Nimecheza Filamu na inatoka wiki ijayo

ndio huyo huyo wa Mjomba Mpoto...

kuweka subtitle sio sawa na kutumia kiswahili

ukiita fila yako mfano 'asiesikia la mkuu.'.....mtu anaejua kiswahili
anapata ujumbe moja kwa moja....

Hebu nitafutie kiswahili cha hiyo tittle ya "In the line of death"

 
Duh, hapo sijakuelewa, kwa hiyo filamu yetu haifai ama!?

siwezi sema haifai kwa sababu sijaiona
lakini jina la kiingereza limeshani punguza hamu ya kuitazama

filam zinaendana na utamaduni.....

na utamaduni lugha pia inahusika......kuna methali na misemo ambayo ikitumika unaelewa
alietunga filam anamaanisha nini.......
 
Wewe kweli aklili zako Mufilisi, nyie ndo tunawaita Ma-Pirates. sie tunaumia kushoot muvi nyie mnasubiri ku-burn na kuangalia bure. ndio maan wasanii wengi hawafaidi jasho lao

Hata nikinunua kwa wamachinga na wenyewe wanakuwa wamechakachua, ni bora ni-burn mwenyewe ili nisiwafaidishe hao wachakachuaji.
 
siwezi sema haifai kwa sababu sijaiona
lakini jina la kiingereza limeshani punguza hamu ya kuitazama

filam zinaendana na utamaduni.....

na utamaduni lugha pia inahusika......kuna methali na misemo ambayo ikitumika unaelewa
alietunga filam anamaanisha nini.......

Tumeshafanya reseach, kwa hapa Bongo Muvi ukiipa jina la kiswahili inapoteza mvuto na haiuziki kama zile muvi zenye tittle za Kiingereza.........
 
Hata nikinunua kwa wamachinga na wenyewe wanakuwa wamechakachua, ni bora ni-burn mwenyewe ili nisiwafaidishe hao wachakachuaji.
Kuna software ambayo ina protect watu ku-burn muvi zetu, imekula kwako majombaaa
 
nimekukubali kwa ukweli wako 2 mzazi. Bt tembelea hata tht wakakufue ili
uwe duki
 
Hongera sana kaka!
Suala la yeye kufanya sanaa kwa sababu ya njaa halitofautianni na mkurugenzi anayefuatwa nyumbani asbh na kurudishwa jioni wote wanafanya kazi kwa sababu ya maisha!
 
USHAURI:

Kwa utashi ulioonyeshwa na The Boss kwenye uzi huu na uwezo aliouonyesha kwenye kutoa miongozo....
Nadhani Ndugu tegelezeni ni busara kwa wewe kumchukua huyu Mkuu kama Director kwa part 2 ya movie hiyo,
Sababu tuanjua bongo movie zetu lazima ziwe na part 2.
 
Huyo mwandishi wa kunihoji mimi ni lazima atume CV yake kwanza nijue kiwango chake cha elimu. Siwezi kuhojiwa na Makanjanja


Nimeangalia comment za watu and how you reply.. Just be careful with your attitude unaweza usifike mbali.. Punguza mkuu naona umeshajiweka kwenye level ambayo hujafika where on earth mwandishi wa habari anaomba interview na anaombwa CV yake kwanza.. In most cases bongo waigizaji ndo wanatafuta magazeti tena ya udaku yawape coverage kwani most customers wa hizo home videos zenu ndio wanasoma hayo magazeti hivyo unayahitaji...
 
Hongera kwa mawazo mbadala...ila kuhusu kuiangalia hiyo movie kwa upande wangu sijui.

Kila ninapotaka kuangalia movie za kibongo hua naishia mwanzoni.

Kuna vitu kama vile sound track,mwanga,sauti zisizopangiliwa, watu wasiobeba na kuwakilisha uhalisia (mtu akiigiza umasikini, anakuwa na sura ya kutia huruma, nani kasema masikini hana furaha?) na wengi wao wanaigiza kuwa wanaigiza vitu hivi huniboa mapema, ni movie chache sana naweza kuziangala moja ni kama hiyo ya Irene Sanga.

Pia watunzi wengi hawawapendi wahusika wao wote kwa usawa kulingana na nafasi zao. Utaona kabisa nyota wa filamu husika ameandaliwa mazingira yote ya kupendwa na audience, wakati washiriki wengine wanapotezewa hata maana ya uwepo wao kati filam husika.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom