hajui kiarabu? Na una uhakika gani juu ya imani yake?

C. Allah huenda akamsaidia!!! (Sometimes hatoi msaada) Bora awe makini na maelezo atakayompa sheikh asije asimwelewe akamsomea albadili badala yake (Salat Al badil)

D. Unawezaje kuzuia kitu ambacho kilishafanyika? Au labda sijakuelewa hapa, ahakikishe hajadhulumu=ahakikishe hadhulumu?
 
Ushauri wangu: Kila mmoja anataka kukusaidia. Una hiari ya kuchagua ushauri unaodhania unakufaa, ila ni vema ukapima pros and cons za kila ushauri. Counsellors tunatoa ushauri wewe unachagua cha kufanya. Hakuna mganga awezaye kumtoa pepo maana yeye mwenyewe ni mtumishi wa mapepo hayo. Sanasana atakubadika agano gumu zaidi na ulimwengu wa giza. Una hiari ya kulichukua au kulikataa. Uko kwenye vita vya kiroho ambavyo si tu vinaanga,iza roho yako bali pia na nafsi na mwili wako na huna budi kuvishinda. Nisingependa kukuuliza dini yako maana hazijatusaidia tangu zilipoletwa na wanadamu. Ninamjua mmoja awezaye kukusaidia ambaye miaka takribani 20 alinisaidia nikiwa kwenye shida kama ya kwako na huenda mmbaya zaidi na sijajuta tangu hapo. Anaitwa Yesu. Yeye alikuja kuwafungua walioonewa na nguvu za shetani yakiwemo mapepo kama yanayokutesa. Nilijaribu kwenda kwa waganga hali yangu ikawa njema kwa muda lakini baada ya muda wakaendelea kunifuatlia ili kunitesa hadi pale nilipoamua kuyakabidhi maisha yangu kwa Yesu. Sikwenda kwa Yesu kujaribu kama anaweza, nilijua anaweza ila nilikuwa nataka niendelee kutumbua maisha. Nilipojikabidhi kwake akanipokea, nikamkabidhi shida zangu akanipa uzima wa mwili na roho na sasa kwa furaha namtumikia. Ushauri wenyewe: kanisa na kazi ya Mungu vimevamiwa na walafi na wanaojipenda. Hivyo basi ni vyema kuwa waangalofu na pale unapopata huduma. Tafuta mtumishi wa Mungu unayemheshimu umweleze shida yako. Ni muhimu hata kabla ya kwenda kwake iwapo umeamua kuyakabidhi maisha yako kwa Yesu kama Mwanawao alivyokushauri. Unaenda kwake kupata mwongozo wa kukua na maombezi. Kuna kipindi utaweza kujisimamia mwenyewe lakini kwa hali uliyonayo nakushauri umwone mtumishi wa Mungu. Huhitaji kuhonga ili tatizo lako liondoke. Huo ni ushauri wangu. UbarikiweApolonary;3424293]Inaweza kutokea wiki nzima mfululizo na kibaya zaidi baada ya kunyongwa naota ndoto ambayo inanionyesha kwamba kuna vitu vya kishirikina[/QUOTE]
 
Pole sana.
Ushauri wangu ni usali misa za kazi na jumapili bila kukosa, usali kabla ya kulala, usali baada ya kuamka, usali rozari kila siku pia uhudhurie sala za jumuia na wakati wa kulala ulale na rozari.
Mie nilikuwa na tatizo kama lako kwa sasa hakuna.
 
Nakupa maksi kwa A.

B. Hii Quran anasoma sehemu yeyote tu? Vipi kama hajui kiarabu? Na una uhakika gani juu ya imani yake?

C. Allah huenda akamsaidia!!! (Sometimes hatoi msaada) Bora awe makini na maelezo atakayompa sheikh asije asimwelewe akamsomea albadili badala yake (Salat Al badil)

D. Unawezaje kuzuia kitu ambacho kilishafanyika? Au labda sijakuelewa hapa, ahakikishe hajadhulumu=ahakikishe hadhulumu?

majibu
a. Kama hajui Quran inabidi ajifunze kwani ni kinga ya majanga mbalimbali ..

