Nimecheza Filamu na inatoka wiki ijayo

Tegelezeni

JF-Expert Member
Dec 31, 2009
268
124
Wanajamvi wenzangu, katika kupambana na hali ngumu ya maisha, nimejiingiza kwenye fani ya uigizaji, na filamu yangu ya kwanza kushiriki inatoka wiki ijayo, inaitwa In the Line of Death…
Katika filamu hiyo nimecheza kama kubwa la maadui na nimeuwa kinyama kama yule mcheza muvi wa Kimarekani aitwae Bill Drago. Naomba wadau muitazame kisha munipe maoni yenu.
 
Watakaohitaji copy za muvi hiyo wani-PM nitawaelekeza pa kuzipata. Naomba ushirkikiano wenu jamani tupende vyakwetu kwani mcheza kwao hutunzwa!
 
kwanza hongera kwa kuwa mkweli
kuwa umeamua kucheza filam kutokana na ugumu wa maisha....na sio kwamba labda ulikuwa na interest before...

mpaka hapo nakupa pointi
subiri tuitazame na tukupe maoni yetu.......
 
@ The Boss-Huu ugumu wa maisha tulio nao unaweza kufanya hata yasiyotarajiwa!
 
pole saana
hauko peke yako.....

labda nikuulize wewe una interest vipi labda??????

bila ugumu wa maisha ungependelea kufanya nini?????

Mimi kwa taaluma ni Afisa Ugani lakini hiyo fani hailipi kabisa, nikaona nijaribu haya mambo ya filamu labda nitatoka
 
act movie za mapilau si hizi za kujipakaoaka poda bana..vipaji mnavyo kutumia hamtaki
 
kwanza hongera kwa kuwa mkweli
kuwa umeamua kucheza filam kutokana na ugumu wa maisha....na sio kwamba labda ulikuwa na interest before...

mpaka hapo nakupa pointi
subiri tuitazame na tukupe maoni yetu.......

Lakini mkuu, mbona maswali yamekuwa mengi, hivi unataka kuniungisha kwa kununua filamu yangu au ndio umeshaanza darasa la ushauri nasaha. sikuelewi bana!
 
Mungu atunusuru na filamu za kibongo. Yaani kumbe si suala la art, talent wala inspiration. Watu wanataka ugali tu, yaani tusiwalaumu matrafiki kila mahali uozo tu
 
Mimi kwa taaluma ni Afisa Ugani lakini hiyo fani hailipi kabisa, nikaona nijaribu haya mambo ya filamu labda nitatoka

afisa ugani ni nini?
nifafanulie please.....

nataka kukushauri kuhusu filam..lakini kwanza nieleweshe kuhusu maafisa ugani,why hailipi...???????
 
afisa ugani ni nini?
nifafanulie please.....

nataka kukushauri kuhusu filam..lakini kwanza nieleweshe kuhusu maafisa ugani,why hailipi...???????

Maafisa Ugani ni wale watu wa wanaosimamia Kilimo Kwanza huko vijijini
 
afisa ugani ni nini?
nifafanulie please.....

nataka kukushauri kuhusu filam..lakini kwanza nieleweshe kuhusu maafisa ugani,why hailipi...???????

Labda nikuulize swali, hivi itakuchukua miaka mingapi kufanya kazi serikalini na kupata zaidi ya milioni 20?
Kwa taarifa yako ukikomaa kwenye Game la Muvi za kibongo, ndani ya mwenzi mmoja unaweza kujipatia milioni zako 20 na ushee?
 
hongera sana mkuu,maisha ni kutafuta na wala sio kutafutana,umeamua jambo la mbolea kabisaa kutumia kipaji kupata ridhiki

ikiwa tayari basi mimi nitakuunga mkono mkuu
 
Mimi naanza kukupongeza japo move sijaliona hongera sana
pia lazima ujue hata hao wamarekani haswwa weusi wamefanikiwa baada ya msoto mkali wa masiha
marehemu babu aliniambia ukiwa na njaa akili nayo inafanya kazi
jitume ugumu wa maisha ulio kuwa nao sasa itakuwezesha kujikwamua hapo baadae,achana na wanategemea maisha bora bila kujituma
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom