Nimechoka kudanganywa na vijana natafuta jibaba

Inabidi ujifanyie assessment kwanza kwa nini wanakutenda!? Nahisi tatizo kubwa utakuwa hauwezi kale kamchezo katamu ndo maana unataka wazee ambao wakishaenda goli moja tu hoi...au haujui ku~care upo busy sana kazi...
 
Inabidi ujifanyie assessment kwanza kwa nini wanakutenda!? Nahisi tatizo kubwa utakuwa hauwezi kale kamchezo katamu au haujui ku~care upo busy sana kazi...


hahahaha wewe hapo sita comment kitu.....
 
Je kama umeshakapiga biashara za usiku mm ntajuaje, na ww unataka kuwalelea watoto wngu??? si utawapa condom wapulize kama puto???
 
Je kama umeshakapiga biashara za usiku mm ntajuaje, na ww unataka kuwalelea watoto wngu??? si utawapa condom wapulize kama puto???

Naomba uelewe hapa mimi siombi kazi daycare.......kama watoto ntalea na mwenye nao lakini sio eti mimi ndio mlezi...i'm sory to say it!!! kwanza wewe uliyetaja habari za condom hapa ni mcharuko tu hata sikutaki mie....
 
Tehe tehe! Utamu wa mapenzi kuzinguana.We unasepa, yaani unamkimbia Mamba nchi kavu ukikimbilia mtoni? Unakimbilia mzee aliyeachika,kama na yeye kaachika kwa ukicheche na anajaa kwenye kipimo chako? Haya we!
 
Sasa dadaa yangu hebu mie niambie mdogo wako nifanyeje??? maisha mimi vijana wananitoa jasho kweli, anajifanya anakupenda kumbe huko nyuma anacheat kwa wengine, au huoni hii ni balaa dada

Hivyo vibabu vya age group hiyo ndivyo vinavyoongoza kwa cheating. Yaani wewe ukimpata umuombe Mungu tu hakuna formula yoyote hapo.

Afterall siku hizi 50 siyo mzee. Wazungu wanasema 'life begins at 50' . Maana pale jamaa ameshapeleka watoto shule na wao tayari wana kazi zao kwa hivyo yaliyobaki ni matanuzi tu.

He Godfrey Tajiri umenichekesha kweli kweli kuwaita above 50 'vimauti'. Sitaki hata kumwambia mume wangu maana yeye ni over 60 na bado ni moto wa kuotea mbali!
 
Naomba uelewe hapa mimi siombi kazi daycare.......kama watoto ntalea na mwenye nao lakini sio eti mimi ndio mlezi...i'm sory to say it!!! kwanza wewe uliyetaja habari za condom hapa ni mcharuko tu hata sikutaki mie....

ndo maana ,,,kijana mdogo ivyo unataka mzee maana huna market??? je kama kitu ipo loose (kitu haina bush)
 
ndo maana ,,,kijana mdogo ivyo unataka mzee maana huna market??? je kama kitu ipo loose (kitu haina bush)

Naona umetumwa, alokutuma kamwambie hujamkuta.........dada wa watu kaandika ili umuandikie huu upupu wako? wewe ndio huna market bana
 
Naona kila mtu anaponda tu ina maana JF kila mtu ni kijana humu eeeeh? Siwaelewi unajua!!
 
Naona kila mtu anaponda tu ina maana JF kila mtu ni kijana humu eeeeh? Siwaelewi unajua!!

We jaribu bahati yako, soma yaliyoandikwa hapa na uchanganye na akili zako halafu ufanye maamuzi unaweza kubahatika na kupata kile utakacho ili kutuliza moyo wako. Kila la heri.
 
Hapa kila mtu anashauri nipunguze vigezo hasa cha umri. Sasa itabidi ni edit angalau experience ipungue hata miaka 5 nyuma
 
Kwanza mapenzi niliyaanza nikiwa na age ya 25 huoni kama nina miaka miwili tu kwenye mapenzi???? pia hao nimewaacha mimi baada ya wao kuwa vicheche....hawajaniacha wao

u mgeni wa mapenzi pengine hawajapenda swaga zako.
 