b. Allah huenda akamsaidia ..hatumlazimishi Muumba wetu..akipenda anasaidia (inategemea muombaji) naona hapo kiswahili ndio tatizo

c. Kama amedhulumu maana yake alipe kwanza kabla ya kumuuomba Allah, maana dua ya anayedhulum nadra sana kusikilizwa
 
majibu
a. Kama hajui Quran inabidi ajifunze kwani ni kinga ya majanga mbalimbali ..

b. Allah huenda akamsaidia ..hatumlazimishi Muumba wetu..akipenda anasaidia (inategemea muombaji) naona hapo kiswahili ndio tatizo

c. Kama amedhulumu maana yake alipe kwanza kabla ya kumuuomba Allah, maana dua ya anayedhulum nadra sana kusikilizwa

Ahaa kumbe!
 
Dawa mfupa wa nguruwe, wewe lala na mfupa wa nguruwe au, pia moshi wa bangi nao unawafukuza.
 
Kula huku umefakamia chipsi mayai (zege) na kokakola juu, utaacha kukabwa?
 
Kuna tatizo linaitwa PAROXYSMAL NOCTUNAL DYSPNEA (PND)
huwa linatokea kuanzia masaa matatu na kuendelea baada ya kulala .
Hii inatokana na maji kujaa kwenye mapafu na mgonjwa hukosa hewa na kujisikia kama amekabwa. Kwa kawaida hii hutokea kwenye watu wenye magonjwa ya Moyo.
Ningekushauri umwone dr unaweza kupata ushauri mzuri zaidi.
 
ukiwa umelala chali huku umeshiba sana,hizo ndoto huwa zinakuja sana...sijajua mechanism yake.....usishibe sana au lala upande au lalia tumbo wakati wa kulala

usiwe preocupied na mawazo ya kishirikina au hofu ya kukabwa na majambazi hasa during the day,yaepuke....sababu ndoto ni matokeo ya tunachowaza mchana...so ukiweza kuwa busy during the day kiasi mwili wako uchoke sana,ikibidi fanya mazoezi ....utalala vyema.
 
Apolinary...sikia! Sala ni muhimu sana kwetu binadamu kwani ni chakula cha roho. Ila pia kuna kitu kinaitwa mizimu nayo ni hatari na lazima izingatiwe. Kama wazazi wako wamefariki uliza ndugu waliobaki ufanyeje ili utekeleze matakwa yao la sivyo utaishia kuhama hama kila kukicha! Kingine, je uliwahi kumdhulumu mtu mali yake? Nakuuliza hivi manake kuna yanki mtaani alijiua miaka ya nyuma baada kuteswa kijinsia kila siku. Sikutishi ila huyu yanki alikuwa anajivinjari na mke wa mtu then jamaa alipogundua akamuonya lakini yule marehemu alinogewa na vya bure. Kwa hiyo mwenye mali akafanya yake ya jadi na yule yanki akaanza kuweweseka usiku kila akienda kulala. Jamaa akawa anapata mateso ya kila aina mpaka mwishoni akawa anafilwa kabisa akiamka asubuhi ****** una muuma na anakuta kinyesi kitandani, jamaa akachoka na mateso akahamua atangulie mbele ya haki na kuacha barua kwa nini alichukua ile hatua. Kwa hiyo bwana kama umemlalia mtu tafadhali omba msamaha wakati muda bado upo!
 
Jaman nimechoka kunyongwa usiku wa manane nikiwa nimelala mbali na hayo nyumba niyokuwa mwanzo nilihama nikidhan ni mikos ya hiyo nyumba, kumbe hata nilikohamia ndo hivyo hivyo nimeshauliza watu mbalimbali na walinipa majibu tofauti tofauti lakini mwishowe nikaambiwa njia pekee ni sala.nikawa nasali asubuh na jion kabla ya kulala lakin mambo yakawa ni yaleyale sasa sina hata hamu ya kuish kwa sababu naona sina msaada tafadhali nipen mawazo yoyote nitayafanyia kazi ili nami niweze kufurahia maisha kama wengine.NAWASILISHA!
Mtafute Mwingira wa Efatha ila usiende na mke wako!
 
Back
Top Bottom