Alvin Slain
JF-Expert Member
- Aug 30, 2011
- 6,375
- 3,655
Yesu ndie njia
angalia jinsi unavyolala[/QU mbona nalala tu vizuri au kuna jinsi ya kulala jamani
Pole sana.. Ushauri wangu..weka maisha yako kwenye mikono ya Mwenyezi Mungu kupitia imani au dhehebu lako. Mwangukie Mungu kwa Moyo wako wote na hata ukisali hakikisha unasali toka moyoni na siyo kuimba sala kama shairi. Jenga imani hadi uone unamwomba Mwenyezi Mungu kuwa kama yeye anataka wewe uendelee unyongwe kila siku na iwe hivyo..lakini si kama wewe unavyotaka. Kama unasali na unayo imani kwa Mungu basi haukuwa na haja ya kuhama ile nyumba ya kwanza. Pia kumbuka kama bado unaamini nyumba ya sasa bado ina mikosi basi hiyo ni dalili ya kuwa imani yako bado ni ndogo... Endelea kusali kwa dhati na Amini Mungu atakusaidia..otherwise, utaendelea kupigika na kusaga meno..[/QU yaani mpaka nikitembea njian nikikumbuka usiku ninavyongwa mwili unasisimka isitoshe saa ambayo ninanyongwa huwa niko macho kabisa lakin nakosa nguvu ya kupiga kelele
Yaani unanyongwa halafu tena bado u mzima! Wewe ni noma. Sinyongwi na kamba ndugu ila nahisi nanyongwa na mikono asubuh najikuta nimechoka sana kiasi kwamba siwez kuamka
Acha kulala umefunga madirisha na milango hadi hewa inaisha.
Hata kama unafungua kidogo, basi unajifunika gubigubi na mwisho unaishiwa hewa.
Pia angalia mto (Pillow) unayotumia maana inaweza kuwa ndogo na ukilala, unajibana kifua.
Ushauri wangu tu huu. Nenda kwa Dr. na usianze sana kuweka Mungu na Uchawi katika hili mara moja.
Mungu nisaidie na wewe unakimbia. Ila usiende kwa Sangoma bana.
Lala na bibilia pembeni.[/QU nimeshafanya hivo lakn bado nanyongwa
Baada ya kusali just amini kwamba maombia yamefanya kazi na hakuna zaidi ya Mungu,ukiendelea kufikiri kuhusu kunyongwa ndilo litakalo tokea mkuu!Lala na bibilia pembeni.[/QU nimeshafanya hivo lakn bado nanyongwa
Well said mkuu!Ndugu pole sana kwa yanayokukumba, wapo wengi ambao wameteseka kwa namna hiyo ila walipochukua hatua ya kubadili life style ya maisha yao wamewekwa huru kabisa.
Piga moyo konde chukua hatua zifuatazo na kwa kumaanisha ndani ya moyo wako utawekwa huru kabisa.
1.Amini katika Jina la YESU, Yohana 1:12, tubu dhambi zako zote popote pale ulipomkosea Mungu yeye ni mwaminifu atakusamehe kabisa, Isaya 1:18, Isaya 43:25, Zab 103:3,11,12, Mkaribishe ROHO MTAKATIFU awe ndani yako na kuyaongoza maisha yako, Wagalatia 4: 6,
2. Kwa kumwamini Bwana YESU, kutubu dhambi zako zote, na kumwalika Roho Mtakatifu kuwa ndani yako, unayo mamlaka na nguvu za Mungu kushinda ulimwengu wote wa giza. Muda wowote utakapo jisikia hiyo hali tumia mamlaka ya JINA LA YESU kukemea hizo nguvu za giza wala hazitakuwa na uwezo juu yako. LUKA 10:19, MARKO 16:17-18,
3. Jiwekee utaratibu wa kusoma na kutafakari neno la MUNGU ndani ya Moyo wako popote pale utakapokuwepo. Kumbuka ibilisi atakuletea hofu ya kukunyonga kama kawaida yake, chukua hatua ya kukemea hiyo roho ya hofu, na mtafakari Mungu na uweza wake katika Jina la YESU badala ya kuwaza hizo hofu za ibilisi. Wakolosai 3: 1-2.
4. Ukifanya maombi usifanye maombi legelege, fanya maombi ya vita ya kujikomboa kutoka katika utawala wa shetani, tumia silaha zote za UFALME WA MUNGU kumpinga na kumpiga shetani ili asikufuatilie. Uhuru haupatikani kilegelege ni kwa vita ndugu. 2-Wakorintho10: 4-5
5. Acha dhambi yoyote ile inayokuzinga ambayo ibilisi anaweza kuitumia kama njia ya kuendelea kukushambulia. Kumbuka MUNGU ni Mtakatifu na anawatetea wale wote wanaoishi katika njia zake. Wagalatia 5:20-21.
6. Hakikisha unahudhuria vipindi vya maombi na kujifunza neno la Mungu katika kanisa linalohubiri Injili ya kweli na kuamini katika karama zote za ROHO MTAKATIFU na si ubabaishaji.
Ndugu, Bwana Yesu akusaidie na kukuweka huru kabisa.