Hapa kila mtu anashauri nipunguze vigezo hasa cha umri. Sasa itabidi ni edit angalau experience ipungue hata miaka 5 nyuma

Unaonekana una njaa kali sana, unataka awe na investment za nini na wewe umelalamika kutendwa hivyo unataka mapenzi ya kweli? What if ukampata wa age hiyo mwenye mapenzi lakini hana investiment?!
 
pole dadangu,mungu anaona kilio chako ila masharti ya huyo umtakae nae ni magumu,punguza kidogo!!mapenzi sio lazima hivyo viwepo

Mwambie bana utafikiri anataka apatiwe sanamu ya kuchongwa kwa vipimo! hahaha...................je unakwenda kuishi naye ama utamweka kabatini? hhahahahah.............no wonder vijana wanakutosa!:biggrin:
 
Unaonekana una njaa kali sana, unataka awe na investment za nini na wewe umelalamika kutendwa hivyo unataka mapenzi ya kweli? What if ukampata wa age hiyo mwenye mapenzi lakini hana investiment?!

Sasa mwanaume kwenye age ya 40's huna investment yoyote kweli utafaa kitu? ulikuwa unafanya nini ujanani? Ila mpatanishi nakuona kama unafaa vile
 
Mimi m ni mwanamke mwenye umri wa miaka 27 ninayejishughulisha na niko focused. Ninasikitika kusema kuwa toka niyajue mapenzi nimekuwa ni mtu wa kutendwa tu kwenye relationship na wapenzi ambao ni vijana. Nimeamua kutafuta baba mwenye umri kuanzia miaka 40-50 ambaye ni single (labda alifiwa na mke, au alipewa talaka). Awe tayari kupima HIV, dini awe mkristo, elimu ya chuo kikuu, asiwe mfupi ila mrefu wa wastani, asiwe na kitambi ila awe na mwili wa wastani, awe anayefanya mazoezi ya viungo mara kwa mara (sio lazima kila siku), awe anajishuhulisha na kazi au biashara, kwa umri huu awe ameshafanya baadhi ya investments za maisha. Atakaebahatika atapata mapenzi motomoto na ya ukweli.. Mwenye vigezo hivyo atakapopatikana dirisha la usajili litafungwa muda wowote.

Niko zaidi ya serious katika hili.
  1. Mimi ni mwanamke ninayejishughulisha na niko focused - Unajishughulisha na nini na uko focused kwenye nini?
  2. Awe tayari kupima HIV - Wewe umeshapima?
  3. Dini awe mkristo - Wewe dini gani?
  4. Elimu ya chuo kikuu - Wewe elimu yako level gani?
  5. Asiwe mfupi ila mrefu wa wastani - Wewe umbo lako likoje?
  6. Asiwe na kitambi ila awe na mwili wa wastani - Wewe huna kebabs?
  7. Awe anayefanya mazoezi ya viungo mara kwa mara (sio lazima kila siku) - Wewe unafanya mazoezi? Mara ngapi kwa wiki?
  8. Awe anajishuhulisha na kazi au biashara - Wewe unajishughulisha na nini?
  9. Kwa umri huu awe ameshafanya baadhi ya investments za maisha - Wewe ushafanya investments au plan yako ni nini? Usikute umeshindwa kupanda unataka kuvuna vya wengine.
  10. Atakaebahatika atapata mapenzi motomoto na ya ukweli - Kama hao vijana wawili walikuwa wanapata mapenzi motomoto kwa nini wamekuacha? Mwanaume makini lazima atataka kujua hiki. Unatoa mapenzi moto moto lakini unatemwa? BTW mapenzi moto moto ndio yapi hayo?
  11. Mwenye vigezo hivyo atakapopatikana dirisha la usajili litafungwa muda wowote: Na ukimpata mwenye vigezo hivyo lakini akakutenda vile vile? Utafungua tena dirisha la usajili?


Kasome hii thread kwanza halafu urekebishe post yako: https://www.jamiiforums.com/love-connect/138719-natafuta-mchumba-wa-kuolewa-kuoa.html. Otherwise, kama kuna mbaba wa maana mwenye hizo sifa ulizozitaja wala hataangaika na wewe.
 
Nakadori! Vigezo vyote ulivyoviweka sina taabu navyo so far nakwazika na kikwazo cha elimu ya chuo kikuu! Hapo ndipo napokuona hauko serious! Kwani kua graduate kunahusika nini na mapenzi pia maisha? Hivi how many couples susceed in their married's life who not graduate? Ingekua hivyo basi ndoa zote zingekua za wasomi! Mf. Mie naekuandikia hapa misifa yote uitakayo ninayo lakini kiwango hicho cha elimu sinacho, hata hicho kingreza changu cha kidhungu hapo juu kama unavyokiona kibovu nimejifunzia mtaani, cha kuzugia kama humu Jf, Fcbk e.c.t manaake humu bila kingereza mama utanyanyasikaje? Shortly my dear fellow am beg u hounestly plz reduce you are Carriculam Vitae to the candidates who need to perticepate in this annouce tender.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom